Ukitaka kununua simu kitu kimojawapo utakachoambiwa ni ukubwa wa RAM
Utasikia ukubwa wake ni GB 128 na RAM GB 8.
Kwa asiyefahamu anaweza kujiuliza RAM ni nini na ina msaada gani kwenye simu.
Haya ndio majibu
RAM ni memori ya kuhifadhi data
Kwenye simu na kompyuta kuna memori za aina mbili
Kuna memori inayofadhi data(mafaili) kwa muda na hata milele kama hujafuta
Na kuna memori inayohifadhi data kwa muda mfupi na baadae kupotea
Memori inayohifadhi data kwa muda mchache inaitwa RAM.
Kwa nini RAM inahitajika
Memori ya RAM ina kasi kubwa ya kusafirisha data
Na ndiyo memori inayowasiliana na prosesa ya simu au kompyuta.
Iko hivi ….
Ukifungua faili au app yoyote data zinatoka kwenye memori kubwa kwenda kwenye RAM
Mchakato wa kila kazi kwenye simu ama kompyuta unafanywa na prosesa(cpu)
Mawasiliano yanatakiwa yafantike kwa haraka sana.
Kasi ambayo memori kuu haiwezi hivyo RAM ndio yenye hiyo spidi
Ukimaliza matumizi ya app ama faili na ukafunga hiyo basi data zote zinajifuta kwenye memori ya RAM mpaka pale utakapokuja kuitumia app au faili tena
RAM kubwa huipa simu uwezo wa kufungua app ama mafaili mengi kwa wakati mmoja bila kukwama kwama
Kwa sasa kwenye unashauliwa kuwa na RAM angalau ya GB 8
Kirefu cha neno RAM
Neno la RAM ni kifupi cha neno Random Access Memory
Kwa maana ni memori inayohifadhi na kuisaidia mafaili ya data mbalimbali kutumika wakati ikihitajika
Ukimaliza kutumia basi mafaili yanajifuta kwenye memori ya RAM
RAm za kwenye simu zinatumia aina ya RAM ziitwazo LPDDR4X
LPDDR4X zimeundwa kutumia umeme kidogo kupunguza kuisha kwa chaji ya betri
Tofauti na Laptop nyingi ambazo huwa zinatumia mifumo ya DDR4
DDR4 zimeundwa kufanya kazi kubwa hivyo matuzi ya umeme yapo juu kidogo
RAM ndogo ni tatizo
Kama simu yako imekuwa nzito moja ya sababu ni RAM ndogo
Na RAM ndogo huwa na GB ndogo yaani GB 4 kwenda chini
Kikawaida mfumo endeshi wa simu kama Android unachukua zaidi ya GB 2
Kwa hiyo unakuta RAM iliyobaki kwako kutumia unakuta ni ndogo
Ukiwasha intaneti kuna app zinajifungua bila wewe mfano notifications kuwa nyingi
Hizi pia zinakula RAM
Sasa kutumia app unayoitaka inakuta RAM imebakisha sehemu ndogo.
Inabidi app isubirie nafasi ipatikane ili data zake ziingie kwenye RAM na ziende kwenye prosesa kuchakatwa
Na hiko kitendo cha kusubiria kama foleni inafanya simu kuwa nzito
Neno la mwisho
RAM ni memori inayotumika kipindi umefungua app na ukiifunga app data hupotea
Ni memori inayowasiliana moja kwa moja na ubongo wa simu yaani prosesa
Ukiwa na RAM kubwa simu hufanya kazi kwa ufanisi zaidi