SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za vivo na bei zake 2022

Brand

Sihaba Mikole

March 2, 2022

Duniani kuna smartphones nyingi nzuri kwa sasa.

Na kampuni hasa za china zipo nyingi zinazotengeneza smartphone.

Ila kwenye soko  kuna kampuni chache maarufu zinazojulikana sana upande wa smartphone.

Kwenye simu za android Samsung inatawala na kwa Tanzania Infinix na Tecno Zimeteka soko.

Ila kuna kampuni zinatengeneza simu kali sana.

Moja wapo ni Vivo ambayo haijateka sana soko la Tanzania.

Simu za vivo huwa ni simu nzuri linapokuja swala la kamera na uwezo mkubwa wa processor.

Sifa nzuri za simu za vivo na bei zake huwa juu pale vivo inapotumia processor yenye nguvu mfano ni vivo tatu za mwanzo za kwenye orodha.

Utakubaliana na maoni ya hii post ukizitazama sifa za simu za vivo na bei zake kwenye orodha iliyopo.

Simu zilizopo zinatofautiana kisifa na bei.

Ni jambo la msingi kuzielewa hizo tofauti kwa kuzitazama sifa za kila simu ya vivo iliyopo kwenye orodha.

Vivo X70 PRO+

Simu ya Vivo X70 Pro plus ni moja ya simu yenye kamera bora kwa sasa.

Kamera ya Vivo X70 Pro+ inazizidi kamera ya samsung s22 ultra na Google Pixel 6

Vivo X70 Pro+ ikipiga picha kwenye mwenge hafifu vitu vinavyotokea kwenye picha vyote vinaonekana bila ukungu.

Na rangi nyeupe na vitu vilivyopo kwenye picha vinabalance vizuri.

Moja ya picha iliyopigwa na Dxomark Vivo, x70 Pro Plus inaonyesha kwa usahihi kitu kilicho mbali na kamera kwenye mwanga hafifu.

Processor ya simu ya X70 Pro+ ni aina ya octacore(core nane).

Inatumia chip ya Snapdragon 888+

Snapdragon 888 imeundwa kwa muundo wa Kryo 680.

Muundo wa Kryo 680 ni maalum kwa ajili ya kutenda kazi kubwa na nzito mfano kucheza gemu za vita au gari.

Muundo huo hufanya processor kuweza kusukuma applikesheni na gemu yoyote kwa urahisi bila kukwama.

Snapdragon 888 ina modem yenye uwezo wa mtandao wa 5G

Inakubali aina zote tatu za 5G.

Kioo cha vivo x70 pro plus ni cha LTPO AMOLED chenye refresh rate ya 120HZ.

Hivyo display ya simu hii inaonyesha vitu kwa rangi zake halisi na ni chepesi(smooth) kwa sababu ya kuwa na refresh rate kubwa.

Hii simu ina uwezo wa kuzuia maji kupenya ikiwa imedumbukia kwenye kina cha maji ya mita moja na nusu kwa muda wa nusu saa.

Maji hayaingii ndani ya simu ya X70 Pro+ kwa sababu ina IP68 ambayo ni waterproof.

Memori yake inatumia muundo wa UFS 3.1 ambao unasafirisha data kwa kasi sana.

UFS 3.1 inasaidia simu kuwaka kwa haraka na applikesheni kufunguka kwa haraka pia

Taarifa za memori unaweza ukaziona kwenye jedwari la sifa za simu ya vivo

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 888+ 5G
  • Core Zenye nguvu(4) – 1×3.0 GHz Kryo 680,3×2.42 GHz Kryo 680
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.80 GHz Kryo 680
  • GPU-Adreno 660
Display(Kioo) LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • Funtouch OS 12
Memori UFS 3.1, 256GB,512GB na RAM 8GB na 12GB
Kamera Kamera nne

  1. 50MP,Laser AF(wide)
  2. 8MP(periscope Telescope)
  3. 12MP(telephoto)
  4. 48MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
  • 4500mAh-Li-Po
  • Chaji-55W
Bei ya simu(TSH) 2,085,930/=

Simu ya Vivo S12 PRO

Processor ya simu ya vivo s12 pro imetengenezwa na MediaTek inaitwa Dimensity 1200.

Chipset ya Dimensity 1200 ina modem inayokubali mtandao wa 5G.

Core zenye nguvu zinatumia muundo wa Cortex A78.

Processor zenye Cortex A78 huwa zinatumia umeme kidogo wakati ikifanya kazi kubwa.

simu ya vivo s12 pro

Ndio maana simu ya Vivo S12 Pro inakaa na chaji muda mrefu japokuwa inatumia chip yenye nguvu kubwa

Na upande wa core zenye nguvu ndogo zinatumia Cortex A55.

Cortex A55 huwa zinatumia umeme kidogo sana na maalum kwa ajili ya kufungua apps ambazo hazihitaji nguvu kubwa kwa mfano kupiga simu, kutuma sms, kuangalia picha, kusikiliza miziki, kusoma vitabu vya pdf nk.

Kamera ya vivo s12 pro ina sensor kubwa.

Simu ina kamera nne ambazo zinakosa teknolojia zinazoongeza ufanisi wa kamera kwenye ulengaji na utulivu wakati wa kupiga picha na kurekodi video.

Kwa maana simu haina optical zoom, dual pixel pdaf au Laser AF na OIS.

OIS hutuliza video wakati ikirekodiwa huku anayerekodi akiwa anatembea.

Dual pixel pdaf huifanya kamera ya simu kulenga kitu kinachopigwa simu kwa usahihi sana kuliko PDAF.

Simu pia ina muundo wa memori wa UFS 3.1 ambao una kasi kubwa.

Mfumo wake wa chaji unajaza simu kwa haraka kwa sababu inapeleka umeme mwingi wa 44W.

Chini ya lisaa limoja simu inaweza kujaa.

Kioo cha vivo s12 pro ni cha amoled chenye refresh rate ya 90Hz.

Kioo cha hii simu kinaweza kuonyesha picha zenye ubora wa HDR10+

Baadhi ya sifa za vivo s12 pro na bei yake.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 1200 
  • Core Zenye nguvu(4) – 1×3.0 GHz Cortex-A78,3×2.6 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G77 MC9
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • Origin OS Ocean
Memori UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB na 12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(ultrawide)
  3. 2MP(macro)
  4. 50MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.56inchi
Chaji na Betri
  • 4300mAh-Li-Po
  • Chaji-44W
Bei ya simu(TSH) 1,104,300/=

Simu ya Vivo iQOO 9 Pro

Processor ya simu ya vivo iqoo 9 pro imetengenezwa na Snapdragon na inaitwa Snapdragon 8 gen 1.

Snapdragon 8 gen 1 ni processor yenye nguvu kubwa kiutendaji na inayosapoti mtandao wa 5G.

Kioo cha vivo iqoo 9 pro kinatumia teknolojia inayonyesha vitu kwa rangi zake halisi.

Ni display aina ya LTPO2 AMOLED.

simu ya vivo iqoo 9 pro

Mfumo wake wa memori aina ya UFS 3.1 pia una kasi kubwa ya kusafirisha data na unaofungua app, kuwasha simu na kuhifadhi mafaili kwa haraka na kwa kasi.

Kamera iQoo 9 pro ina mfumo mzuri wa kamera.

Kwa maana una OIS aina ya Gimbal OIS.

Kamera zake zinawezo kurekodi video za ubora wa 4K na 8K.

Hizi ni resolution kubwa sana.

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi sana wa wati 120W.

Umeme wa Wati 120 unajaza betri la simu ya vivo iqoo 9 pro lenye ujazo wa 4700mAh kwa 100% ndani ya dakika 20 tu.

Iwapo simu haitumiki sana, betri lake linakaa na chaji masaa 97.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 8 Gen 1
  • Core Zenye nguvu(4) – 1×3.00 GHz Cortex-X2,3×2.50 GHz Cortex-A710
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.80 GHz Cortex-A510
  • GPU-Adreno 730
Display(Kioo) LTPO2 AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • Funtouch 12
Memori UFS 3.1, 256GB,512GB na RAM 8GB na 12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 16MP(telephoto)
  3. 50MP(ultrawide)
  4. 16MP(selfie kamera)
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
  • 4700mAh-Li-Po
  • Chaji-50W
Bei ya simu(TSH) 1,938,090/=

Simu ya Vivo Y33s 5G

Simu ya Vivo Y33s 5G  ni moja simu za 5g za bei nafuu kwa wakati huu.

Bei yake ni nafuu kwa sababu zifuatazo.

Processor ya Vivo Y33s 5g ni processor yenye ubora wa wastani(kundi la kati) ya MediaTek Dimensity 700.

Haitumii vioo bora vya AMOLED bali inatumia teknolojia ambayo kwa sasa inaonekana wakati wake kuisha.

simu ya vivo y33s 5g

Display ya vivo y33s ni IPS LCD.

Mfumo wake wa memori una kasi ya wastani ya kusafirisha data kutoka na kutumia na kutumia UFS 2.1 inayozidiwa na UFS 3.1

Simu ina kamera mbili upande wa nyuma.

Kamera zake zinapiga video za full hd na sio za ubora wa 4K(hujulikana pia kama Ultra HD)

Kamera ambazo hazina vitu muhimu vinavyoongeza ufanisi na ubora wa kamera.

Simu inakosa uwezo wa kuzuia maji kupenya endapo simu ikiingia kwenye maji ya kina kirefu.

Na imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na kioo chake si cha Gorilla glass 6 ambacho huwa ni kigumu kupasuka.

Ukitaka kujua ubora wa vioo vya Gorilla fuatilia simu za iPhone 13 Pro Max na Samsung Galaxy S22 Ultra

Mfumo wa chaji unapeleka umeme wa wastani wa wati 18W.

Hivyo betri lake kubwa lake kubwa la 5000mAh linachukuwa masaa takribani matatu kujaa.

Sifa za vivo y33s zilizopo kwenye jedwari zinaweza zidiwa na simu ya infinix zero 5g

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 700 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 12
  • Origin OS Ocean
Memori UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB na 4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,AF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 13MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 461,400/=

Simu ya Vivo V23 Pro

Simu ya Vivo V23 Pro ni simu ya 5g yenye uwezo mkubwa kiutendaji ambayo inatumia toleo jipya la Android 12.

Ubora wa vivo v23 pro unachangiwa na mengi ambayo yanasababisha bei ya vivo v23 pro kuzidi shilingi milioni moja.

Processor ya simu ya vivo v23 pro ina nguvu kubwa ya kufungua app yoyote.

Inatumia processor ya MediaTek Dimensity 1200.

simu ya vivo v23

Kioo cha 23 pro ni cha amoled kinachoonyesha rangi za picha kwa usahihi mkubwa na ni chepesi sababu ya kuwa na refresh rate ya 90Hz.

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi wa wati 44W.

Wati 44W unajaza simu mapema sana.

Kamera zake zina resolution kubwa ila ufanisi wake si mkubwa kwa sababu ya kukosa teknolojia ya dual Pixel PDAF na OIS na hata optical zoom.

Simu inatumia mfumo wa memori wa wakawaida unaosafirisha data kwa kasi ya kwaida.

Baadhi ya sifa za simu ya vivo v23 pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 1200
  • Core Zenye nguvu(4) – 1×3.0 GHz Cortex-A78,3×2.6 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G77 MC9
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 12
  • Funtouch 12
Memori 128GB,256GB na RAM 8GB na 12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(ultrawide)
  3. 2MP(macro)
  4. 50MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.56inchi
Chaji na Betri
  • 4300mAh-Li-Po
  • Chaji-44W
Bei ya simu(TSH) 1,226,000/=

Simu ya Vivo Y33t

Simu ya vivo Y33t ni simu inayotumia android 11 na Funtouch 12 na yenye ubora wa kati ambayo bei ingetazamiwa kuwa chini ya laki nne.

Bei ya vivo y33t ni kubwa ukilinganisha na sifa za simu hii ambazo zimeonyeshwa kwenye jedwari.

Kwanza, inatumia processor ya daraja la kati ya Snapdragon 680 ambayo haina mtandao wa 5G.

Processor ya simu ya vivo y33t inatumia muundo wa Kryo 265

Ni aina ya processor inayotunza chaji muda mrefu na ina nguvu ya wastani.

simu ya vivo y33t

Hivyo simu inakuwa na uwezo wa wastani.

Bodi ya simu imeundwa kwa plastiki na si kwa vioo vya gorilla glass vinavyoimarisha uwezo wa simu kudumu muda mrefu.

Kioo chake ni IPS LCD  na si amoled.

Inatumia mfumo wa memori unaosafirisha data kwa kasi ya kawaida.

Mfumo wa chaji ya vivo y33t unapeleka umeme wa wastani wa wati 18W.

Umeme wa Wati 18 unajaza simu ya betri 5000mAh kwa muda mrefu.

Baadhi ya sifa za vivo y33t

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • Funtouch 12
Memori 128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 16MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.58inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 581,000/=

Simu ya Vivo Y21

Simu ya vivo y21 ni simu ya daraja la chini ambayo bei ya inafikia laki nne.

Sifa za vivo y21 zinafanya simu kuwa sio smartphone ya bei rahisi.

Sababu processor ya y21 ina nguvu ndogo kutokana core zote nane(octacore) kutumia muundo wa Cortex A53.

Processor yake ni MediaTek Helio P35 inasapoti 4G hivyo simu haina mtandao wa 5G.

simu ya vivo y21

Haitumii vioo vya amoled bali ni vioo vya ips lcd vyenye changamoto ya kuonyesha rangi halisi.

Mfumo wa memori wa vivo y21 unasafirisha data kwa kasi ya wastani.

Vivo y21 imeundwa kwa plastiki na inakosa IP68 yaani haiwezi zuia maji kupenya.

Simu ina kamera mbili ambazo haziwezi piga eneo pana sana na picha ya mbali.

Na pia ufanisi wa kamera ni mdogo kutokana kutokuwapo kwa teknolojia bora za autofocus kama dual pixel pdaf.

Kamera yake haizwezi piga picha za ubora wa ultra hd yaani 4K

Simu inakaa na chaji muda mrefu kwa sababu betri ni kubwa la 5000mAh na chip ya Helio P35 inatumia umeme mdogo.

Wakati wa kuchaji simu itachelewa kujaa kutokana na chaji kupeleka umeme wa wati 18.

Baadhi ya sifa za vivo y21

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio P35
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.35 GHz Cortex-A53
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.8 GHz Cortex-A53
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • Funtouch 11.1
Memori  128GB,64GB na RAM 4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 8MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 428,000/=

Simu ya Vivo Y21e

Simu ya vivo y21e ni simu ya 4g ambayo mfumo wake endeshi ni Android 11 na Funtouch 12.

Vivo y21e ni simu ya daraja la kati yenye bei inayovumilika inayofikia laki tatu na tisini.

Kwa nini simu ya vivo y21e ni simu nzuri ambayo bei yake inavumulika?

Processor ya vivo y21e ina nguvu ya wastani inayoweza kusukuma app nyingi bila kukwama.

simu ya vivo y21e

Inatumia processor ya snapdragon 680 iliyotumika kwenye simu Vivo y33t inayouzwa zaidi ya laki tano.

Mfumo wake wa memori una uwezo kusafirisha data kwa wastani kama zilivyo simu zingine zilizotangulia.

Kioo cha vivo y21e ni cha ips lcd hivyo ubora wa rangi si mkubwa.

Simu ina kamera chache zinazoweza kupiga eneo la upana mdogo(wide) na vitu vya karibu sana(macro) pekee.

Lakini kamera zake hazina teknolojia nzuri ya kulenga vitu vinavyopigwa picha wala uwezo wa kuzoom picha bila kupoteza ubora wa picha.

Betri ya vivo y21e lina ukubwa wa 5000mAh linachongia simu kutunza moto muda mrefu.

Kwa bahati mbaya chaji yake inapeleka umeme mdogo wa wati 18W hivyo betri inachukua muda mrefu kujaa.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • Funtouch 12
Memori 64GB na RAM 3GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 8MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 384,500/=

Simu ya Vivo Y32

Simu ya vivo y32 ni simu yenye 4g bila kuwa na mtandao wa 5g.

Vivo y32 ni simu unayoweza kuimiliki kutokana na kuuzwa kwa bei nafuu ya kiasi cha laki tatu na sitini.

Sifa za simu ya vivo y32 zinazizidi sifa za vivo y21e ambayo inauzwa ghali.

Ni kivipi vivo y32 ina ubora wa mkubwa kuliko vivo y21e?

simu ya vivo y32

Processor ya simu ya vivo y32 snapdragon 680 inayotumia muundo wenye nguvu za wastani wa Kryo 265.

Mfumo wa memori wa Vivo Y32 ni UFS 2.1 unachagiza simu kuwa na kasi kubwa ya kufungua app na kuhifadhi mafaili.

Haya mambo mawili yanaifanya simu kuwa na unafuu na tofauti na simu iliyotangulia.

Sifa zingine kama kamera na chaji zipo sawa na Vivo y21e

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • OriginOS 1.0
Memori UFS 2.1, 128GB,64GB na RAM 8GB, 6GB na 4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,AF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 8MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 358,900/=

Simu ya Vivo Y76s

Simu ya Vivo Y76s ni simu ya 5g inayotumia mfumo endeshi wa Android 11 na OriginOS.

Vivo Y76s ni simu ya daraja la kati(mid range) ambayo inatumia Processor yenye nguvu.

Processor iliyotumika kwenye simu hii ni Dimensity 810 5G.

Ina core mbili zinatumia muundo unaotumia umeme mwingi.

simu ya vivo y76s

Muundo huo ni Cortex A76 wenye nguvu kubwa kiutendaji.

Kamera zake zinaweza kupiga eneo sio kubwa sana kwa sababu haina kamera ya ultrawide.

Kamera zake hazina OIS wala dual pixel japokuwa zina megapixel nyingi.

Vivo y76s haitumii vioo bora vya amoled bali inatumia ips lcd.

Ina mfumo mzuri wa memori wa Vivo y76s unasafirsha na kuhifadhi vitu kwa kasi ya kawaida.

Simu ya vivo y76s ina chaji inayojaza betri lake la 4100mAh kwa haraka.

Chaji ya vivo y76s inapeleka umeme wa 44W.

Umeme wa 44W unaweza kujaza betri chini ya lisaa limoja

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g na 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 810 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • OriginOS
Memori  128GB,256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera mbili

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 8MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 4100mAh-Li-Po
  • Chaji-44W
Bei ya simu(TSH) 615,200/=

Maoni 3 kuhusu “Simu za vivo na bei zake 2022

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

No Featured Image

Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa Kwa maana […]

OnePlus 11R

Simu 15 za OnePlus na Bei zake (Aina zote)

OnePlus inaweza ikawa ni jina geni kwa watumiaji wengi smartphone Tanzania Ila OnePlus ni moja ya kampuni kutoka china inayotengeneza simujanja za madaraja ya kati na ya juu Simu nyingi […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company