Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka sasa 2024 tayari kampuni ya OPPO toka china wametoa simu zaidi ya 15 za madaraja mbalimbali
Hapa utakutana na orodha ya simu mpya za oppo na bei zake kwa mwaka 2024
Hii orodha inahusisha OPPO za bei rahisi na Oppo za bei kubwa
Kwa maana kuna oppo za madaraja ya chini na za madaraja ya juu kabisa
Kwa maana hiyo utafanya uchaguzi kulingana na bajeti yako pamoja na vigezo unavyopendelea simu kuwa navyo
1. OPPO Reno11 F
Bei ya OPPO Reno11F: 870,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Simu ya OPPO Reno11 iilianza kupatikana sokoni mnamo february 8
Ni OPPO ya kamera tatu na inayotumia kioo cha AMOLED chenye kuonyesha rangi zaidi ya bilioni
Hii oppo ni ya daraja la kati japo nkiharaka bei yake
Utendaji wake una nguvu kwa sababu chip yake imeundwa kwa muundo wa Cortex A78 kwenye core zenye nguvu
Inatumia processor ya mediatek Dimnensity 7050
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 67 hivyo hujaa ndani ya muda mfupi
2. OPPO Pad Neo
Bei ya OPPO Pad Neo: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Oppo Pad Neo ni kishikwambi(tablet) chenye ukubwa wa inchi 11.4
Ukubwa wake unavizidi vishikwambi vya walimu
Kioo cha Oppo pad neo kina resolution kubwa inayofanya vitu kuonekana vizuri
Betri yake ina ujazo wa kukaa na chaji masaa mengi kwani ukubwa wake ni 8000mAh
Kamera yake sio nzuri ila chaji yake inachaji simu kwa haraka kutokana na kupeleka umeme wa wati 33
3. OPPO Reno 11 Pro
Bei ya OPPO Reno11F: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Moja ya kitu cha kuvutia kwenye OPPO Reno 11 Pro ni kio chake kuwa na HDR10+
Hii inafanya kioo kuwa na utajiri wa rangi unafanya vitu kuonekana kwa uzuri
Kamera zake tatu na zote ni nzuri zenye uwezo wa kurekodi video za 4K
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 80, hii inaweza kuijaza betri yake ndani ya dakika 45 kwa 100% kutoka zero
Ila betri yake sio kubwa kama zilivyo simu nyingi za siku hizi kwani ukubwa wake ni 4600mAh
Nguvu ya utendaji ni ya kuridhisha kwani inatumia chip ya Mediatek Dimensity 8200
4. OPPO Reno 11
Bei ya OPPO Reno11: 1,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Kisifa ni ngumu kuitofautisha OPPO Reno11 na OPPO Reno11F
Zote zinatumia processor ya aina moja ambayo ni Mediatek Dimensity 7050
Hivyo hakuna utofauti katika utendaji
Kiuhalisia ukiiona Reno11F ni kama umeiona Reno 11
Inawezekana ikawa ni simu moja yanayotofautiana bei kutokana na soko lengwa
5. OPPO Find X7 Ultra
Bei ya OPPO Find X7 Ultra: 2,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Oppo Find X7 Ultra ni simu kali kabisa ya OPPO ambayo ipo kwenye kundi la daraja la juu
Simu inatumia chip yenye nguvu kubwa na iliyotumika kwenye simu nyingi za madaraja ya juu
Chip hiyo ni Snapdragon 8 Gen 3 ambayo hata Samsung Galaxy S24 Ultra wameitumia kwa samsung za Marekani
Hii simu inakupa na mfumo wa chaji unaosapoti umeme wa kasi ya wati 100, hii inajaza simu kwa wastani wa dakika 30
Ni simu yenye kamera nne na zote zinapiga picha vizuri kwa nyakati zote(mchana na kwenye mwanga mdogo)
Hii ni oppo yenye waterproof
6. OPPO Find X7
Bei ya OPPO Find X7: 2,400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Oppo Find X7 zinafanana na mkubwa kitu kinachotofautiana na aina za processor
Oppo Find X7 inatumia processor ya Dimesnity 9300
Hata Chip ya mediatek dimensity 9300 na Snapdragon 8 gen hazina tofauti kihivyo kiutendaji
Na kwa mtumiaji yeyote anaweza asione tofauti
Sifa zingine zote kuanzia betri, kioo na chaji zipo sawa na Find X7 Ultra
7. OPPO A59
Bei ya OPPO A59: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Oppo A59 ni simu ya daraja la kati ambayo haina vitu vingi vizuri kama simu zilizotangulia
Hii simu iliingia sokoni mnamo mwezi desemba mwaka 2023
Kwa mpenzi wa oppo za bei nafuu huu ndio mbadala
Kikubwa ambacho ni kizuri ni chaji ya wati 33 na uwepo wa kioo chenye refresh rate
Ni simu nzuri kama hujari sana ubora wa kamera
Utendaji wake ni wa wastani kwani chip yake ni Dimensity 6020 ambayo haina nguvu kama dimensity 9300
8. OPPO Pad Air2
Bei ya OPPO Pad Air2: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Hii ni tablet(kishkwambi) chenye ukubwa wa inchi 11.4
Haina sehemu ya kuweka laini ya simu hivyo ukitaka kuunga intaneti itakulazimu kuunga wifi
Kwa maana sio kishikwambi kwa ajili ya kupiga simu
Utendaji wake sio mkubwa ni wa wastani na inatumia processor ya Mediatek helio G99 kufanya kazi zake
Betri yake na yenyewe ni kubwa ina mAh 8000 inayoifanya simu kukaa na chaji masaa mengi
9. OPPO A2
Bei ya OPPO A2: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Simu ya OPPO A2 ni simu nyingine iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2023
Hii simu ina kamera mbili, ila moja tu ndio inatoa picha nzuri
Inatumia processor yenye nguvu ya wastani hivyo utendaji wake sio mkubwa
Chaji yake inasapoti umeme wa wati 33 kama ilivyo kwa OPPO nyingi za siku hizi
Ukubwa wa betri ni 5000mAh
10. OPPO A79
Bei ya OPPO A79: 550,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Oppo A79 na yenyewe iliingia sokoni mwishoni mwa mwaka 2023
Ni simu ya daraja la kati inayospaoti mtandao wa 5G
Inatumia chip ya Dimensity 6020 katika kufanya kazi zake
Pia chaji yake inapeleka umeme wa wati 33 unaoweza kujaza simu kwa asilimia mia moja kwa DAKAIKA 80
Ubora wa kamera yake ni wa kuridhisha pia
11. OPPO Find N3
Bei ya OPPO Find N3: 5,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM: 12GB
Kwa kuangalia bei ya simu tayari unapata picha ubora wake ukoje
Hii ni simu ya kukunja na kukunjua na kioo chake cha LTPO Amoled
Kamera zake zote ni nzuri katika upigaji wa picha
Betri yake ina ukubwa wa wasatani wa 4800
Chaji ina kasi yakujaza simu kwa muda mfupi kutokana na kupeleka umeme wa wati 67
Inahitaji uwe na bajeti nzuri kununua simu ya milioni tano
12. OPPO A2X
Bei ya OPPO A2X: 400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Oppo A2X ndio oppo ya bei nafuu na ndogo kwenye orodha iliyopo
Inatumia chip ya dimensity 6020 kama ilivyo kwa matoleo mengine ya adaraja ya kati ya oppo kwa mwaka 2023 na mwaka 2024
Kwa bahati mbaya kamera yake sio ya kuvutia sana kama ilivyo oppo zingine za hapa tofauti na vishikwambi
Pia chaji inapeleka umeme kidogo ukilinganisha na oppo zote zilizopo kwenye orodha
Ni simu inamfaa mtu asiehitaji mambo mengi sana
Kumbuka: bei za simu zinabadilika kutokana na mambo mbalimbali, si lazima bei unayoiona hapa ikawa kama ilivyo kwa nyakati zote
Maoni 12 kuhusu “Simu mpya 12 nzuri za Oppo na bei zake 2024”
Je kuna oppo ya 300000
Zipo
Mikoani simu azipo na zinahitajika sana
Tufikishiwe huduma mikoani
Jee OPPO Reno 12 pro shilings ngapi
Oppo reno 12 5g ni shilingi milioni 1.5 ya GB 256
Je Kuna oppo ya laki tatu
Yap
Nahitaji hio ya 2.5 Niko mbea ntaipataje?
Natumia OPPo A12 GB32 ram3 mpya ina bei Gan maana hii nilipandia juu juu
hii kwa sasa sifahamu bei yake
Nahitaji kuunda account kwenye OPPO