Simu ya Infinix Hot 30i ni infinix mpya iliyotoka pamoja na toleo la Infinix Hot 30
Tofauti ya Hot 30i na Hot 30 ni nguvu ya kiutendaji ambapo hot 30 ina memori kubwa na kioo kizuri
Ila kiutendaji infinix hot 30 inaizidi kidogo mwenzake
Ndio maana bei ya infinix hot 30i inaikaribia kidogo hot 30
Ukisoma sifa zake zote utagundua utofauti mdogo baina ya simu hizi mbili
Bei ya Infinix Hot 30i Tanzania
Infinix ya GB 128 kwa hapa nchini inapatikana kwa bei ya shilingi 315,000/=
Kikawaida matoleo ya hot yenye harufi “i” huuzwa kwa bei nafuu zaidi
Hii ipo tofauti kwani uwezo wake ni mkubwa na unaizidi simu ya hot 12i ambayo unaweza ipata kwa laki mbili na nusu
Hivyo bei kubwa isikushangaze, kinachopaswa kujiuliza ipi ya kuichukua kati ya matoleo mawili ya hot 30
Jibu linategemea na nini unapendelea kwenye simu, fuatilia sifa zake uelewe
Sifa za Infinix Hot 30i
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 128GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera moja
|
Muundo | Urefu-6.56inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 315,000/= |
Upi ubora wa Infinix Hot 30i
Simu inatumia mfumo wa memori wenye kasi kubwa ya kusafirisha data
Inadumu na chaji muda mrefu
Utendaji wake ni wa kuridhisha
Ina kioo chenye refresh rate kubwa inayofanya simu kuwa laini wakati wa kuperuzi
Inakuja na nafasi kubwa unayoweza kuhifadhi vitu vingi
Urefu wake ni wa wastani
Mambo mingine yana ubora wa kawaida kama utakavyoona kwenye maelezo yaliyopo
Uwezo wa network
Simu inasapoti mtandao mpaka wa 4G aina ya LTE Cat 7
LTE Cat 7 ina kasi ya juu kabisa ya 300Mbps sawa na 37MB/s
Hii inamaanisha kama mtandao wa simu unakupa kasi hii basi faili la 37MB linaalizika kudownload kwa sekunde moja
Tanzania, mitandao ya simu za mkononi hawatoi kiwango hiko cha spidi
Hata hivyo kutokana na gharama za intaneti kuongezeka unaweza usifurahie kasi hii hata kama ikiwepo
Pamoja na kuwa simu imetoka mwaka 2023 ila haijaja na 5G
Kuna simu za 5G nyingi za chini ya laki tano ila hapa Infinix wamejisahau
Uzuri kuwa mitandao ya Vodacom na Tigo wameanzisha hii huduma japo haijasambaa sana
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 30i
Kioo cha infinix hot 30i ni cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz
Resolution ya kioo sio kubwa kwani kina 720 x 1612 pixels, baadhi ya zitaonekana kuwa kubwa sababu ya ujazo mdogo wa pixels
Ila ukiwa unacheza gemu utafurahi kwa sababu ya kiwango kikubwa cha refresh rate
Ikiwa kubwa inafanya simu ni nyepesi ni skrini kubadilika kwa unadhifu pindi unapotachi
Hasara ya refresh rate kubwa ni kutumia umeme mwingi wa betri
Hata hivyo hii simu betri yake ni kubwa
Unagavu wa kioo unafika nits 500, kwenye jua kali kioo kinaweza kisionyeshe kwa mwanga mwingi
Nguvu ya processor Unisoc T606
Ni kawaida kwenye simu za android kukuta chip zilizotengenezwa Taiwan(mediatek) au Marekani(Snapdragon)
Unisoc ni kampuni ya china, chip zake nyingi huwekwa kwenye simu za daraja ya chini ama la kati
Utendaji wa Unisoc T606 unaenda na kuzidiwa kidogo na chip ya Helio G88 iliyopo kwenye Tecno Spark 10 Pro na Hot 30
kwenye app ya kupima nguvu za processor ya geekbench, hii processor ina alama 311
Hivyo sio chip nzuri kucheza magemu yanayohitaji nguvu kubwa kama PUBG Mobile 2018
Kiujumla ina core(sehemu) nane ambapo core zenye nguvu zaidi zinatumia muundo wa Cortex A75
Kitu kikubwa zaidi utakachonufaika na Unisoc T606 ni ulaji mdogo wa umeme kwa gharama ya utendaji
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya infinix hot 30i ina ukubwa wa 5000mAh
Na kasi ya chaji yake ni wati 18
Kasi ya chaji inaweza kujaza betri kwa muda unaozidi masaa mawili
Ukiwa unatumia intaneti muda wote bila kuzima data hii simu inaweza kukaa masaa zaidi ya 15
kwa mtumiaji asiyetumia intaneti mara kwa mara atashuhudia ukaaji wa muda mrefu
Hii ni sehemu nyingine ambao 30i inazidiwa na hot 30 ambayo ina chaji ya wati 33
Ukubwa na aina ya memori
Simu inatumia memori aina ya UFS 2.2 ambayo kasi yake ya kusafirisha data 1200MBps
Kasi hii inafanya simu kuwaka kwa haraka na appliksheni kufunguka kwa sekunde chache
Pia Hot 30i ina toleo moja tu lenye memori ya GB 128 na RAM GB 4
Hata kama memori itajaa kuna sehemu ya kuongeza memori kadi tofauti na simu za siku hizi za madaraja ya juu
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 30i
Bodi ya Infinix hot 30i ni ya plastiki, plastiki huwa ni rahisi kupauka rangi ukilinganisha na simu zenye vioo
Kuimarisha ubora utakaokaa muda mrefu ni vizuri ukawa unaitumia kavaa mara kwa mara
Simu haina viwango vya IP hivyo inamaanisha haina uwezo wa kuzuia maji pindi ikizama kwenye kina kikubwa
Umakini unahitajika hasa unapotumia kwenye mvua au unapoenda kuogelea
Pia ina kimo cha wastani na sio nzito sana
Ubora wa kamera
infinix hot 30i ina kamera mbili na haina ulengaji wa PDAF
Kamera kubwa ina megapixel 13, wakati kamera ya pili sio ina lenzi ambayo haipigi picha (yaani ni depth)
Kwa kuangalia haraka ni kuwa mfumo wa kamera sio mzuri sana
Sio kwa sababu ina megapixel 13, hapana, kiwango cha 13MP ni kikubwa kutoa picha nzuri
Ila ukosefu wa teknolojia ya pdaf ni ishara kuwa hii kamera ni ya kawaida sana
Upande wa video simu inaweza kurekodi video za full hd(1080p)
Na haina OIS kwa ajili ya kutuliza video wakati ukirekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Ungetaraji kuwa simu yoyote ya mwaka 2023 inafaa ije na Android 13
Ila kwa infinix inakuja na Android 12 na mfumo XOS wa zamani kidogo yaani XOS 10.6
Hakuna tofauti kubwa sana kati Android 12 na 13
Ila simu kuwa na mfumo zaidi inapendeza
Mfumo mpya unaipa simu thamani kubwa na muda mrefu wa kutumia appliksheni mbalimbali bila shida
Washindani wa Infinix Hot 30i
Mshindani wa kwanza na mkubwa zaidi kwa hii simu ni Tecno Spark 8C
Spark 8C ina mfanano wa kila kitu mpaka utendaji ila tecno ina bei ndogo zaidi
Mshindani mwingine ni Samsung Galaxy A04 na Redmi Note 10 5G
Bei ya simu za samsung na redmi ni chini ya laki nne kwa sasa
Faida ya hot 30i ni kuwa inakuja na memori kubwa ila mambo mengine yanafanana
Hata pixel 3 iliyotumika ni mshindani wa hii simu
Neno la Mwisho
Infinix Hot 30i ni kama mbadala wa toleo la infinix hot 30
Kwa maana kama bajeti imebana sana unaweza ukasogeza siku
Ugumu utakaopata hii simu ni kwenye bei kwani inaipeleka kwenye ushindani mkali na matoleo mengi ya laki nne
Maoni 11 kuhusu “Bei ya infinix hot 30i na Sifa Zake Zote”
Kuna baadhi ya website znasema infinix hote30 ina camera ya MP50 nisaidie napata stomfaham kwenye hili
Pila ni oppo gani camera yake ina MP50 na bei yake ni ipi
Hii inayozungumziwa hapa ni hot 30i sio hot 30,na oppo yenye kamera ya 50MP ni oppo Reno 8
Vip juu ya finger print iko mbele ya kioo au pemben mwa sim
IPO nyuma
Nikushukur kwa kunielekeza kuitambua hot 30i
Bei
Bei imeanishwa huko juu
Je kati ya infinix hot 30i na spark 10C ipi bora
Hizi zinaendana Tu kiutendaji
Nimenunua Infinix hot 30i lakini mtandao wa halotel haufanyi kazi inasoma imegency call only tatizo Nini
Hot 30i ina masafa pia ya halotel kuna uwezekano kukawa na tatizo kwenye line yako. Jaribu kuweka laini nyingine ya halotel kama inakubali ama la