Kwa miaka ya karibuni baadhi ya makampuni ya simu yamekuwa yakiachia simu za kujikunja yaani Fold
Simu hizi ukikunjua upana wa screen unaongezeka na ukikunja upana unakuwa wa simu ya kawaida
Na inakuwa na screen mbili, mbele na ndani
Moja ya simu hiyo ni Samsung Galaxy Z Fold 4 ya mwaka 2022
Simu za kujikunj(Fold) a huwa zinakuwa na gharama kubwa bila kujali kampuni
Mfano bei ya samsung galaxy z fold 4 inazidi milioni tatu kutegemeana na ukubwa wa memori
Bei ya samsung galaxy z fold 4 ya gb 512
Galaxy Z Fold ya Gb 512 na RAM GB inaenda shilingi 3,500,000/=
Kwa baadhi ya wauzaji wa Tanzania bei inaweza kuwa kubwa zaidi
Muundo wasimu unachangia bei kuwa kubwa Sana
Kwa mfano, upande wa vioo kuna display mbili amabapo vioo vyote ni vya AMOLED
Vioo vya AMOLED vinatengezwa kwa gharama za juu.
Sasa ukijumlisha na sifa zingine zote utagundua kuwa sio rahisi kuipata hii kwa bei ndogo.
Sifa za Samsung Galaxy Z Fold 4
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Foldable Dynamic Amoled 2x, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB,512GB,1TB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-7.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,500,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy Z Fold 4
Hii ni simu yenye utendaji wenye nguvu kutokana nakutmia processor yenye nguvu
Simu Ina kupa uhuru kutokana na kuwa na screen kubwa inayoweza kufanya kazi nyingi yaani multtask
Kwa maana unaweza kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja
Ina vioo viwili kimoja Cha kujikunja na chingine Cha kawaida
Ni simu nzuri kwa wanaopenda kusoma vitabu kutokana na upana wake
Uwezo wa Network
Samsung Galaxy Z Fold 4 Ina uwezo wa kutumia mtandao wa 5G
Hii inamaanisha 3g na 4g pia inaweza kufanya kazi
Inakubali masafa yote ya 5G ikiwemo Yale yenye mask Sana aina ya mmWave
Kwenye eneo lenye minara ya mmWave simu inaweza kupakua mafaili kwa Kasi inayozidi 1gbps
Kwa bahati mbaya kwa Tanzania kuna mtandao mmoja tu wenye 5g kwa maeneo machache.
Na 5G iliyopo ni ya Masafa ya kati, inawezekana mbeleni mambo yakabadilika
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy Z Fold 4
Galaxy Z Fold 4 inatumia kioo Cha dynamic Amoled chenye resolution ya 1812 x 2176 pixels
Na pia kina refresh rate inayofika 120Hz kitu kinachofanya kioo kuwa na unyororo flani wakati wa kutachi bass ukiwa unaperuzi vitu mfano meseji
Ubora mwingine ni kioo kuwa na HDR10+ hii ni teknolojia inayotengeneza utofauti sahihi kati ya sehemu yenye mwanga mkubwa na sehemu zenye kiza
Hii inahakikisha muonekano wa vitu unaendana na jinsi vinavyoonekana kwenye mazingira halisi
Refresh rate ikiwa kubwa kunakuwa na matumzi makubwa ya betri
Lakini kioo Cha hii simu hakitumii refresh kubwa muda wote
Maana kuna kazi zingine zinaitaji kiwango kidogo Cha refresh rate
Hivyo ni kioo chenye urahisi katika matumzi ya chaji
Nguvu ya processor Snapdragon 8+ Gen 1
Snapdragon 8+ Gen 1 ndio processor inayoiwezesha Samsung Galaxy Z Fold 4 kufanya kazi zake
Hii ni processor yenye core ambazo zimegawanyika sehemu tatu
Kuna sehemu moja yenye nguvu sana ambalo hufanya kazi pale simu inapofungua vitu vingi Sana au ukiwa unacheza gemu
Magemu hutumika nguvu kubwa ndio maana huhitaji core yenye nguvu sana
Core hiyo yenye nguvu kubwa zaidi kwenye hii simu huitwa Cortex X2 na Kasi yake inafima 3.19GHz yaani mizunguko bilioni tatu na zaidi kwa sekunde
Ndio maana gemu la Call of Duty Mobile inacheza kwa 60fps kwa graphics zenye resolution kubwa Sana yaani ultra
Hii inamaanisha simu haiwezi kuganda Ganda unapocheza magemu mazito
Uwezo wa betri na chaji
Kutokana na ukubwa wa simu unaweza ukazani betri yake itakuwa kubwa lakini la hasha.
Betri yake Ina ukubwa wa wastani wa 4400mAh
Lakini itakushangaza kuwa hii ni moja ya simu yenye utendaji wenye nguvu unaokaa na chaji muda mrefu
Hii simu inaweza kukaa na chaji takribani masaa 15 ikiwa kwenye intaneti muda wote mfululizo.
Chaji yake Ina Kasi ya wastani ila inaweza kujaza betri kwa haraka kwa sababu betri lenyewe sio kubwa sana
Kwa mujibu wa data za GSMArena, Samsung Galaxy Z Fold 4 inajaa kwa asilimia 50 kwa muda wa nusu saw
Hii inamaanisha kuwa simu inaweza kujaza kwa 100% ndani ya dakika 120
Kumbuka kuwa chaji yake ni ya watu 25 tu
Ukubwa na aina ya memori
Unapotaka kujua simu yenye utendaji mkubwa basi aina ya memori ni mambo la muhimu kulijua.
Fold 4 inatumia memori za UFS 3.1 ambazo huwa Zina Kasi Sana japo si kama UFS 4
Kwa memori hii, simu itakuwa inafungua app kwa haraka, inawahi kuwaka na mafaili yanakopika kwa muda mfupi
Kuna matoleo matatu ya hii simu upande wa memori na zote Zina RAM ya GB 12
Kuna Z Fold 4 ya GB 256, 512 hadi 1TB
Na Haina sehemu ya ziada ya kuweka memori
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy Z Fold 4
Pamoja na kuwa hii ni simu ya kujikunja ila simujanja isiyopitisha maji
Kwani Ina viwango vya IPX8 inayomaanisha kuwa maji hayawezi kuingia kama itaingia kwenye maji ya kina Cha MITA 1.5 kwa muda wa nusu saa
Pia simu imewekewa kioo Cha gorilla victus+ ni vioo ambavyo vimetengenezwa kuhimili mipasuka na michubuko
Kiujumla Galaxy z fold 4 ni simu ngumu na inaweza kudumu miaka mingi hats ukaja kuiuza kwa bei rafiki ikiwa imeshatumika
Ubora wa kamera
Hii ni simu yenye kamera zipatazo tatu
Kamera zake zinakuwezesha kupiga picha eneo Pana Sana na kukiliga picha kitu ambacho kitu kilicho mbali Sana
Ubora wa picha ni mkubwa kwa nyakati zote
Na uhalisia wa rangi ni WA kiwango sahihi, sehemu yenye kivuli inaokana vizuri bila kuathiriwa na mwanga mwingi wa just
Kamera zake zinaoa picha bila chengachenga ikiwa unachukua picha nyakati za usiku
Vitu vinatokea kwa ustadi na hata kurekodi video simu inatumia kutokana na uwezo wa OIS
OIS hutuliza kamera kama ukiwa unarekodi video Hulu ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Samsung Galaxy Z Fold 4 inatumia android 12l na mfumo wa One UI 5.1
Vitu vingi vinapatikana kwenye hii simu ila Cha kuvutia ni jinsi mfumo unavyoweza kutumia vizuri upana wa kioo.
Mfumo wa simu unaruhusu kutumia app zaidi ya moja tofauti na tablet nyingi
Kwa maana unaweza kuweka YouTube upande wa kushoto na upande wa kulia unachati
Kitendo hiki kinaitwa multitasking
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy
Hii simu Ina mapungufu machache kama vile kutokuwa na sehemu ya memori, redio na sehemu ya earphone
Hata matoleo ya simu hizi ya bei ya juu hayaji na hivyo vitu
Ikiwa unahitaji kuwa navyo gharama ya ziada lazima ilipwe
Neno la Mwisho
Samsung Galaxy Z Fold 4 ni simu ya mwaka 2022 ila ni toleo Kali hata kwa mwaka 2023
Changamoto kubwa ni bei ila kwa anaependa kitu kizuri hii ni moja ya simu ya kuwa navyo kwa mwaka huu.
Wazo moja kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy Z Fold 4 na Ubora wake kiundani”
Hii galaxy iko vzuri sana labda bei kuwa juu