Infinix Note 60 Pro ni bonge la simu inayozitoa “knock out” simu shindani nyingi
Ukilinganisha na matoleo ya infinix yaliyopita, Infinix Note 60 Pro imeboreshwa pakubwa sana
Ni simu ya daraja la kati inayolenga utendaji mkubwa kwa kadri inavyowezekana
Utaona hili kwa kutazama sifa zake zote
Ila kwanza ijue bei ya Infinix Note 60 Pro kwa hapa Tanzania
Bei ya Infinix Note 60 Pro ya GB 256
Infinix Note 60 Pro yenye GB 256 na RAM ya GB 12 inauzwa milioni moja na laki mbili (1,200,000)
Inatumia mfumo wa memori wenye kasi aina ya UFS
Pia kuna toleo la infinix la GB 128 na bei yako ipo chini kidogo
Mgawanyo wa RAM umegawanyika, zipo za GB 12 na GB 8
Mpangilio unatoa picha juu ya utendaji wa simu kiujumla
Sifa za Infinix Note 60 Pro
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g,5g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:144Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 128GB, 256GB na RAM 12GB, 8GB |
| Kamera | Kamera mbili
|
| Muundo | Urefu-6.78inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 1,200,000/= |
Uwezo wa network
Infinix Note 60 Pro inasapoti mtandao hadi wa 5G
Pia inasapoti laini za eSIM
Simu matoleo yaliyopita hayakuwa na uwezo wa eSIM
Hili ni eneo mojawapo lililoboreshwa
Ila yenyewe inasapoti mpaka laini mbili za eSIM
Ubora wa kioo
Inatumia kioo cha Amoled kama ilivyo kwa matoleo ya nyuma
Na refresh rate ya 144Hz hivyo kina mwitikio mkubwa unapo-scroll
Kioo ni angavu na unaweza kuona vitu kwa uzuri ukiwa kwenye mazingira yenye jua kali
Maana uangavu wake unafika nits 1600
Nguvu ya utendaji
Hii simu ina nguvu ya kufanya vitu vingi kwa ufanisi
Hii inatokana na kutumia prosesa aina ya Snapdragon 7s Gen 4
Ni kitu kipya, mara nyingi infinix hutumia chip kutoka kampuni ya Snapdragon
Kama wewe unapenda kucheza gemu sana basi hata gemu za kompyuta zinacheza bila shida kutumia emulator
Ukilinganisha utendaji wa Infinix Note 50 Pro, utofauti ni mkubwa sana kwa karibu 60%
Kwa kifupi Infinix Note 60 Pro inashindana na simu kama Redmi Note 15 Pro Plus au Tecno Camon 50 Ultra
Uimara wa bodi
Kioo cha hii simu kinalindwa na kioo cha Gorilla Glass 7i
Ni kioo kigumu kupasuka simu ikianguka kwenye kimo cha mita
Pia inaweza kuzuia maji ya kiwango cha kutiririka
Kama simu ikizama ndani ya maji muda inaweza haribika
Hapa hawajafanya mabadiliko makubwa ukilinganisha na simu ya Tecno Camon 50
Hata hivyo bado uwezi ilinganisha hii simu na simu za bei rahisi ikiwemo camon 50
Ubora wa kamera
Infinix Note 60 Pro ina kamera mbili tu
Na kamera kubwa ina megapixel 50
Kuhusu ubora wa picha ni mzuri
Ila kuna mazingira yanaathiri ubora wa picha hasa mwingi ukiwa mkubwa
Lakini kwa mtumiaji wa kawaida anaweza asione tofauti sana ya kamera
Hii simu inarekodi pia video za 4K ambazo huwa na mng’ao mkubwa
Uwezo wa betri na chaji
Infinix Note 60 Pro inakuja na betri kubwa yenye 6500mAh
Ukubwa huu unaifanya simu kufikia masaa 15 ukiwa kwenye intaneti muda wote
Japo sina data za uhakika kwenye ukaaji wa chaji lakini kiuzoefu simu inaweza fika huko
Inakuja na chaji ya umeme wa wati 90
Hii inajaza betri kwa kasi kubwa na ndani ya muda mfupi
Kimakadirio ndani ya dakika 40 simu inajaa
Ubora wa software
Infinix Note 60 Pro inapewa nguvu na mfumo wa XOS 16 ukiwa ndani ya Android 16
Android 16 ina muonekano mzuri wa icon
Na pia XOS 16 inasapoti uwezo wa kutumia app zaidi ya moja kwa wakati mmoja
Yaani skrini inajigawa pande mbili juu na chini
Kila upande unaonyesha app labda juu whatsapp na chini ni TikTok
Pia mifumo mbalimbali ya AI inapatikana kwenye hii simu
Simu itapokea matoleo mapya ya Android kwa miaka 3, yaani itapata hadi android 19
Simu Mbadala
Kuna simu nyingi sokoni zenye ubora sawa ama zaidi ya hii
Bei ya hii infinix inaendana na simu ya Samsung Galaxy A57
Samsung Galaxy A57 ina vitu vya ziada ambavyo havipo kwenye hii infinix
Mfano ni uwepo wa hdr10+ na ip68, na kamera aina ya macro japo si ya muhimu sana
Simu zingine ni Redmi Note 15 Pro+ na Tecno Camon 50 Ultra
Neno la mwisho
Kama simu yako ya sasa ni Infinix Note 50 Pro basi una sababu nyingi za kuibadilisha
Maboresho yaliyoletwa na Infinix Note 60 Pro yana tofauti kubwa sana
Japo bei yake inaingia katika kundi lenye simu nyingi kali pia