Kwa mwaka 2024, kampuni ya HMD Global inayotengeneza simu za Nokia hawajatoa toleo jipya mpaka sasa machi 2024
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema HMD inatarajia kutoa matoleo 17 mwaka 2024
Tusubiri tuone, hata hivyo hapa kuna baadhi ya simu mpya za nokia zilizotoka mwaka 2023
Pamoja na kutoka 2023 bado ni simu mpya kwani hakuna toleo jipya kwa sasa la mwaka huu
Nokia C210
Bei ya Nokia C210: 260,000/= ,Ukubwa wa Memori: 32GB, RAM: 3GB
Simu ya Nokia C210 ni toleo la hivi karibuni kabisa la Nokia lilitoka mwezi agosti 2023
Ni simu ya daraja la chini na utendaji wake sio mkubwa
Inatumia chip yenye nguvu ndogo ya Snapdragon 662
Nokia C210 kioo chake ni cha IPS LCD chenye resolution 720p ambayo ni viwango vya kawaida sana kwa nyakati za sasa
Hii simu inamfaa kwa mtumiaji mwenye matumizi madogo ya simu
Nokia G310
Bei ya Nokia G310: 490,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Nokia G310 ni nokia ya 5G na yenyewe iliingia sokoni mnamo mwezi wa nane ya mwaka 2023
Kioo chake kina resolution ndogo
Utendaji wake unachagizwa na chip ya Snapdragon 480+ 5G
Hii ni chip ya daraja la chini yenye mtandao wa 5G
Ina kamera tatu ambapo kamera kubwa ina megapixel 50 bila kuwa na ulengaji wa PDAF
Nokia 150 (2023)
Bei ya Nokia 150: 120,000/= ,Ukubwa wa Memori: 4MB, RAM:
Simu ya Nokia 150 (2023) ni simu ya batani ambayo imetoka 2023
Betri yake ni ndogo ukizingatia simu za batani huwa hazitumii moto mwingi
Hata memori yake ni ndogo kwani ina MB 4
Kwa maana hiyo mnunuaji wa hii simu hana budi kununua memori kadi ya ziada
Kwa wapenzi wa simu za batani basi hili ni chaguo zuri
Nokia G42
Bei ya Nokia G42: 430,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu nyingine ya daraja lachini yenye 5G ambayo ilitoka mwezi juni 2023
Utendaji wake sio mkubwa kutokana na kutumia chip ya Snapdragon 480+ 5G
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake ina kasi ya kupeleka umeme wa 20W
Hivyo kwa kiasi fulani betri haitochukua muda mrefu kujaa
Kamera zake zina lenzi za wide, ultrawide na macro na kamera kubwa ina megapixel 50
Nokia C300
Bei ya Nokia C300: 350,000/= ,Ukubwa wa Memori: 32GB, RAM: 3GB
Betri ya Nokia C300 ukubwa wake ni mAh 4000
Na chaji yake inapeleka umeme wa wati 10
Pamoja na udogo wa betri simu inaweza kuchukua masaa mengi kujaza betri
Kamera zake zipo tatu na kamera kubwa ina megapixel 13
Kiujumla mfumo wake wa kamera sio wa kutoa picha nzuri ukifananisha na simu za samsung s-series
Nokia C110
Bei ya Nokia C110: 280,000/= ,Ukubwa wa Memori: 32GB, RAM: 3GB
Simu ya Nokia C110 ni nokia ya daraja la chini yenye utendaji mdogo kati ya nokia nyingi zilizoorodheshwa
Kitu kinachofanya kuwa na utendaji wa chini ni kuwa na processor ambayo ina nguvu ndogo
Nokia C110 inatumia processor ya Mediatek Helio P22
Hii simu inalenga watumiaji ambao wana matumizi ya kawaida ya simu na wale ambao hawana bajeti ya kumiliki simu janja zenye bei kubwa
Lakini ndio hivyo simu za bei nafuu huwa zina changamoto ya utendaji nmdogo
Nokia XR21
Bei ya Nokia XR21: 1,700,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Kati ya simu nyingi za nokia zilizopo kwenye orodha Nokia XR21 ina ubora unaoendana na viwango vya simu nyingi za sasa
Ila bei yake ni kubwa kwa sababu inaendana na simu zenye ubora mkubwa kuliko hii nokia
Unaweza kuziona hizi simu hapa: Simu mpya matoleo ya 2024
Nokia XR21 inatumia processor ya Snapdragon 695 5G na utendaji wake ni wa wastani
Ina kamera mbili za wide na ultrawide huku kamera yenye ulengaji wa PDAF ina megapixel 64
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 33, hivyo betri haichukui muda mrefu kujaa
Nokia C12 Pro
Bei ya Nokia C12 Pro: 240,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 2GB
Simu nyingine ya daraja la chini ya nokia ambayo inawafaa wenye matumizi ya kawaida
Inatumia chip iliyotengenezwa na kampuni ya china ya Unisoc SC9863A1
Unisoc SC9863A1 utendaji wake sio mkubwa hivyo usitarajie ubora mkubwa kutoka kwa Nokia C12 Pro
Kioo chake ni cha aina IPS LCD chenye resolution ndogo ya HD
Kamera yake moja ubora wake sio mzuri
Hii simu ina kamera moja tu upande wa nyuma
Nokia C32
Bei ya Nokia C32: 780,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 4GB
Simu ya Nokia C32 ina ufanano wa kiwango kikubwa na Nokia C12 Pro
Tofauti kubwa inapatikana upande wa kamera
Nokia C32 ina kamera nzuri kidogo na ina ukubwa wa megapixel 50
Betri yake ukubwa ni 5000mAh ila chaji yake haina kasi kubwa
Chaji inapeleka umeme wa wati 10 tu
Nokia C22
Bei ya Nokia C22: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Nokia C22 pia ni moja ya nokia ya bei nafuu ambayo na yenyewe utendaji sio mkubwa kivile
Kwani processor inayotumia haina nguvu kutokana na kuwa na core ndogo kwenye kila sehemu
Ni simu inayomfaa mtumiaji mwenye matumzi ya wastani
Ila kama unapenda kamera nzuri Nokia C22 sio chaguo zuri
Kwani ina kamera mbili na moja ukubwa wake ni 13MP
Kioo chake kina resoltuion ya 720 x 1600 pixels ambayo sio kubwa kwa viwango vya sasa
Maoni 2 kuhusu “Simu mpya za Nokia zilizotoka 2023-2024 na bei zake”
Nahitaji kuanza biashara ya kuuza simu,niwe na mtaji kiasi Gani kama kuanzia KULINGANA na new current model za simu za batani au kiswaswadu ,,msaada tafadhari .
Me naitaji simu ya mkopo