Simu ya Tecno Spark 8P ni simu ambayo imezinduliwa mwaka 2021
Baadhi ya sifa za Tecno Spark 8P zinaifanya Spark 8P kuwa simu nzuri ya bei nafuu kwa mwaka 2022
Kwa nini?
Sifa za betri zinafanya simu kukaa na chaji muda mrefu.
Memori kubwa ya Spark 8P inaweza kuhifadhi mafaili mengi
Hii ni moja ya simu ya android inayouzwa chini ya laki tatu.
Tazama jedwari kufahamu sifa zote na bei ya Tecno spark 8P
Sifa za Tecno Spark 8P
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC, 64GB,128GB,256GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 256,765.88/= |
Upi ni ubora wa Simu ya Tecno Spark 8P
Ubora wa tecno spark 8p upo katika sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza ni memori
Memori yake ina ujazo wa kuhifadhi mamia ya apps
Na sehemu ya pili ni betri.
Tecno Spark 8P ina betri kubwa.
Uwezo wake wa processor unatumia umeme kidogo
Hii sio simu ndogo kiupana na kierufi
Mkanganyiko upo kwenye sifa zingine kama utakavyoona baada kusoma mada yote
Network ya Tecno Spark 8P
Simu ya Tecno Spark 8P inakubali mitandao yote kama ilivyo Tecno Spark 7P
Simu inakubali ainakubali 3G na 4G.
4G yake ipo kundi la nne yaani LTE Cat 7
Tofauti na simu ya Vivo T1 5g
Spidi ya juu ya kudownload inafikia 300Mbps sawa na 35MBps
Iwapo mtandao wa simu inakupa spidi ya 35Mbps,
Basi simu inadownload file la 1300MB kwa sekunde 37
Hakuna mtandao wa simu unatoa kasi ya aina hii Tanzania
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 8P
Aina ya kioo kinachotumia na Tecno spark 8p ni IPS LCD
Kioo cha tecno spark 8p kina resolution 1080 x 2408 pixels
Ukubwa huu wa resolution unaonyesha vitu vizuri kwenye screen
Miaka ya nyuma IPS LCD vilikuwa vinaongoza kwa ubora.
Ila vina shida ya kuwa na contrast ndogo ukilinganisha na Amoled.
Hivyo huwa vina rangi chache
Kitu kibachosababisha baadhi ya vitu kutoonesha rangi halisi.
Nguvu ya processor MediaTek Helio G70
Processor ya simu inayoutmiwa na hii Tecno ni MediaTek Helio G70.
Ni chip yenye core nane (Octa-core
MediaTek Helio G70 ina nguvu ya wastani.
Ndio maana gemu la Call of Duty: Mobile linacheza kwenye resolution ndogo.
Na kwa spidi ndogo.
Hata hivyo MediaTek Helio G70 inaweza kufungua apps nyingi kwa urahisi
Uwezo wa core kubwa
Kuna core nne zenye nguvu kubwa
Kila core ina spidi ya 2.0GHz
Na core zote zinatumia muundo Cortex A75
Kipindi Cortex A75 imetoka 2017 ilitumika kwenye simu za daraja la kati
Kiutendaji, inaizidi Cortex A73 kwa 16% mpaka 46%
Cortex A73 ni Kryo 260 gold upande wa snapdragon
Kryo 260 imetumika kwenye chip ya Snapdragon 662
Snapdragon 662 inaipa nguvu simu ya Nokia 5.4
Hivyo Tecno Spark 8P inaizidi simu ya Nokia 5.4 kiutendaji
Uwezo wa core Ndogo
Core zenye nguvu ndogo zipo nne.
Kila core ina spidi ya 1.7GHz
Na core zote zimeundwa kwa Cortex A55
Cortex A55 ina utendaji unatumia umeme mdogo.
Cortex A55 inasaidia kuhifadhi betri pale simu inapofanya kazi ndogo ndogo.
Hii ni core maalumu inayofanya shughuli zisizohitaji nguvu kubwa
Cortex A55 ni bora kuliko Kryo Silva ya Snapdragon.
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya tecno spark 8p ni 5000mAh(Li-Po).
Simu nyingi ziazotumia betri la sazi kubwa kama hii hukaa na chaji muda mrefu
Kwa kuzingatia nguvu ndogo ya processor,
Tecno hii inaweza kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 14 simu ikiwa kwenye intaneti.
Tecno hawajainisha spidi ya chaji
Hii inaonesha simu haina fast chaji
Ukubwa na aina ya memori
Memori za spark 8P ni aina ya eMMC.
Spidi yake ya kuandika na kusoma mafaili ni ya wastani ukilingansiha na UFS
Kuna Tecno spark 8p za aina tatu kwenye memori
- 64GB, 4GB RAM
- 128GB, 4GB RAM
- 256GB, 4GBRAM
Kiujumla memori zake ni kubwa
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 8P
Fremu na upande wa nyuma wa hii tecno una plastiki.
Na ina kioo sio cha gorilla kwenye screen.
Lieke akilini hili.
Plastiki huwa na kawaida ya kuchunika rangi kadri simu inavyotumika mara kwa mara
Kwa ulinzi wa muda mrefu kava inahitajika
Simu ni nyepesi kuebeba na nyembamba kiasi
Kwana ina unene wa milimita 8.85
Ubora wa kamera
Kamera za tecno spark 8p ziko tatu.
Kamera kuu ina resolution kubwa ya 50MP inayopiga eneo pana kiasi
Kamera ya pili ni aina ya depth yenye 2MP
Moja ya depth camera ni kufanya mahesabu ya umbali kati ya kamera na kinachpigwa picha.
Inasaidia kamera kukilenga hiko kitu kwa usahihi
Kamera ya tatu ni kamera VGA
VGA ni kamera za kizamani zenye pixel chache
Picha na video za VGA sio nzuri kwani hutoa resolution ndogo ya 640×480 pixels
Ubora wa video
Tecno spark 8p inaweza kurekodi video za aina moja tu.
Simu inarekodi vidoe za full hd(1080p) kwa spidi ya 30fps
Hakuna video za 4k wala 8k
Ubora wa Software
Tecno spark 8p ni simu ya android 11 yenye HiOS 7.6
Tazama vitu vilivyopo kwenye HiOs kwenye huu ukurasa wa tecno
Bei ya Tecno Spark 8P Tanzania
Bei ya tecno spark 8p inafika shilingi 260,000/=
Japokuwa kwa Tanzania Tecno Spark 7P zinapatikana kwa urahisi kuliko tecno spark 8p
Ila natumai ukizunguka maduka ya kariakoo mitaa ya uhuru unaweza ukaipata hii zimu
Tazama: simu zingine za bei nafuu
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 8P
Kiuhalisia simu ina mapungufu mengi.
Utayajua baadhi.
Kamera zake hazina teknolojia nzuri ya autofocus aina dual pixel pdaf
Hakuna kamera iliyowekea OIS kutuliza mitikisiko ya video inayorekodiwa wakati wa kutembea
Processor ya spark 8p haina nguvu kubwa kama ya kwenye Redmi note 11 pro+ 5g
Simu haitumii vioo vizuri aina ya amoled na gorilla glass
Pia simu imeundwa kwa plastiki na haina viwango vya IP rating
IP rating huonesha uwezo wa simu kuzuia maji.
Neno la Mwisho
Kitu kimoja cha kuweka akilini kuna matoleo mawili ya simu ya Tecno spark 8p
Kuna Tecno spark 8p yenye nguvu ndogo inayotumia procrssor ya Helio P22
Unapaswa kuwa makini unapotaka kununua hii simu