Huu mwezi wa tatu 2025 tecno imetangaza ujio wa matoleo mapya ya Tecno Camon 40
Simu hizo ni
- Tecno Camon 40
- Tecno Camon 40 Pro 5G
- Tecno Camon Pro
- Tecno Camon 40 Premier
Kwenye hii post utafahamu baadhi ya sifa za muhimu za kila tecno
Na tecno kali zaidi kati ya zilizotangazwa
Tuzame kiundani na kwa kifupi sana.
Tecno Camon 40
Tecno Camon 40 inakuja na mfumo endeshi wa Android 15
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Mediatek Helio G100 Ultimate
Inakuja na memori ya GB 128 na GB 256 na RAM ya GB 8 ama 12
Betri yake kubwa ina mAh 5200
Pia ina kamera mbili kubwa ikiwa na megapixel 50
Tecno Camon 40 Pro 5G
Kioo cha Tecno Camon 40 Pro 5G kina refresh rate ya 144hz ambazo huwa ni smooth
Hii ni tecno iliyowekwa waterproof aina ya IP68 ambayo inaashilia maji hayatoingia kwenye simu ikizama kwenye kina ch mita 2
Upande wa kamera, zipo kamera mbili moja ya 8MP na nyingine ya 50MP
Ukubwa wa memori ni GB 256 ila RAM unaweza pata ya GB 8 na GB 12
Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri ukubwa wake ni 5200mAh
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu ya utumiaji wa chip ya Dimensity 7300
Tecno Camon 40 Pro
Tecno Camon 40 Pro ni simu ya daraja la kati
Utendaji wake ni wa wastani kwani processor yake ni Helio G100 Ultimate
Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz
Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri yake ina 5200mAh
Ukubwa wa memori ni wa aina moja ambayo ni GB 256 NA RAM ya GB 8
Ina kamera mbili pekee ambapo kamera kubwa imewezeshwa OIS
OIS hufanya kamera kutulia wakati ukiwa unarekodi video huku unatembea
Tecno Camon 40 Premier
Tecno Camon 40 Premier ndio tecno bora zaidi kati ya zilizotangazwa
Ina kamera tatu na zote ukubwa wake ni 50MP
Kamera ya Periscope Telephoto inasapoti ya optical zoom inayoweza ku-zoom mara tatu
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 70 na betri lake lina ukubwa wa 5100mAh
Kioo chake ni cha LTPO AMOLED chenye refresh rate ya 144Hz
Na yenyewe ina waterproof ya IP68