Simu ya apple iphone se(2022) ni simu ndogo yenye kamera moja upande wa nyuma.
Simu mpya ya Apple iPhone SE ni iPhone ya bei nafuu japo bei itakushangaza
Kwa sababu ukilinganisha na simu zingine, iPhone se bado ni simu ya gharama
Simu ina sifa nyingi za iPhone 13
Japokuwa SE imepunguza ubora wa kioo.
Sifa za simu ya Apple iPhone SE(2022)
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Retina IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 64GB,128GB,256GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-4.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 995,280/= |
Upi ubora wa simu mpya ya iPhone SE(2022)?
Simu iPhone SE inatumia processor bora ya simu duniani kwa sasa.
Uimara wa processor unachangia bei yake kuwa juu
Simu hii inatumia memori zenye kasi zaidi kuliko memori za simu ya android
Network ya 5g inakubali spidi ya kasi sana.
Na mtandao wake wa 4g unakubali karibu bands zote duniani.
Hivyo simu inaweza tumika popote
iPhone SE inaweza kutumia mtandao bila laini ya simu.
Huduma hii hupatikana endapo kampuni ya simu ina huduma ya eSim
Network
Simu mpya ya iPhone SE(2022) inaweza kutumia 4G au 5G kuperuzi mtandao.
Jambo la kustahabisha,
5G yake inakubali masafa marefu yenye kasi zaidi.
Ukiona bands za simu zimeandikwa A2783, A2784, A2785 na A2782
Basi hiyo simu inadownload file kwa spidi kubwa zaidi ya 5g
Na upande wa network ya 4G inakubali mitandao yote ya hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha iPhone SE(2022)
iPhone SE imetengenezwa kwa kioo cha IPS LCD.
Apple wanakiita Retina IPS LCD
Sifahamu utofauti wa ips ya apple na za simu zingine.
Ila IPS LCD havitoi rangi iliyokolea ukilanganisha na vioo vya Amoled au OLED
Resolution ya SE(2022) ina ubora wa kati
Kutokana na kuwa na ukubwa wa 750 x 1334 pixels
Moja ya kitu kinachokosekana kwenye hii simu ni HDR10
HDR10 hurekebisha muonekano wa rangi wa display na kufanya vitu vionekane kiuhalisia.
Nguvu ya processor Apple A15 Bionic
Mpaka kufikia sasa hakuna chip yoyote ya simu inayofikia Apple A15 Bionic.
Apple A15 Bionic inaizidi kwa kiasi kidogo processor mpya ya Snapdragon 8 gen 1
Matoleo mapya ya simu za samsung s-series zinatumia Snapdragon 8 gen 1
Kiujumla apple a15 bionic ina core sita
Core sita zimegawanyika mara mbili.
Zipo core kubwa na ndogo.
Uwezo wa core kubwa
Core zenye nguvu zipo mbili.
Hizi hufahamika kama Avalanche
Kila core kubwa ina spidi inayofikia 3.223GHz
Ongezeko la spidi limekuza utendaji kwa karibu 8% ukilinganisha Apple 14 ya iPhone 12.
Geekbench inaipla A15 Bionic alama 1739
Wakati Antutu ni 804813
Processor nyingi zilizowahi kufafanuliwa hapa hazifikii alama 800
Chipset mpya ya apple ina utumiaji mzuri wa umeme
Hii inamaanisha ukiwa unacheza gemu kwa masaa mengi mfululizo simu itachelewa kuisha chaji
Uwezo wa core ndogo
Kuna core sita zenye nguvu ndgo.
Hizi ni aina ya processor mahsusi kwa matumizi madogo ya umeme
Kazi ndogo ndogo zinafanyika ndani ya simu hutumia core ndogo
Kila core ina spidi inayofikia 2.0GHz
Na hizi core kwenye iPhone huitwa Blizzard
Uwezo wa betri na chaji
Simu ya iPhone SE 2022 ina betri yenye ujazo mdogo.
Betri yake ni aina ya Li-Ion yenye ukubwa wa 2018mAh
Ukubwa huo wa betri unaweza kujazwa kwa 50% na chaji ya wati 20
Ila hii ni simu inayokaa na chaji muda mfupi
Ukubwa na aina ya memori
Simu nyingi za iPhone huja na memori aina ya NVMe.
NVMe ina spidi ya kasi sana linapokuja swala la kusoma na kuandika faili.
Hivyo data husafirishwa kwa kasi.
Spidi yake kwa maana ya bandwidth inafika 42.7 Gbit/s
Ram za SE 2022 zina ukubwa wa 4GB pekee
Na kuna aina tatu za hii simu upande wa memori 64GB, 128GB na 256GB
Uimara wa bodi ya iPhone SE(2022)
Hii ni simu fupi ya iphone yenye urefu wa inchi 5.4
Urefu unaojaa kwenye mkono
Simu ni ngumu, na maji hayawezi penya kirahisi ikidumbukia kwenye kina cha mita moja
Kwa sababu simu ina viwango vya IP67
Upande wa nyuma na mbele unalindwa kwa vioo
Haijaainishwa aina ya vioo.
Frame za apple iphone se ni za aluminium
Kiujumla bodi ya simu ni imara kwa kiasi chake.
Ubora wa kamera
Kamera ya iPhone se 2022 ipo moja kila upande(mbele na nyuma)
Kamera zinatumia teknolojia ya ulengaji wa moja kwa moja aina ya PDAF.
PDAF si nzuri sana kama dual pixel pdaf ila bado ni teknolojia inayotoa picha nzuri
Video itatokea vizuri tu pale unaporekodi video wakati ukiwa unatembea.
Kwa sababu kamera ina OIS
Ubora wa video
Simu inarekodi aina mbili za video
iPhone se inaweza kurekodi video za 4k na full hd
Uzuri wa kamera hii ni kurekodi video kwa spidi kubwa inayofikia 240fps
Nini maana ya 4k?
4K ni aina ya video ambazo zina pixels 3840(4000) kutoka kushoto kwenda kulia na pixel 2160 kutoka juu kwenda chini.
Pixel ni vinukta vidogo sana ambavyo huwa na mchanganyiko wa rangi tatu
Rangi hizo ni nyekundu, blue na kijani.
Hivyo vinukta(pixel) ndivyo vinavyounda picha unazoziaona kwenye simu, tv nk
Pixels zinapokuwa nyingi zinaunda picha nzuri zaidi.
Ubora wa Software
iPhone SE 2022 inatumia mfumo endeshi wa iOS 15.4
Kwenye iOS 15.4 kuna emoji mpya 38
Mfumo una face id inayotambua sura hata ukieka barakoa
Baadhi ya simu za android zina face lock yenye ufanisi mdogo
Simu kama redmi note 10 haiwezi kuitambua sura kama mwanga ni mdogo
Zitazame emoji zote za iOS 15.4 : emoji za apple
Bei ya iPhone SE(2022) Tanzania
Bei ya iphone se 2022 inaweza kuzidi 996,000/= kwa Tanzania.
Maduka mengi ya Tanzania wanauza iPhone mpya kwa bei ya juu kidogo
Bei ya hii simu inanunua simu kali ya android kuliko hii
Kuna simu za oppo, samsung, realme, oneplus zenye “premium feature” za kutosha
Yapi Madhaifu ya iPhone SE(2022)
iPhone SE 2022 haijatumia kioo bora cha Super Retina OLED
Simu haina kamera ya telephoto, ultrawide, macro
Apple hawajaweka autofocus ya dual pixel pdaf
Hii simu ni fupi sana kwa watu wengine haiwapi burudani
Simu ina betri ndogo inayokaa na chaji masaa machache
Inaweza ikakulazimu kununua power bank
Simu inakosa sehemu ya kuweka memori card
Neno la Mwisho
Apple ni brand ya simu yenye wapenzi wengi.
Kwa wapenzi wa apple wenye bajeti ndogo simu mpya ya iPhone SE itakupa vitu vingi vinavyopatikana kwenye iPhone zingine.
Lakini kwa wale ambao hawajali kuhusu brandi wanaweza wakaangalia machaguo mengine ya iPhone za zamani au simu mpya za android.