Oppo A78 5G ni simu nyingine ya 5G inayouzwa kwa bei nafuu ukilinganisha na simu zinazotumia mtandao
Ni simu ya mwaka 2023 na inakuja na baadhi ya vitu vipya ambavyo havikuwepo kwenye oppo A77
Bei ya Oppo A78 5G kwa Tanzania inazidi laki sita pia inategemea na mkoa uliopo
Bei inaonekana kuwa ni kubwa ila ukilinganisha na simu nyingi za 5G, bei hii nafuu
Ina sifa zinazochuana na simu ya Redmi Note 10 5G ila redmi inauzwa chini ya laki nne
Kuna sababu za msingi zinasobabisha bei ya oppo kuwa kubwa hasa ukitazama sifa za hii simu
Bei ya OPPO A78 5G ya GB 128
Kwa Tanzania unaweza kuimiliki simu kwa bei ya shilingi 610,000/=
Si bei rafiki kwa mtu anaetaka simu ya laki mbili
Uwepo wa 5G na mfumo mzuri wa kamera ndio unaosababisha bei ya hii simu kufika huko
Kama isingekuwa na vifaa vya kawaida kwa kiwango kikubwa ungeweza kuinunua simu kwa bei chini ya laki nne
Vinginevyo huna budi kujichanga kumili simujanja yenye 5G
Sifa za Oppo A78 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2,128GB na RAM 8GB na 4gb |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 610,000/= |
Upi ubora wa Oppo A78 5G
A78 inakaa na chaji muda mrefu sabau ya uwepo wa betri kubwa
Inakuja na chaji yenye kasi inayojaza betri kwa muda mfupi
Inasapoti mtandao wa 5G na inadownload mafaili kwa kasi kubwa
Ina ulinzi wa kuzuia manyunyu ta maji
Kamera zake zinatoa picha nzuri hasa nyakati za mchana
Inakuja na mfumo endeshi mpya wa android
Uwezo wa Network
Kama jina la simu linavyooleza ni kuwa utaweza kutumia 5G bila shida
5g ya OPPO A78 spidi yake inafika zaidi ya 1000Mbps hasa ukiwa nje
Ukiwa ndani ya jengo spidi inashuka mpaka mpaka 500Mbps
Mawimbi ya 5G huwa yanapata changamoto pale inapokutana na kigingi kama ukuta
Ila hata hivyo spidi ya 500Mbps ni kubwa kwa sababu ukipakua gemu la GB 1.2 kule playstore inachukua sekunde 30 tu kumaliza
Hiki kitu ni kigumu kukipata kwenye 4G ya mitandao ya hapa Tanzania
Bahati mbaya kuwa 5G Tanzania ndio kwanza ipo hatua za mwanzoni bado haijasambaa sehemu kubwa hata kwa mji kama Dar Es Salaam
Ubora wa kioo cha Oppo A78 5G
Kioo cha hii simu ni cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1080 pixels
Na kinasapoti refresh rate ya 90Hz ni kama tu ilivyo kwa simu Tecno Spark 10 Pro
Refresh rate 90Hz husaidia simu kuwa “smooth” na nyepesi wakati ukiwa unatachi kioo mfano kuangalia picha za instagram picha zinakuwa zinadirika kwa mwendo mzuri na wa haraka
Ila kuna kasoro kwenye hii simu upande wa kioo
Resolution ni ndogo ukilinganisha na bei lakini pia kutumia kioo cha IPS LCD ni kama simu imeshushwa hadhi
Kwa bei iliyoanishwa simu ilipaswa kuwa na kioo cha amoled na resolution kubwa
Resolution ndogo husababisha muonekano usiovutia kwa baadhi ya vitu
Yaani kuna vitu vinakuwa vinaonekana vikubwa kwenye simu sababu ya mkusanyiko mdogo wa pixel kwa kila inchi
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 700
Oppo A78 5G inatumia processor ya MediaTek Dimensity 700 kufanya kazi zake
Ina nguvu ya wastani kutokana na muundo wake wenye nguvu kutumia Cortex A76 yenye kasi inayofika 2.2GHz
Kwa viwango vya sasa chip zenye nguvu huanza kutumia Cortex A78 na matoleo mengine mapya
Kwa mpenzi wa magemu makubwa, atalazimika kucheza kwa resolution za chini kuepuka kugandaganda na simu kupata moto
Ukicheza kwa resolution za juu simu itapata shida hata kufika kwa frem 30 na hali ya kuganda ganda itakuwa inatokea
Dimensity 700 ina ufanisi mkubwa kwenye matumizi ya betri
Nguvu yake ni ya wastani na ndio maana betri inachelewa kuisha
Uwezo wa betri na chaji
Oppo A78 5G ina betri kubwa ya 5000mAh na inakuja na chaji ya 33W wanaita supervooc
Chaji yake inajaza betri kwa asilimia 100 kwa karibu masaaa mawili
Hii kasi inakaribiana na simu na simu ya Samsung Galaxy A14 5G
Ukiwa unaangalia video muda wote na ukaseti mwanga kwa kiwango cha juu kabisa simu inachukua masaa 12 kuisha chaji
Na ukiwa unaitumia matumizi madogo inaweza mpaka siku mbili chaji kuisha
Kwa kifupi uwezo wa Oppo A78 5G kutunza chaji ni wa kuridhisha isipokuwa kasi ya chaji ni tofauti na kiwango cha wati chaji inayopeleka
Ukubwa na aina ya memori
OPPO hii mpya inatumia memori aina ya UFS 2.2 ambazo huweza kusoma na kuandika data kwa kasi ya 1200MBps
Kasi hii inafanya mafaili kuhifadhiwa kwa haraka wakati unatumia 5G
Na pia ukiwa unakopi faili kwenda kwenye simu basi kitendo hiki kitachukua muda mfupi sana
A78 5G ipo ya aina moja upande wa memori na yenyewe ina GB 128 na RAM GB 8 au GB 4
Ni ukubwa sahihi kuhifadhi vitu vingi ndani ya simu
Uzuri mwingine ni kuwa simu ina sehemu ya kuweka memori card
Hivyo ikijaa utaongeza nafasi kwa kununua memori kadi
Uimara wa bodi ya OPPO A78 5G
Bodi ya oppo a78 5g ina uwezo wa kuzuia maji tiririka kama yale ya mvua
Kwani ina viwango vya IP54
Ila haiwezi zuia maji kama simu ikizama kwenye kina cha maji mengi
Upande wa nyuma simu ina plastiki wala haina kioo
Ni muhimu kuwa na kava ili rangi isichunike kirahisi
Ubora wa kamera
Simu inakuja na kamera mbili pekee moja ikiwa na megapixel 50 na nyingine ina megapixel 2
Kiuhalisia simu ina kamera moja tu kwa sababu kamera ya depth haipigi picha
Huwa inatumia kukotoa umbali kati ya kamera na kinachopigwa picha
Depth sensor haina umuhimu kwa miaka na sijui kwa nini kampuni bado wanaendelea kuziweka
Ubora wa picha ni wa kiwango kizuri kiasi fulani kwa nyakati zote za usiku na mchana
Kiwango cha chengachenga(noises) ni ngumu kuziona ila zipo
Na usahihi wa rangi na utofautishaji kati ya rangi nyeusi na nyeupe ni wa kuridhisha
Ukitumia AI muonekano wa picha unakuwa hauwendani na picha halisi
Upande wa video simu inaweza kurekodi video za full hd pekee
Ubora wa Software
Oppo A78 5G inatumia mfumo wa Android 13 na mfumo wa ColorOS 13
Mfumo wa coloros ni mzuri na unakuja na apps zingine za ziada
Changamoto utakayokutana nayo ni matangazo kwa njia ya notification
Yapi Madhaifu ya A78 5G
Mfumo wa kamera wa hii simu unakosa kamera ya Ultrawide
Kamera ya ultrawide huwa inapiga picha eneo pana sana mfano uwanja wa mpira
Matangazo kwenye mfumo wa software ni kitu kinachokera
Ukizingatia bei ya simu ni kubwa hakukuwa na haja ya kuwa na matangazo mengi
Chaji yake inachukua muda mrefu ukilinganisha na wati za chaji
Chip yake si nzuri kucheza gemu nzito kwenye resolution kubwa
Neno la Mwisho
Matoleo ya 5g ya bei ya kati yanazidi kuachiwa ikiwemo OPPO A78 5G
Sio mbaya ukajiandaa wakati ukisubiria 5G kuenea maeneo mengi
Mpenzi wa kamera na utendaji, hii simu inakidhi hitaji lako kwa kiasi kikubwa
Ila ukiona huielewi kuna mbdadala kama Mi 11 , Realme 10 na hata OPPO Reno8 5G
Maoni 2 kuhusu “Bei ya Oppo A78 5G na Sifa Zake Muhimu”
Shida ya simu hii haizimiki ikiwekwa chaji na ukizima ukiisha weka chaji na kuwasha umeme inajiwasha yenyewe
Tunaomba bro ipunguzwe