Kwenye mlolongo wa matoleo ya Google Pixel 8, Google Pixel 8a ndio ina bei ndogo zaidi
Bei ya Google Pixel 8a ya GB 128 ni shilingi za tanzania milioni moja laki tatu na nusu
Inashangaza lakini milioni 1.35 ni bei ndogo ukilinganisha na Google pixel 8 au matoleo ya Samsung Ultra
Maeneo makubwa yenye ubora zaidi kwenye hii simu ni
- Kamera
- Kioo
- Nguvu ya processor
- Ukaaji wa chaji
Kuna vitu vichache vinavyokosekana kwenye hii ila vipo kwenye matoleo mengine ya google pixel 8, lakini kwa kiasi kikubwa hakuna tofauti kwenye sifa nyingi
Sifa za Google Pixel 8a
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,350,000/= |
Uwezo wa network
Google Pixel 8a ni simu inayosapoti mtandao mpaka wa 5G
Inasapoti aina zote za 5G ikiwemo za masafa ya kati yanayopatikana hapa nchini
Upande wa 4G, ina LTE Cat 24 ambayo kasi yake inafika 7300Mbps
Yaani kama unapakuwa muvi ya GB 1, simu itamaliza kupakuwa faili ndani ya sekunde moja
Kasi hii inategemea kama mtandao wa simu una miundombinu ya namna hiyo
Kwa Tanzania ni nadra kupata kasi hii upande wa 4G
Ubora wa kioo cha Google Pixel 8a
Kioo cha google pixel 8a kimeundwa kwa teknolojia ya oled
Oled huundwa kwa matirio yanayotoa mwanga yenyewe pindi umeme ukipita bila kutegmea taa za LED
Inafanya simu kuwa na utajiri mkubwa wa rangi, ukizingatia resolution yake ni kubwa ya 1080 x 2400 pixels
Pia refresh rate inaweza fika hadi 120Hz, na mwangaza mkubwa unaoenda mpaka nits 2000
Ukiwa juani kioo kitaonekana vizuri tu
Ila kwenye kioo google pixel 8a imepungua baadhi ya vitu kama vile hdr10+ na pia hiki sio cha ltpo oled
LPTO oled hudhibiti matumizi ya refresh rate yenyewe ili kupunguza ulaji wa chaji
Nguvu ya processor ya Google Tensor G3
Google Pixel 8a inatumia chip ya Google Tensor G3 kufanya kazi zake
Tensor G3 ina idadi ya core zipatazo tisa tofauti na processor za mediatek, snapdragon na apple bionic
Lakini hili halifanyi chip ya google kuwa na utendaji mkubwa kuliko Snapdragon 8 Gen 3 ya Samsung Galaxy S24 au Apple A17 Bionic ya iPhone 15 Pro
Hata hivyo nguvu yake ni kubwa ya kufanya chochote bila shida kwenye gemu
Hata ukiangalia alama za app inayopima nguvu za processor utaona kuwa alama zake ni kubwa
Hivyo kwa mpenzi wa magemu ataweza kucheza gemu za kila aina pasipo na shida
Uwezo wa betri na chaji
Betri yake ina ukubwa wa 4492mAh, haijafika mAh 5000 kama ilivyozoelezeka
Lakini inakaa na chaji masaa mengi kama tu simu zingine
Simu inasapoti chaji ya wati 18, kwa chaji ya wati 18 simu inachunkua dakika 129 mpaka kujaa
Sio spidi ya kuridhisha ukilinganisha na simu ya Samsung Galaxy S24 inayojaza betri kwa dakika 75 tu
Mbali na chaji ya kutoridhisha ila ukaaji wa chaji unaridhisha
Kwani kwa matumizi ya hapa na pale inastahimili mpaka masaa 11
Kwa kucheza gemu pekee muda wote inachukua masaa saba (sio mbaya)
Ukubwa na aina ya memori
Google Pixel 8a inatumia memori aina za UFS 3.1
Kasi ya kusafirisha data huwa ni kubwa kwenye muundo huu wa memori
Kuna matoleo mawili tu ya hii simu upande wa memori
Ambapo kuna ya GB 128 au ya GB 256 na ram za ukubwa wa GB 8
Hiko kiasi kinatosheleza kuhifadhi mafaili mengi
Haina sehemu ya kuweka memori kadi ya ziada
Uimara wa bodi ya Google Pixel 8a
Simu ya Google Pixel 8a ina viwango vya IP67
IP67 inamaanisha simu haipitishi maji kama ikizama kwenye kina kinachofika mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Yaani kama ukiizamisha simu kwenye diaba simu inaweza kuzuia maji kwa muda huo
Uimara wa skrini protekta inayokuja nayo upo sana kwenye kuzuia mikwaruzo
Kutokana na kutumia kioo cha gorilla glass 3, hivi huwa ni imara kuzuia mikwaruzo
Kwa hiyo ni muhimu pia kununua skrini protekta kuzuia kupasuka
Ubora wa kamera
Google Pixel 8a inakuja na kamera mbili tu ambapo moja wapo ni ya ultrawide
Kamera kubwa ina megapixel 64 na ulengaji wa kiotomatiki wa dual pixel
Kamera yake inatoa picha zenye usahihi wa rangi kwa kiasi kikubwa
Ina kiwango kizuri cha utofautishaji rangi yaani kama kuna sehemu ina kivuli basi kivuli hakiathiriwi na mwangaza mkubwa kwenye mwanga mwingi
Hakuna kiwango chengachenga(noises) kinachoonekana kwa picha zilizopigwa nyakati za mchana
Kwa picha zilizopigwa kwenye mwanga hafifu bado vitu vinaonekana kwa ustadi
Kwenye mwanga mdogo sana vitu havionekani
Kamera zake zinarekodi pia video za 4K kwa kasi ya 60fps
Ubora wa Software
Google ndio watengenezaji wa mfumo endeshi wa Android
Hivyo simu inatumia mfumo wa Android 14, kama kuna toleo jipya simu itapokea
Katika android hii kuna maingizo ya matumizi ya AI kwa kiasi kikubwa
Kwa mfano, app ya kamera inakupa uwezo wa kuondoa kitu ambacho hutaki kitokee
Na hata ukiondoa ubora wa picha unabaki kama ulivyo
Washindani wa google pixel 8a
Kuna washindani wengi kwenye hiki kipengele
Ila kwa mwaka huu washindani wakubwa kuna Tecno Camon 30 premier, Samsung Galaxy S4 na hata iPhone 15 bila kusahau Oppo Reno12 Pro
Hizi zina sifa zinazofanana nyingi ila kuna eneo moja pixel inaachwa nyuma pakubwa
Eneo hilo ni upande wa utendaji wa processor
Tensor G3 hazifanyi vizuri ukilinganisha na ubora wa chip za samsung na apple ama mediatek za toleo la juu
Kwa mtu anayetaka simu iliyokamilika kwenye idara zote anaweza akawashawishika kuchukua toleo lingine mbali na google
Ila google ina nguvu katika upande wa kamera
Neno la mwisho
Kiujumla bei ya Google pixel 8a inaendana na vitu inavyoambatana navyo
Ukiwa nayo utafurahi ubora wa picha unaozarishwa na kamera
Utashuhudia mambo mbalimbali ya artificial intelligence yaani kwa kiswahili inaitwa akili mnemba
Pamoja na yote wapo washindani wanaotoa vitu kama hivyo
Wazo moja kuhusu “Bei ya Google Pixel 8a na Sifa zake Muhimu”
Nawakubali