Apple iPhone 15 Pro Max ni toleo jipya la iphone kwa mwaka 2023
Ni simu ya kwanza kutoka Apple kutumia chaji aina ya USB Type C ambazo hutumika na simu za android kwa muda mrefu
Hii inamaanisha apple wamekubali kufuata matakwa ya EU
Utendaji wake ni mkubwa kutokana na kutumia processor mpya
Japo kumeibuka na changamoto ya simu hizi kupata moto mwingi kitu kilichowalazimisha apple kutoa maboresho ya mfumo wa iOS
Kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye maeneo mengi, bei ya Apple iPhone 15 Pro Max ni zaidi ya milioni mbili na nusu kwa hapa Tanzania
Bei ya iPhone 15 Pro Max ya GB 256
Bei ya iPhone 15 Pro Max yenye ukubwa wa gb 256 inafika shilingi milioni nne na laki sita (4,600,000) kwa hapa Tanzania
Kwa bei halisi ya Marekani na maeneo mengine duniani simu inauzwa kwa kima cha milioni tatu na laki nne
Kuna utofauti mkubwa wa bei kwa hapa nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kodi na gharama za usafirishaji
Kwa mtu anayejua namna ya kuagiza vitu mtandaoni hasa kupitia Amazon anaweza nunua huko kwa kima cha chini
Ila kwa hapa Tanzania bei lazima iwe kubwa
Isikushangaze sana kuona iPhone kuwa na bei isiyoendana na vipato vya watanzania wengi
Hizi ni simu zinazotengenezwa kwa kuwalenga watu wenye vipato vikubwa na pia sifa zake ni kubwa sana.
Sifa za Apple iPhone 15 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,512GB,1TB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 4,600,00/= |
Upi ubora wa iPhone 15 Pro Max
Simu ina kioo kionyeshacho picha kwa mwangaza mzuri na uangavu wa kuonyesha vitu kwa ustadi
Processor yake ina uwezo wa mkubwa hivyo inaifanya simu kuwa na utendaji wenye nguvu kwenye mambo mengi
Ni simu ya 5G na pia ina eSIM ambayo zimeanza kutumika na mitandao mbalimbali hapa nchini
Betri yake inakaa na moto muda mrefu kiasi cha kwamba hutohitaji kuichaji simu kila wakati
Inasapoti chaji yenye kupeleka umeme mwingi na hivyo kujaza betri kwa haraka
Ubora wa kamera ni wa kiwango kikubwa na ni moja ya simu zenye kamera nzuri kwa mwaka 2023
Uwezo wa network
iPhone 15 Pro Max ni simu yenye uwezo wa kusapoti mtandao wa 5G wa aina zote
Kumbuka kuna aina tatu za 5G zinazoweza kutumia miundombinu ya aina mbili
iPhone 15 Pro Max inasapoti mpaka 5G ya SA ambayo huwa ina kasi kubwa sana
Kwa hapa Tanzania mitandao yenye 5G inasapoti masafa ya kati
Hata hivyo network bado inaoatikana maeneo machache ya Dar Es Salaam, kwa maana haijasambaa nchi nzima
Ukitazama hii video hapa chini utaona kasi yake ya intaneti inatembea mpaka 4Gbps
Kwa mfano ukiwa unataka kupakua faili lenye ukubwa wa 1000MB, simu inachukua sekunde mbili tu kudownload kikamilifu
Yaani kwa mfano umekutana na movie ya kikorea(sizoni) yenye ukubwa wa GB 7, basi series nzima utaipata ndani ya sekunde 14
Wakati huo ukilipia 5g ya Vodacom yenye kasi 30Mbps itakuchukua zaidi ya dakika 30 kuipata sizoni
Hii ni 5G aina ya mmWave kwa hapa nchini huwezi kuipata kasi ya kiwango hiki hata ukiwa na hii simu
Ubora wa kioo cha iPhone 15 Pro Max
Kimuonekano wa vitu kioo cha iPhone 15 Pro Max kinaonyesha vitu kwa uangavu mkubwa
Rangi zake za kioo zina kina kikubwa, hivyo vitu vingi vinaonekana kwa rangi zake halisi kwa kiasi kikubwa
Sababu kubwa ni kioo cha hii simu ni aina ya LTPO OLED apple wanakiita LTPO Super Retina XDR OLED
Ustadi wa rangi unachagizwa na uwepo wa teknolojia za HDR10 na Dolby Vision
HDR10 na Dolby Vision zinasaidia kuongeza kina cha rangi ya kioo hivyo kioo kinakuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Kioo cha iPhone 15 Pro Max ni chepesi wakati ukiwa unascroll(kugusa kutoka kwenda chini) kwa sababu ya kuwa na refresh rate ya 120Hz
Kutumika kwa LTPO kunafanya kioo kidhibiti kiwango cha refresh rate kwani kikiachwa kama kilivyo inasababisha chaji kuisha haraka
Nguvu ya processor Apple A15 Pro
Kwa kutazama data za app ya Geekbench inaonyesha kuwa apple a15 pro ndio processor ya simu yenye nguvu kuliko zote kwa sasa
Kwa maana inaizidi hata ile chip iliyotumika kwenye Samsung Galaxy S23 Ultra
Ila kuna changamoto moja imejitokeza kwa watumiaji iPhone 15 Pro Max
Changamoto hiyo ni simu kupata joto sana baada ya muda mfupi wa matumizi
Apple wanadai baadhi ya apps zinaifanya processor ifanye kazi kupitiliza hivyo kusababisha processor kupata moto
Ila sababu kuu wanadai kuwa ni swala la software na sio uwezo wa chip
Sasa basi apple wamelizimika kutoa maboresho ya mfumo endeshi kutoka kutoka iOS 17 hadi iOS 17.0.3 kurekebisha tatizo
Upande wa utumiaji app zinazohitaji nguvu kubwa ya utendaji chip inafanya vizuri na haina mkwamo wowote
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iPhone 15 Pro Max ina ukubwa wa 4441mAh
Katika matoleo yote mapya hii ndio iphone yenye betri kubwa
Hivyo ukaaji wake wa chaji unachukuwa masaa mengi
Kutoka tovuti ya GSMArena, hii simu ukiwa upo unaperuzi intaneti muda wote inachukua masaa 24 mpaka kuisha
Hii ina maana kuwa kwa siku unaweza kuichaji simu mara moja tu
Hata iphone 15 pro max haiwezi kudumu muda huo ukiwa unacheza gemu, unaangalia youtube, ukiwa unatimua tiktok ama instagram
Kiuhalisia kwa matumizi simu inaweza kudumu kwa kipindi cha masaa 11 tu
Hivyo kwa mtumiaji mkubwa wa simu itamlazimu kuichaji simu mara mbili kwa siku
Kwenye kiepengele hiki Samsung Galaxy S23 Ultra iko njema
Ukubwa na aina ya memori
iPhone 15 Pro Max inakuja katika matoleo ya aina tatu na zote zina RAM ya GB 8
Kuna yenye GB 256, 512 na 1TB
Hivi viwango vinatosheleza kuhifadhi mafaili mengi na app za kutosha
Ndio maana simu za daraja la juu siku hizi haziji na sehemu ya memori kadi
Ila jua kuwa hii simu inaweza ikatumia flash ama external hard disk cha msingi isapoti waya wa USB Type C
Uimara wa bodi
Apple wametumia materio mapya kwenye bodi za iPhone 15 Pro Max
Bodi hizo ni za aina ya Titanium
Ilitarajiwa kuwa titanium kuwa ni ngumu kuliko matoleo yaliyopita ambayo yanatumia glasi
Kwa bahati mbaya matokeo yako kinyume
Titanium imeonyesha kuvunjika kwa urahisi ukilinganisha na iPhone 14 Pro Max
Kama ilivyo kawaida, simu hii ina viwango vya IP68
Kwa maana haiwezi kuingia maji kwa muda wa nusu hata ikiwa imezamishwa kwenye kina cha mita 6 kwa muda wa nusu saa
Ubora wa kamera
Simu ina idadi ya kamera zipatazo tatu ambazo ni za wide, ultrawide na telephoto
Kamera aina ya ultrawide inapiga eneo pana sana kwa mfano uwanja wa mpira wote
Telephoto kazi yake ni kupiga vitu ambavyo vipo mbali na kamera
Kamera yake inapiga picha vizuri hivyo usahihi wa rangi ni mkubwa
Yaani vitu vinaonekana kwa rangi zake harisi
Hakuna changachenga kwa nyakati za mchana
Na hata kwenye mwanga hafifu vitu vinaonekana kwa uzuri
Washindani wa iPhone 15 Pro Max
iPhone hii mpya haina tofauti kubwa na matoleo yaliyopita
Hii inamaanisha iPhone 14 Pro Max bado itaendelea kuwa simu yenye soko kubwa
Hivyo kuipa changamoto toleo jipya la iPhone
Kuna simu kali nyingine ya Samsung Galaxy S23 Ultra ambayo ukaaji wake wa chaji ni mkubwa
Hata kiutendaji hakuna tofauti inayoweza kuonekana kwa macho yenye utofauti mkubwa
Hitimisho
Kwa ujumla apple inatarajiwa kuendelea kushika hatatu kwenye kitengo cha simu za madaraja ya juu
Ila apple wana kazi ya kurekebisha changamoto za simu kupata moto ambazo zimelalamikiwa na watumiaji wengi
Hata hivyo hii ni simu kali
Maoni 3 kuhusu “Bei ya iPhone 15 Pro Max na Sifa Zake”
Iko vizu sana kwamuonekan
Naitajiii kujua nini maana ya LLA
LLA inamaanisha model ya iphone kwa ajili ya soko la marekani/canada (north america)