Simu ya Infinix Hot 30 imeingia sokoni mwishoni wa mwezi wa tatu 2023
Ni simu mpya ya infinix 2023 ya daraja la kati yenye utendaji wa wastani na inayoweza fanya kazi vizuri kwenye vitu tofauti tofauti
Bei ya Infinix Hot 30 kwa Tanzania ni zaidi ya laki nne
Bei yake inachagizwa zaidi na kuja na kiwango kikubwa cha memori na pia utendaji wa kuridhisha kama utakavyoona kwenye hii makala
Bei ya Infinix Hot 30 ya GB 256
Kwa maduka ya hapa Tanzania bei yake ni shilingi 465,000/=
Hii ni infinix ambayo ipo tofauti na simu kama infinix smart 6 kwenye maeneo mengi
Ukianzia chaji,kioo, kamera na nguvu ya processor utaona sababu za msingi kwa nini bei ya simu inakaribia laki tano
Ndio maana hata ukiangalia ubora wa picha, picha zinatoka vizuri japo si kwa kiwango kama cha simu za samsung galaxy s23 au iphone 14
Ila kwa kuzingatia bei simu inaendana na ubora wake
Na bei hiyo pia inaipeleka simu kwenye ushindani na simujanja kutoka Tecno, Redmi, Samsung na Motorola
Sifa za Infinix Hot 30
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 465,000/= |
Upi ubora wa Infinix Hot 30
Hot 30 ina kioo chenye refresh rate kubwa kinachofanya simu kuwa nyepesi unapotachi
Ni simu ndefu hivyo skrini inakuwa nzuri zaidi kama unapenda kusoma vitabu
Inakaa na chaji muda mrefu na chaji yake inajazaa betri kwa muda mfupi
Ina utendaji wa wastani unaofaa kwa kazi nyingi za kwenye simu
Inakuja na memori yenye uwezo wa kuhifadhi mafaili mengi
Kamera yake inatoa picha nuzri hasa kwenye mwanga mwingi
Uwezo wa Network
Mtandao unasapoti mpaka mtandao wa 4G pekee
Kwani processor iliyotumika haisapoti 5G
Inatumia 4G ya LTE Cat 7 ambayo kasi yake ya kupakua vitu ni 300Mbps
Kwa maana kama unapakua gemu la Call of duty lenye 2GB simu itamaliza kudownload kwa sekunde 55
Mitandao mingi hapa Tanzania huwa ina spidi ya 4G ambayo ni ngumu kufika 100Mbps
Hivyo uwezo wa network ya 4G wa hii infinix unaweza usinufaike nao
Ila kwa 5G inawezekana japokuwa inapatikana sehemu chache
Pia 4G yake ina masafa yote ya mitandao ya simu iliyopo nchini
Hakuna mtandao utakaogoma kwenye intaneti
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 30
Infinix Hot 30 inakuja na kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 1080×2460 pixels(full hd+)
LCD huwa havina ubora mkubwa kwenye usahihi wa rangi ukilinganisha na kioo cha amoled
Ila lcd ikiwa na resolution kubwa muonekano wa vitu unakuwa mzuri kama ilivyo kwenye hii simu
Na pia skrini yake ina refresh rate inayofika 90Hz
Ukiwa unaperuzi(kuscroll) kioo kinakuwa na kasi ya haraka na muonekano wenye kuvutia macho
Simu inakupa chaguo la kuzima hii refresh rate kwa sababu refresh rate kubwa hula chaji nyingi
Uangavu wa kioo ni nits 500, kwa maana ukiwa kwenye jua kioo kinaweza kisitoe mwanga mkubwa wa kuonyesha vitu vizuri
Nguvu ya processor MediaTek Helio G88
MediaTek Helio G88 ndio chip inayoipa nguvu simu ya hot 30
Utendaji wake sio mkubwa kama processor ya Dimensity 700 ila utaweza kufanya vitu vingi unavyovihitaji
Utendaji wake wa kiwango cha kati unasababishwa na sehemu yenye nguvu(zipo mbili) kutumia muundo wa Cortex A75
Wakati core kwa ajili ya kazi zinoumi nguvu ndogo zipo SITA.
Hata hivyo magemu mengi yanacheza vizuri ila Yale makubwa utalazimika kupunguza ubora wa graphics.
Vinginevyo unaweza kukuta simu inapata joto Sana na pia kucheza gemu kwa kukwama
Mfano wa magemu hayo ni genish impact na call of duty
Uwezo wa betri na chaji
Chaji inayokuja na Tecno Ina Kasi ya wati 33
Chini ya masaa mawili simu inajaa kwa 100% kutokana 0%
Ukiwa huitumii Sana betri yake inaweza kudumu mpaka siku mbili
Ukiwa muda wote unatumia intaneti na basi inaweza chukua mpaka masaa 15 kuisha chaji.
Sababu ya ukaaji wa chaji ni kuwa betri Ina ukubwa wa 5000mAh na chip ya simu haitumii nguvu kubwa Sana kufanya kazi zake na pia uangavu wa kioo sio mkubwa
Ukubwa na aina ya memori
Aina ya memori iliyopo kwenye hii simu ni eMMC 5.1
Huu ni mfumo kwa Sasa hautumiki na simu mpya nyingi kwani usafirishaji wake wa data sio mkubwa kama mfumo UFS 2.1 na kuendelea
Kama unawasha simu ya UFS 2.1 na ya eMMC 5.1, basi ya UFS itawahi kuwaka
Kuna toleo moja tu la Infinix upande wa memori ambayo Ina GB 256 na RAM 8
Simu inarushusu kuongeza kiwango Cha RAM mpaka GB 16
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 30
Bodi ya Infinix hot 30 Ina muundo wa flati ikiwa ni plastiki upande wa nyuma
Hivyo basi ni muhimu kutumia kava na uzuri utakuta kwenye box
Simu Haina viwango vya IP vinavyoashiria uwezo wa kuzuia maji kupenya kama ikizama ndani ya maji
Pia ni muhimu kuweka skrini protekta kulinda kioo Cha simu kwani Haina vioo vya gorilla
Ubora wa kamera
Idadi ya kamera za Infinix hot 30 ni mbili ila kiuhakisia ni kamera moja tu inyopiga picha
Kwa sababu kamera ya pili yenye lenzi ya depth huwa haipigi picha Bali kwa ajili ya kupima kitu kinachopigwa picha na umbali wa kamera
Kamera kubwa inakuja na megapixel 50 na ulengaji wa AF (sio PDAF)
Muonekano wa picha ni mzuri japo kuna kiwango Cha noise kwa mbali
Ila usahihi wa rangi sio wa kiwango kikubwa(rangi nyeusi inkuwa n mng’ao usioendana na m
Ubora wa Software
Hii infinix inakuja na android 13 na mfumo wa XOS 12.5
Hapa kuna maelezo kuhusu mfumo wa android 13
Moja ya applikesheni utakayoipata kwenye hii simu ni AI Gallery inayokupa uwezo wa kuhariri picha kwa kutumia teknolojia ya artificial inteligence
Mfumo wa AI unasaidia kufanya editing kwa kuzingatia rangi sahihi za vitu unavyovihariri
Ila simu inakuja na app nyingi(bloatware) ambazo nyingi sio muhimu kwako
Kuna baadhi zinaweza kutoka lakini nyingine hazitoki
Washindani wa Infinix Hot 30
Kuna simu nyingi za hivi karibuni na za miaka ya nyuma kidogo ambazo unapata kwa bei ya hot 30 au zenye uwezo sawa na kuzidiana kidogo
Kuna simu ya Xiaomi Poco M4 5G ambayo ina 5G na utendaji unaizidi hii simu, bei ya poco kwa Tanzania ni shilingi laki nne na thelathini
Mshindani mwingine ni Samsung Galaxy A14, hii ina kamera tatu ikiwemo kamera ya kupiga eneo pana yaani ultrawide ambayo haipo kwenye hot 30 bei yake ni chini ya laki nne na nusu
Simu janja nyingine Redmi Note 11 yenye utendaji unaoendana na hii simu ila redmi inakuja na kioo cha amoled, kamera nne na pia uwezo wa kuzuia vumbi na maji ya kiwango cha kunyunyuzia
Wakati redmi note 11 bei yake ni shilingi laki nne
Pia mshindani mwingine ni Simu ya Tecno Pova 3
Neno la Mwisho
Infinix hot 30 ni toleo zuri kwa walio na bajeti ndogo
App karibu zote zitafanya kazi, na anayetafuta simu inayokaa na chaji masaa mengi hii simu itamfaa
Ila kama unahitaji vitu vya ziada kwa bajeti hii washindani wake wanaweza kuwa mbadala
Maoni 30 kuhusu “Bei ya infinix hot 30 na Sifa Zake Muhimu”
Nimefurahi kusikia sifa ya Infinix hot 30. Nitakuwa mteja wenu mzuri.
Iyo inifinx hot 30 inauzwaje
Bei gan iyo
Bei mbona inaonekana hapo kiongozi
Mbona mtaani zinauzwa Bei kubwa tofauti nayakwenu au hakuna Bei elekezi
Bei kubwa zaidi ya hapo sio sahihi
Changamoto hiyo ni bei ambayo utaikuta kwenye maduka yenyewe YA Infinix, tofauti na hapo bei lazima iwe juu. Mathalani mfanyabiashara toka Mtwara akija chukua dar, akileta hulu bei haiwezi kuwa ya 400k
Hiyo ni kweli lakini Kwa ulimwengu WA sasa unaweza nunua kitu chochote kutoka eneo lolote Kwa bei isiyotofautiana Sana
Kwa hapa dar naipataje Hii nimeipenda
Infinix nyingi huwa zinaleta matangangazo mengi wakati umewasha data. Je’ hi hot 30 mmeliondoa hilo?
Hii ni moja ya changamoto za infinix
Nimoja yasimu nzuli Sana lakn kuipata kwa Bei hio kwetu nishida Sana
Hakika ni simu nzuri sana hata ndiyo ninaitumia
Ni nzuri
Kwa mkopo zinapatikana
Inawezekana
Punguzeni bei tuchukue
Iko vizuri
Ni nzuri nmeipenda na nahitaji naipaje?
Naomba maelekezo zaidi kuhusu apatikanaji wake Kwa bei rahisi kidogo
hongera sana nauliza je kuna infinix laini moja 2u au ndy lazma lain 2
Sijawahi bahatika kuziona
Nimesoma ni kwa ujmla iko vizur sana
Dahh jamani naenjoy sana nimeichikua jana lakini nilibahatisha kwa laki 3na elfukumi. Iko vzr sn pia chaji inatunza sana chaji nzuriiii
Pia inatachi nyepesi mno pia memory yake kubwaaaaaaaaa. Hata kuitazama kwa macho dah rahaaaaaaaa
Natafuta Infinix hot 30i GB 128 Kwa laki 2 na 30 naweza pata
Haiwezekani kiongozi
Infinix hot 30i Ram 8gb ROM 256 naweza pata kwa 400,000?
Nimeikubal.
Kwa Sasa ni Bei gani