GPS ni mfumo wa utambuzi wa maeneo duniani unaotumia satelaiti ambao unamilikiwa na nchi ya Marekani
Mara ya kwanza wakati unaanzishwa ulilenga matumizi ya kijeshi
Ila hali ilianza kubadilika mnamo mwaka 1983 baada ya USSR kulipua ndege ya Korea kusini iliyokuwa inatokea Marekani
Ndege ya Korea Kusini ilingia kwenye anga ya USSR iliyokatazwa bila kutambua
Mpaka mwaka 2000 GPS ilianza kutumika kwa matumizi ya kiraia
Mifumo mingine ya utambuzi wa maneneo ni GLONASS ya Urusi, Galileo ya Ulaya, Baedou ya China
Baada ya kujua GPS ni nini basi ni vizuri ukajua jinsi inavyofanya kazi
Mgawanyo wa GPS katika utambuzi wa Eneo
Ili mfumo wa Global Positioning System utambue eneo kuna vitu vinahitajika kufanya kazi kwa pamoja
- Setilaiti
- Receiver (simu)
- Control Center (kituo cha udhibiti)
Satelati ni kitu chochote kinachoizunguka dunia
Katikamfumo wa GPS kuna idadi ya satelaiti zinazofika 30
Japokuwa kikawaida huwa kunahitajika satelaiti walau nne ili eneo litambulike
Lakini kadri satelaiti nyingi zinavyopatikana ndio usahihi mkubwa wa utambuzi wa eneo unakuwepo
Setilaiti huwa inatuma signal (mawimbi) kwenda kwenye simu
Ndani ya simu kunakuwa na kifaa kinachopokea hayo mawimbi
Kifaa hiko hutambulika kama GPS receiver
Ufuatiliaji wa karibu wa mwenendo wa ufanyaji kazi wa setilaiti unahitajika
Hiyo kazi inafanywa na kituo cha udhabiti (control center)
GPS ina vituo vya aina hiyo vinavyofika 17
Kwa afrika kituo kinapatikana afrika ya kusini pekee kwenye mji wa pretoria
Jinsi GPS inavyofanya kazi kwenye simu
Kila simu janja huwa ina receiver kwa ajili ya utambuzi wa eneo
Receiver ina kazi ya kupokea data kutoka kwenye setilaiti kisha inafanya mahesabu ya kujua latitudo na longitudo ya eneo uliopo
Ili GPS ya simu ionyeshe eneo sahihi inahitaji kupokea data kutoka kwa setilaiti zaidi ya nne
Kisha GPS receiver inakokotoa umbali kati ya setilaiti na simu kwa kila setilaiti inayopatikana
Tofauti ya umbali zitaonyesha taarifa ya eneo ilipo gps receiver ya simu husika
Hivyo eneo ulilopo taarifa zake zinakuwa wazi
Tuchukulie mfano ufuatao.
Kuna mtu A anaishi mwanza na kuna mtu B anaishi dar es salaam
Halafu, tunataka kujua mtu A anaishi wapi
Ukitaka kujua nitamuuliza mtu B umbali kati ya Dar na anapoishi mtu A
Lakini taarifa ya mtu B pekee haitoshi kujua eneo ambalo mtu A anapatikana
Hivyo inahitajika mtu C anayeishi kigoma, mtu D anaeishi Arusha na mtu E anayeishi Mbeya kwa mfano.
Kisha ataulizwa mtu C, D na E umbali kutoka maeneo wanayoishi hadi kwa mtu A
Urefu wa maeneo yote hayao utakuwa unakutana kwenye eneo moja
Kwa staili hiyo mtu A anayeishi atatumbulika eneo lake analoishi ambalo litakuwa ni Mwanza
Kwa sababu upande unaopatikana mwanza utakuwa umejulikana
Hivyo ndivyo GPS receiver ya smartphone inavyoweza kujua eneo ulilopo kwa kupima umbali wa kati ya simu yako na setilaiti zaidi ya nne
Uonyeshaji wa eneo hutumia njia ya ukokotoaji inayofahamika kama trilateration na Multilateration
Hatutoingia kiundani kufafanua trilateration na Multilateration ila pitia wikipedia, Global Positioning System
Jinsi ya kuwasha GPS kwenye Smartphone
Ni rahisi kuwasha gps kwenye simu
Upande wa juu wa screen unaoonyesha tarehe, network ya simu nk
Iguse hiyo sehemu kwa kushusha chini
Utaona machaguo mengi kama kuwasha data, bluetooth, wi-fi, tochi na vitu vingine
GPS hutambulika kama Location
Ukigusa tu basi gps receiver ya simu itaanza kusoma eneo ulilopo
Na unaweza ukaona eneo ulilopo kwa kufungua ramani ya Google
Itakuonyesha ulipo kwa wakati huo
Usahihi wa GPS kuonyesha Eneo
Mfumo unatoa kwa usahihi mkubwa taarifa za eneo ambalo simu ipo
Ila si kwa usahihi wa asilimia mia
GPS huwa ipo nyuma kwa umbali wa mita tano toka eneo ambalo kifaa cha gps kilipo
Tatizo linakuwepo hasa pale simu inakuwa inapata data kutoka kwenye setilaiti chache
Tatizo hili linalekebeshwa kwa kuiwezesha simu janja kusapoti mifumo kama ya GPS ya nchi zingine
Ndio maana simu nyingi za daraja la kati na juu huwa zina mifumo zaidi ya mmoja ya utambuzi wa maeneo
Utakuta simu moja inakubali Galileo ya umoja wa ulaya, Glonass ya urusi na Beidou ya china
Kama utakuwa na matumizi mengi ya GPS inafaa ukawa na simu inayokubali mifumo mingi
Matumizi ya GPS na Faida Zake
Taarifa za GPS zinaweza kukusaidia kwenye mengi mno
Ukiwa umeiwasha itakusaidia kujua spidi ya chombo chochote cha usafiri unachosafiria ikiwemo baiskeli
Hilo linafanikiswa kwa kutumia aplikesheni
Kuna app nyingi zinazoweza kuonyesha spidi na umbali kutumia gps
Moja ya app iyo inaitwa GPS speedometer
Pia, inaimarisha ulinzi hasa pale simu inapopotea
Kama gps ikiwa imewashwa utaweza kufuatilia eneo ambalo simu ipo
GPS pia hutumika kupima viwanja
Je Ni Salama kuwasha GPS muda wote?
Kiujumla ni salama kama wewe si muharifu
Ubaya wa kuwasha gps mara kwa mara unakuja kwa makampuni makubwa ya teknolojia kama Google, Facebook, Apple nk
Yana tabia ya kuchota taarifa zako pasipo kujua japokuwa wengi hurusu hizo app kuchota data
Haya makampuni hutumia hizo taarifa kwenye biashara zao za matangazo
Mtu akiweka tangazo anaweza kuchagua eneo ambalo tangazo linapaswa lionekane
Kiujumla, ni vizruri GPS ikawa ON muda wote
Inakupa urahisi kuifutalia simu inapopotea
Hitimisho
Ukiwa ni mtu wa kuzingatia faragha itakulazimu kuzima GPS muda mwingi
Ikizingatiwa tayari unafahamu maana ya GPS ni nini na umuhimu wake
Maana kila kilicho na maana hakikosi mapungufu
Lakini jua kuwa huu mfumo unaweza kurekebisha saa ya simu kwa usahihi mkubwa
Kwa sababu gps inasifirisha data zinawakilisha nyakati
Muda unaoletwa na setilaiti ni sahihi zaidi kuliko uliopo kwenye simu
Kwa sababu satelaiti zake zinatumia Atomic Clock kusoma muda
Maoni 19 kuhusu “GPS ni Nini? Maana na Kazi ya GPS”
Sawa samahani je hii nikizima inaweza saidia mtu yoyote asijue nilipo maana kuna mda mtu anakufatilia ili ajue tu mahali unapoenda
Ndiyo inawezekana
Sasa kama GPS iko OFF ila simu iko ON je inaweza kutambua mahali nilipo?
Haiwezekani Kwa kutumia GPS kama IPO off
U na ifatiliaje sm yako kwa tumia gps
Soma haya maelezo utafahamu hatua za kufuata, https://simunzuri.com/jinsi-ya-kutumia-gps-kwenye-simu/
Mfano nimepoteza simu na gps location ikiwa onn,naweza kuipataje nkiitafta kutumia simu nyingine
Ndio unaweza kutumia GPS kuitafuta simu
Je, nawezaje kuitafuta simu yangu ikiwa off location
Kama GPS IPO off, njia nyingine ni kutumia IMEI namba na hapo ndipo unapolazimika kushirikisha polisi
Kuna njia nyingine ya kutafuta simu ikiwa imezimwa location..?
Nataka kujua au kutafuta simu yangu ilio potea au kuibiwa kwa kutumia gps ya simu nyingine nifanye je?
Jinsi ya kutafuta simu iliopotea
Mfano simu A yenye gps iimepo lakini hapa nina simu B nawasha gps nitatafutaje ?
Inakubidi uingie kwenye email uliyotumia kwenye simu iliyopotea. Halafu ingia Google kisha andika findmy device. Halafu unabinyeza link ya Kwanza iliyoandikwa find my device. Utaweka email yako. Kama GPS IPO on. Utaona simu yako eneo ilipo
https://www.google.com/android/find/
simu yangu inaeza potea akini aliyeokota ama kuiba akazima gps location ili simu isitambulike mahali ilipo, je kuna mbinu au settings za gps kutozimwa na mtu mwengine isipokuwa mtumiaji?
Hakuna, njia nzuri ni kuificha icon ya location
Natakabichapishwa
je ukiwa upata Kwa mfano Mimi nimepoteza SIMU yangu nikiwa manyara lakini aliyeokota SIMU ni mtu wa Arusha na nimepata location halafu nafika sehemu husika je utamjuaje mwenye nayo???
Kwenye app ya find my device kuna sehemu ya kubonyeza ambayo itaifanya sehemu iite Kwa sauti kubwa