Simu ya iPhone 14 Plus ni iphone ya mwaka 2022 ambayo bado ni mpya kwa mwaka 2023
Bei ya iPhone 14 Plus kwa Tanzania ni zaidi ya milioni moja na nusu ama zaidi kutegemeana na ukubwa wa memori
Kumbuka iPhone 14 Plus ni toleo jipya lililotoka miezi ya mwishoni mwaka 2022
Ukiitazama vitu vipya ambavyo vimewekwa kwenye simu utaelewa sababu ya kuwa na bei kubwa
Kwenye makala hii kuna ufafanuzi wa sifa za iphone 14 plus zinazoipa simu ubora unaochangia bei yake kuwa ghari
Bei ya iPhone 14 Plus ya GB 256
Bei ya hii simu kwa hapa Taznania inafika shilingi 2,800,000/=
Bei ya GB 128 ni nafuu japo si kwa utofauti mkubwa.
Kuna vitu vingi vinavyoifanya simu kuuzwa hiyo bei kama utakavyoona baadae
Lakini kitu kikubwa ni uwezo mkubwa wa kiutendaji wa processor unaochangia simu hii kuzipita simu nyingi za Android
Ubora wa processor unaisaidia hii simu kukaa na betri masaa mengi kuliko hata iphone 12 pro max
Sifa za Simu ya iPhone 14 Plus
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED, |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB, 512GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,800,000/= |
Upi ubora wa iPhone 14 Plus
Kikawaida simu zinazouzwa kwa bei kubwa huzingatia ubora kwenye nyanja karibu zote
Kitu ambacho kipo kwa simu za apple
Kwa mfano, iphone 14 plus inakubali masafa ya mitandao karibu yote duniani
Kwa maana unaweza ukasafiri na simu sehemu yoyote duniani na ikafanya kazi
Kuna baadhi ya simu kama umeagiziwa kutoka Marekani ikija Tanzania inashindwa kushika network
Lakini kwa iphone karibu zote hazipo hivyo
Pia hii ni simu ambayo imewekewa ulinzi wa kutopitisha maji endapo ikidumbikia kwenye maji
Hii inakupa uhuru wa kuitumia simu hata kwenye mvua ikiwa inanyesha
Uwezo wa Network
Simu ya iphone 14 plus ni simu ya 5G inayokubali pia 3G na 4G
Ina uwezo wa kupakua faili kwa sekunde chache kwani ina 5G inayokubali masafa ya mmWave
mmWave ni aina ya masafa ya 5G yanayosafirisha data kuanzia masafa ya 24GHz na kuendelea
mmWave inatoa spidi inayofikia 2Gbps ambayo ni sawa na 255MBps kwa maana file ukubwa wa MB 255 simu inadownload kwa sekunde moja tu
Taasisi ya Signal Research Group ya Marekani iliripoti kasi inayofikia 2Gbps kwenye mji wa Tokyo Japan
Aina hii ya 5G ni tofauti na ya Vodacom Tanzania kwani yenyewe ni ya masafa ya kati
Kiujumla hupaswi kuwaza kuhusu network ya simu hii kama mtandao upo vizuri
Ubora wa kioo cha iPhone 14 Plus
iPhone 14 Plus inatumia kioo cha OLED kinachoitwa Super Retina XDR OLED
Super Retina XDR OLED kimeundwa na apple wenyewe kwa kushirikiana na samsung
Lengo kubwa ni kupunguza mapungufu ambayo yanatokea mara kwa mara kwenye vioo vya OLED kama vile burn-in
Apple wanadai vioo vya XDR OLED vinatoa taswira nzuri ya muonekano kutokana na kuwa na resolution kubwa, usahihi wa rangi, uwezo wa kuonyesha rangi nyeusi halisi na rangi nyeupe halisi na kuwa na uwezo kuonyesha rangi nyingi
Kivyovyote vile, vioo vya OLED huwa vina ubora mkubwa ukilinganisha na vioo vya IPS LCD
Ukizingatia iPhone 14 plus kioo chake kina HDR10, Dolby vision na Uangavu unaofikia kiwango cha nits 800
Nits zikiwa nyingi zinasaidia simu kuonyesha vizuri kabisa ikiwa inatumika juani kwenye mwanga mkali
Mwanga mwingi wa jua huwa unasababisha baadhi ya simu kutoonyesha vitu vizuri mpaka uweke mkono kwa juu
Nguvu ya processor Apple A15 Bionic
Kwenye upande wa simu janja apple huzipita kampuni nyingi linapokuja swala la kuwa processor za simu zenye nguvu
Processor ikiwa na nguvu inakuwa na utedaji wa haraka na ufanisi wa matumizi madogo ya betri
Simu ya iphone 14 plus inatumia chip apple A15 Bionic
Ni chip ambayo inatumika kwenye iPhone 13 Pro Max kitu kinachofanya hii simu kuzidiwa na iPhone 14 Pro kwa mbali.
Hii chip ina idadi ya core 6 na inatumia GPU aina ya Apple GPU (5 cores)
Moja ya kazi kubwa ya GPU ni katika kucheza magemu, gpu yenye nguvu hufanya gemu kuchezeka kwa muonekano mzuri bila kukwama wala kuganda
Bila gpu hutoweza kucheza gemu kwenye simu.
Apple A15 Bionic ina core (sehemu ya processor) mbili kwa ajili ya kufanya kazi kubwa ama kazi nyingi kwa wakati mmoja
Kwenye app ya nguvu za processor za simu, A15 Bionic ina alama 1700 kwenye geekbench na 795947 kwenye antutu
Hii inamaanisha uwezo wa iPhone 14 Plus ni mkubwa kuliko Samsung Galaxy S22+
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri wa iPhone 14 Plus ni 4323mAh
Unaweza ukadhani simu hii haikai na chaji kwa kuwa betri yake halijafika 5000mAh
Mambo yapo tofauti, kwani ni simu inayokaa na chaji muda mrefu sana kuliko hata zenye 5000mAh
Kwenye majaribio ya GSMArena, iPhone 14 Plus imeweza kukaa na chaji kwa masaa 16 simu ikiwa inaperuzi intaneti muda wote
Na imestahamili ukaaji wa chaji wa masaa 11 ilipokuwa inaperuzi intaneti kwa mtandao wa 5G
5G inakula chaji kutokana na kasi kubwa ya kupokea na kutuma data
Kwa bahati mbaya simu haiji na chaji, utalazimika kununua chaji kama hauna chaji ya iPhone
Ukubwa na aina ya memori
Unaweza ukamiliki apple yenye ukubwa wa GB 128, 256 au GB 512
Ukubwa wa memori unasababisha bei kuongezeka kama ilivyo kawaida
Aina ya memori za simu zote za apple huwa ni NVMe
NVMe ni aina ya memori ambayo ina uwezo wa kusoma na kuhifdhi faili kwa kasi inayofika 5444MBps
Spidi hii inaiwezesha simu kufungua app kwa haraka, kuzima ama kuwaka kwa sekunde chache na kukopi mafaili ndani ya muda mfupi
Memori yenye kasi inaboresha utendaji wa simu, iphone zote za 2022 zinatumia RAM ya 6GB
Uimara wa bodi ya iPhone 14 Plus
Bodi ya iPhone 14 Plus imeundwa kwa alminiamu upande wa pembeni
Na glass za gorilla nyuma na mbele
Bodi yake imetengenezwa iweze kuzuia maji kupenya hata ikiwa imezama kwenye kina cha maji cha mita 6 kwa muda wa nusu saa
Ni tofauti na baadhi ya simu zingine ambazo huhimili kwenye kina cha mita 1.5
Vioo vya gorilla na vyenyewe ni himilivu simu ikianguka urefu mkubwa (kimakadirio mita 2)
Simu hii inasapoti laini mbili au moja inategemea na soko lengwa
iPhone 14 Plus zinazouzwa Marekani hazina sehemu ya kuwekea laini bali hutumia eSIM (embeded SIM)
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera mbili upande wa nyuma na kamera moja upande wa mbele (selfie camera)
Kamera zake zinatoa picha na video kwa usahihi mkubwa rangi na muonekano halisi
Inatumia ulengaji aina ya dual pixel pdaf ambao hufanya kamera ya simu ifokasi kwa haraka inapopiga kitu kinachotembea mfano ukiwa unapiga ndege anayepaa angani
Uwezo mwingine ni kurekodi video za 4K kwa idadi ya fremu mpaka 60fps na video za full hd mpaka 240fps
Video yenye fps kubwa inakuwa ni “smooth” kwa maana video iliyorekodiwa inakuwa inaonyesha kila hatua
Kwenye mwanga hafifu simu inajitahidi kwa kiasi kuonyesha vitu bila kuathiriwa na mwanga mdogo hasa nyakati za usiku
Japokuwa mapungufu yapo ambayo ni ngumu kwa mtumiaji wa kawaida kutambua hizo “noises”
Ubora wa Software (iOS 16)
Kila toleo jipya la iphone huambatana na mfumo mpya endeshi
Ambapo matoleo ya 2022 yana iOS 16.
Kufahamu vitu vipya vya iOS 16 unaweza pitia, makala ya simu ya iphone 14 pro max
Yapi Madhaifu ya iPhone 14 Plus
Simu haina sehemu ya kuweka memori kadi
Inatoa changamoto ya kutanua memori simu inapojaa hasa toleo la GB 128
Kwa mwingine GB 128 ni nyingi ila ukiwa unarekodi sana video za 4K memori itajaa tu
Neno la Mwisho
iPhone 14 Plus haina tofauti kubwa na iPhone 13 Pro Max
Ikizingatiwa zote zinatumia chip ya aina moja
Bei ya iPhone 14 Plus inaweza kukupa iPhone 13 Pro Max ambayo inakuja na kamera tatu
Kwani kuna aina moja ya kamera haipo kwenye hii simu