Fold ni aina ya simu za kujikunja.
Kwa muda mrefu makampuni ya Samsung, Huawei na Oppo wamekuwa wakitengneza simu za aina hii
Hivi karibuni tecno na pixel pia zimeingia katika uzalishaji wa simu za fold
Google wametoa simujanja ya fold inayotambulika kama Google Pixel Fold
Kikawaida simu za kukunja huuzwa kwa gharama kubwa
Kwa maana hiyo bei ya google pixel fold inazidi milioni nne kwa Tanzania na duniani kwa ujumla
Bei ya Google Pixel Fold
Simu ina miezi miwili tangu ilipoachiwa
Bei yake ni shilingi milioni nne na laki tano (4,500,000)
Ni bei inayoendana na simu za samsung fold
Ni kiasi kikubwa cha pesa ukilinganisha na kipato cha watanzania wengi
Ila kwa mwenye uwezo, atapata simu yenye ubora katika utendaji, kamera, kioo chenye kuonyesha vitu vingi kwa wakati mmoja na kwa ukuibwa, na memori kubwa yenye kutosheleza kuhifadhi vitu vingi
Ni moja ya simu nzuri ukiangalia sifa ilizo nazo.
Sifa za Google Pixel Fold
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Foldable OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB,512GB,na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-7.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 4,500,000/= |
Upi ubora wa Google Pixel Fold
Kioo chake kina uwezo wa kuonyesha vitu kwa ukubwa kama ukikunjua
Inatumia kioo chenye ustadi mzuri kwenye uwasilishaji wa rangi
Ina betri kubwa ya kukaa na chaji muda mrefu
Mfumo wake wa kamera ni mzuri kwenye upigaji picha na kurekodi video
Utendaji wake ni mkubwa kwa sababu simu ina chip yenye nguvu
Inatumia muundo wa memori wenye kasi ya kusafirisha data kwa haraka
Mfumo wa chaji unapokea umeme mwingi unaoweza kujaza betri kwa muda mfupi
Uwezo wa Network
Google Pixel Fold ni simu ya 5G kama ilivyo kwa matoleo mengine ya daraja la kati na la juu za siku hizi
Na inasapoti pia aina zingine za network
Hii simu inakubali aina zote za 5G zikiwemo zinazotumiwa na mitandao ya simu nchini
Hivyo basi 5G ya Vodacom, airtel na Tigo hazitokuwa na shida kwenye pixel fold
Hata hivyo, 5g haijasambaa sana hapa nchini
Inapatikana tu baadhi ya maeneno ya Dar Es Salaam
Upande wa 4G inatumia LTE Cat 24 ambayo kasi yake ya kudownload 2Gbps
Kwa bahati mbaya 4G ya maeneo mengi duniani haifiki kasi hii
Hii ni kasi inayopatikana kwenye 5G aina ya mmWave
Ubora wa kioo cha Google Pixel Fold
Kioo cha google pixel fold kina upana wa inchi 7.6 kikiwa kimekunjuliwa
Huu upana ni pungufu kwa kima cha inchi 2.4 wa vioo vya vishikwambi walivyopewa walimu
Ila zingatia kuwa resolution ya kioo cha google fold ni kubwa na ina kioo cha Amoled
Yaani muonekano wa vitu ni mzuri kutokana na kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Kwani ina HDR10+ na pia refresh rate yake inafika 120Hz
Kwa maana utakapokuwa unatachi skrini utaona simu kuwa ipo nyepesi
Uang’avu wa kioo unafika nits 1000
Nits 1000 inasaidia skrini kuonyesha vizuri hata ukiwa juani
Nguvu ya processor Google Tensor G2
Simu ya Google Pixel Fold imewezeshwa utendaji na chip ya Google Tensor G2
Matoleo mapya ya google yanatumia processor zinazoundwa na goole wenyewe wakati zamani zilikuwa zinatumia chip za snapdragon
Ina idadi ya core nane ambazo zimegawanyika katika sehemu tatu
Core yenye nguvu sana ni aina ya Cortex X1
Kwenye app ya kupima nguvu za processor ya geekbench 6, google tensor ina wastani za alama 1400
Hiki ni kiwango kinachoshahabiana na processor ya iPhone 14 Pro Max iitwayo Appple A15 Bionic
Ndio maana gemu zinacheza kwa fremu nyingi
Na kila aina ya app inafunguka pasipo kugandaganda
Uwezo wa betri na chaji
Betri yake ina ukubwa wa 4821mAh
Ukubwa wa betri hautofautiani sana na betri nyingi za siku hizi ambazo zina ukubwa wa 5000mAh
Hii ina maana kuwa ukaaji wa chaji unazidi masaa 12 ukiwa kwenye intaneti muda wote
Chaji inasapaoti mfumo wa PD3.0 yenye uwezo wa kupokea umeme wa wati 100
Ukiwa na chaji yenye kasi hiyo simu inaweza kujaa ndani ya dakika 25
Pia hii simu inasapoti wireless chaji
Ukubwa na aina ya memori
Matoleo ya Google Pixel Fold upande wa memori yapo mawili yenye ukubwa wa RAM ya GB 12
Kuna yenye GB 256 na GB 512 ambazo ni kubwa na zinaweza hifadhi vitu vingi
Inatumia memori aina ya UFS 3.0
Kasi ya UFS 3.0 kwenye kusafirisha data ni 2400MBps
Kwa maana kama unakopi kitu kwenda kwenye hii simu kitamalazika ndani muda mfupi
Uimara wa bodi ya Google Pixel Fold
Google ni simu imara kwani ina viwango ip vinavyoonyesha uwezo kwa kuzuia maji kuingia ndani ya simu pindi ikizama kwenye maji
Lakini jua simu inapaswa itolewe kwenye maji ndani ya nusu saa
Kwenye skrini kuna protekta ya kioo cha Corning Gorilla Glass Victus
Wenyewe gorilla wanadai kuwa ni ngumu kioo kupasuka pale simu inapodondoshwa kwa kimo cha mita mbili
Hata umakini ni muhimu kwenye matumizi ya simu
Ubora wa kamera
Simu ina idadi ya kamera zipatazo tatu
Kuna kamera ya kupiga eneo pana, na umbali mrefu yaani telephoto
Kamera kuu na ya telephoto zina ulengaji wa dual pixel pdaf
Uwepo wa hii kitu unafanya simu kuweza kukilenga kitu kwa ustadi na kukusanya data sahihi za kinachopigwa picha
Ubora wa picha nyakati za mchana ni mkubwa na wa kustaajabu
Rangi za vitu vinaonekana kwa usahihi mkubwa na unaoendana na uhalisia
Ubora wa picha unapungua ikiwa simu inapiga kwenye kiza kingi sana
Ubora wa Software
Google Pixel Fold inatumia mfumo wa Android 13 asilia (stock android)
Kutokana na simu kuweza kutanuka, google wameweza kutumia faida ya uwepo wa kioo kipana
Kwani inakupa uwezo wa kutenganisha skrini na kutumia app mbili kwa wakati mmoja
Kwa mfano, upande wa kushoto ukawa unaangalia video youtube na upande wa kulia ukawa unaandika barua
Upana wa kioo unatoa fursa kubwa ya kutumia app nyingi kwa wakati mmoja bila shida
Washindani wa Google Pixel Fold
Mshindani mkubwa wa pixel si mwingine bali ni samsung fold
Google pixel Fold ina kimo kidogo ambacho ni inchi 5.8
Ila samsung galaxy z fold 5 urefu wake ni 6.2
Hiki ni kitu kimoja wapo kinachoweza mfanya mtu aaachane na pixel
Na pia samsung galaxy z fold 5 zinaboreka kadri matoleo mapya yanavyotoka
Neno la Mwisho
Ushindani kwenye simu za kujikunja unazidi kuimalika
Changamoto ni kuwa bei za hizi simu ni kama zinalenga watu wachache wenye kipato kizuri
Ukiangalia bei ya google pixel fold inamfaa mtumiaji mwenye bajeti kubwa
Na bei yake inaendana sana na ubora ila bei hii unapata matoleo mazuri ya simujanja za kawaida na chenji inabaki
Ila kama unataka kuonja teknolojia ya folding sio mbaya kununua
Maoni 2 kuhusu “Ubora na bei ya simu mpya ya Google Pixel Fold”
Simu poa sana hii watuletee na za laki tano labda tutanunua
Labda baada ya miakq mingi