Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30
Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range
Ubora wa kiujumla uliopo kwenye simu zote tatu ni kasi kubwa ya kuchaji, mfumo endeshi wa HIOS 14 uliowezesha AI(akili mnemba)
Tutaangalia baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hios 14
Na kingine ni kwamba simu zote zinakuja na memori kubwa za kuanzia GB 256
Tuzame kiundani.
Bei za Tecno Camon 30
SIMU | BEI(Tanzania) |
---|---|
Tecno Camon 30 | 690,000/= |
Tecno Camon 30 Pro | 990,000/= |
Tecno Camon 30 Premier | 1,250,000/= |
Ubora wa software
Simu zote yaani Tecno Camon 30, Tecno Camon 30 Pro na Tecno Camon 30 Premier zinatumia mfumo endeshi wa Android 14
Na pia inaambatana na mfumo wa Tecno wa HIOS 14
HIOS 14 inakuja na vitu vingi vya artificial intelligence yaani akili bandia
Cha kwanza kuna kinaitwa AI Eraser
Fikiria upo mtaani unapiga picha, kwenye mtaa kuna watu wanapita kwa nyuma
Ukaja kugundua wapita njia wametokea kwenye picha yako na wewe hutaki
AI Eraser ina uwezo wa kuwaondoa hao watu bila kuharibu uhalisia wa muonekano wa picha
Kitu kingine ni kutengeneza wallpaper unayotaka wewe
Unaitengeneza kwa kuifafanulia simu kwa maandishi yanayoelezea muonekano wa wallpaper
Ukishaandika, sehemu itaanza kutengeneza wallpaper kulingana na maelezo uliyotoa
Nguvu ya Processor
Tecno Camon 30 inatumia chip ya Mediatek Helio G99
Wakati huo Tecno Camon 30 Pro na Premier zinatumia chip Mediatek dimensity 8200
Tuangalie uwezo wa kiutendaji wa kila chip
Mediatek helio G99
Utendaji wa mediatek g99 ni wa wastani ila inaweza kufanya vitu vingi
Kwenye core yenye nguvu kubwa helio g99 inatumia muundo wa Cortex A76
Kuna baadhi ya gemu inacheza kwa fps kubwa na kwenye graphics za hd
Zingine ili ucheze vizuri inakulazimu kupunguza ubora wa graphics ili ucheze kwa ultra hd
Kiuhalisia inazidiwa karibu mara mbili na chip ya mediatek dimensity 8200 ambayo ipo kwenye camon 30 pro na premier
Tuangalie sasa 8200 utendaji wake
Mediatek dimensity 8200
Mediatek dimensity 8200 ina ubora mkubwa zaidi ndio maana hata bei za Camon premier na pro ni kubwa
Muundo wake wenye nguvu kubwa unatumia Cortex A78,
Utendaji wa cortex a78 unaweza kusukuma vitu vingi sana vinavyohitaji nguvu kubwa bila kukwama
Ndio maana dimensity 8200 ina alama
Gemu nyingi zinacheza kwa kiwango cha fhd na kwa fremu nyingi
Kwa mantiki hiyo Camon 30 Pro na Camon 30 Premier zitakupa ufanisi stahiki zaidi
Betri na chaji
Simu zote zina betri zenye ukubwa wa 5000mAh na chaji ya wati 70
Kama una haraka ya kwenda sehemu na simu yako haina chaji
Unahitaji dakika 45 kuijaza betri lote kutoka 0 hadi 100
Camon zote zinajitahidi kutunza chaji hata katika matumizi ya intaneti
Kiwastani, na kwa majaribio mbalimbali ukiwa kwenye intaneti simu inakaa karibu masaa 11 kwa kuperuzi
Ila kama ni mchezaji wa gemu utadumu na chaji kwa masaa saba
Ubora wa kioo
Simu zote zinatumia kioo cha Amoled ila kioo cha tecno camon 30 premier ni kizuri zaidi
Tecno Camon 30 na camon 30 premier zinakuja na skrini ya refresh rate inayofika 120Hz
Ila Camon 30 Pro inafika hadi 144Hz
Premier ina ubora wa ziada kwa sababu kioo chake ni cha LTPO AMOLED kikiwa na HDR
Kioo cha namna hii kinadhibiti kiwango cha refresh rate chenyewe na kinaonyesha vitu kwa mkolezo sahihi
Ila Tecno walipaswa waweke angalau HDR10+
Kamera
Tecno Camon 30 Premier inakupa mfumo mzuri wa kamera kuliko camon 30 zingine
Kwa mfano Camon 30 ina kamera mbili moja ina 50MP na OIS huku ya pili ikiwa na 2MP ambayo depth sensor
Depth sensor huwa ni kamera inayopima eneo na kina cha kitu kinachopigwa picha
Hivyo haipigi picha na haina umuhimu kwa sababu teknolojia za PDAF zinafanya hiyo kazi
Camon 30 Premier ina lenzi za ultrawide na wide
Wakati premier ina kamera muhimu za tekephoto, ultrawide na wide
Na Pro na Premier zinarekodi video za 4K
Wazo moja kuhusu “Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)”
Kwa hiyo spea zake zinapatikanaje na bei elekezi ya tecno cammon 30 premium kwa sasa inakuwa shilingi ngapi