Moja ya sifa ya kampuni ya samsung ni kutengeneza simu zinazolenga kila aina ya watumiaji.
Hutengeneza simu zenye ubora ambazo huwalenga watumiaji wenye matumizi makubwa na wanaopenda smartphone nzuri za gharama.
Matoleo ya S-Series mfano Samsung S20 ni ya gharama.
Pia samsung huunda simu zenye ubora wa kati na zingine ubora wa kawaida.
Matoleo ya A-Series na M-Series yamegawanyika makundi ya simu zenye ubora wa kati na wa chini.
Simu nzuri za samsung hutumia vioo angavu vya Amoled na Processor zenye utendaji mkubwa wa kufungua app yoyote.
Matoleo ya A-Series na M-Series yanalenga kushindana na brand za kichina hasa simu za xiaomi na simu za oppo
Orodha ya simu iliyopo inahusisha samung matoleo ya S-Series, M-Series,Note-Series na A-Series.
Kama umeshawahi kujiuliza kwa nini baadhi ya simu huuzwa milioni mbili basi hilo jibu utalipata kwa kufahamu kila sifa ya samsung iliyopo hap chini.
Bonyeza simu unayotaka kuijua kuifahamu sifa zake kati ya zilizopo kwenye orodho chini.
Orodha haipo kwenye mtiririko ila katika hii orodha kuna simu ambayo ni bora kwenye kila idara.
Pitia sifa ya kila simu
SAMSUNG GALAXY S21 FE 5G
Samsung galaxy s21 fe 5g ni simu bora kuanzia upande wa network(5g), kamera, memori, kioo(display), processor(SoC ama chip pia hufahamika kama chipset), uimara na hata ukaaji wa chaji.
Galaxy s21 fe 5g zipo matoleo mawili.
Toleo lilitengenezwa kwa ajili ya kuuzwa Marekani na Toleo kwa ajili ya soko la kimataifa nje ya Marekani.
Toleo la Marekani inatumia SoC(processor) ya Snapdragon 888 5G, simu bora za android zimeutumia hii soc sana.
Toleo la kimataifa inatumia chip ya Exynos 2100.
Chip zote mbili yaani Exynos 2100 na Snapdragon 888 5G zina nguvu kubwa ya kiutendaji.
Muundo wa Kryo 680 na Cortex X1 unaziwezesha processor kufanya kazi kubwa kwa kutumia nishati ndogo ya betri.
Hivyo simu hukaa na betri muda mrefu tofauti na matoleo ya zamani ya samsung.
Japokuwa zamani Simu nzuri za samsung galaxy zililkuwa na changamoto ya ukaaji chaji.
Hali imebadilika kwa sasa
Simu hii ni simu yenye kamera nzuri tatu.
Kamera mbili zina OIS na teknolojia ya dual pixel.
OIS husaidia video kutulia wakati ukipiga huku unatembea.
Dual pixel hufanya kamera kulenga kwa sahihi kitu kinachopigwa picha na hivyo picha kutokea vizuri ikipigwa kwenye mwanga hafifu hasa nyakati za usiku.
Endapo samsung galaxy s1 fe 5g ikiingia kwenye maji ya kina cha mita 1.5, maji hayapenyi ndani ya simu kwa muda wa nusu saa.
Hii inatokana na kuwa na IP68.
Simu ina kioo chenye screen protector ya Gorilla Glass Victus ambacho hufanya kioo kuwa kigumu kuvunjika na kuchunika.
Kioo(display) chake huonyesh picha kwa uang’avu na kwa uhalisia sababu ya kuwa na resolution ya 1080×2400 na kioo cha amoled 2x.
Vioo vya amoled huonyesha picha kwa uhalisia bila kupoteza ubora sababu huwa vina rangi nyingi.
Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa umeme wa wati 25, pia ina uwezo wa kuchaji vifaa vingine kwa wati 15 sababu ina reverse charging.
Betri yake hukaa na chaji masaa 92.
Betri lake la 4500mAh hujaa asilimia 50 ndani ya dakika 30.
Ujazo wa memori ni 128GB na 256GB.
Pia baadhi zina RAM ya 6GB na 8GB.
Hivyo simu inakuwa uwezo wa kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja kwa haraka na bila kukwama kwama.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | , 128GB,256gb na RAM 8GB, 6GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,342,120/= |
SAMSUNG GALAXY S21 ULTRA 5G
Samsung galaxy s21 ultra 5g inafanana vitu vingi kitu kinachotofoautiana na simu iliyotangulia ni urefu na upana, kamera, ukubwa wa betri na resolution ya kioo.
Galaxy s21 ultra ina urefu na upana wa inchi 6.8. Ni simu ndefu.
Kioo chake ni amoled ila simu hii ina resolution kubwa 1440 x 3200 hivyo ubora wa picha na video ni mkubwa zaidi.
Betri yake ni kubwa pia lenye ujazo wa wati 5000mAh. Hii ina maana s21 ultra 5G inakaa na chaji zaidi kwa masaa 114 data ikiwa imezimwa.
Kamera zake zote zina dual pixel PDAF na OIS. Hivi ni vitu vinavyofanya kamera ya simu kutoa kamera nzuri nyakati zote.
Mengineyo mengi yako sawa na samsung galaxy fe 5g.
Sifa za samsung galaxy s21 ultra kwa uifupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 128GB, 256GB, 512GB na RAM 12GB, 16GB |
Kamera | Kamera NNE
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,844,258/= |
SAMSUNG GALAXY A52s 5G
Samsung galaxy a52s 5g ni simu nzuri ya samsung yenye ubora wa kati ambayo ina ubora kwenye idara nyingi.
Ni simu yenye 5G ambayo imejaribu kuweka vitu vingi ambavyo hupatikana kwenye simu za bei ghari.
Inatumia SoC ya Snapdragon 778G yenye modem ya 5G.
Ni processor yenye nguvu na uwezo wa kufungua app zinazohitaji nguvu kubwa(gemu) kwa wepesi .
Pia 4g yake ina spidi kubwa ya ku-download ya 1200Mbps yaani kasi ya 150MB/s.
Kwa mfano kama unatumia mtandao wenye kasi kubwa basi faili unalodownload litamalizika kwa haraka.
Kamera zake nne ni moja tu yenye OIS na zote hazina dual pixel.
Kamera kubwa ina megapixel 64 na sensa yake ni kubwa.
Pia simu ina ulinzi wa kuzuia maji kupenya endapo imeingia kwenye kina cha mita 1 kwa muda wa nusu saa.
IP67 pia huruhusu simu kutumika hata kwenye mvua.
Storage(memori) ina uwezo wa kuhifadhi vitu vingi.
Upande wa memori, Galaxy A52s zipo za matoleo matano amazo hutofautiana kwa memori na ram.
Kiujumla zipo za 128GB na 256GB.
Na mgawanyo wa RAM ni 6GB kwa 8GG.
Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi wa wati 25W.
Ndani ya dakika 90 simu inaweza kujaa.
Betri lake la ujazo wa 4500mAh linatunza chaji kwa muda mrefu.
Iwapo simu ikiwa haitumikii hukaa na chaji kwa masaa 113.
Na ukiwa unatumia intaneti mfululizo betri inaweza isha baada ya masaa 12.
Sifa za Samsung galaxy a52s 5g kwa ufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB,256GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera NNE
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 856,180/= |
SAMSUNG GALAXY A52
Samsung galaxy a52 ni simu yenye ubora wa kati ambayo haina 5G bali ina 4G.
Processor iliyotumika kwenye simu hii ni snapdragon 720G ambayo ina ubora wa kati.
Snapdragon 720G ina uwezo mkubwa kiutendaji kutokana na muundo uliotumika wa katika processor wa Kryo 465.
Muundo wa Kryo 465 husaidia simu kufanya kazi kubwa lakini pia hupunguza matumizi makubwa ya betri.
Hii inafanya Galaxy A52 kuwa simu inayotunza chaji kwa muda mrefu wa masaa 105 ikiwa kwenye matumizi ya kawaida yasiyohusisha data pamoja na kwamba betri yake ni ndogo la ujazo wa 4500mAh.
Mfumo wake wa chaji hupeleka moto mwningi wa wati 25 ambao hujaza betri kwa asilimia 50 ndani ya dakika 30.
Simu ya samsung galaxy a52 ina ulinzi wa maji ambao ni IP67.
Simu ikizama kwenye kina cha mita moja maji hayawezi penya kwa muda wa nusu saa.
Simu ina kamera nne, moja ina OIS na kamera kuu ina megapixel 64.
Kamera zingine zote hazina dual pixel wala OIS, pia inaweza kuchukua video bora za 4K.
Memori zake zina ukubwa wa 128GB na 256GB.
RAM zipo za 4GB, 6GB na 8GB.
Kwa mtumiaji sana wa simu A52 yenye RAM ya 8GB inafaa zaidi.
Sifa za Samsung galaxy a52 kwa ufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB, 256GB na RAM 8GB,6GB, 4GB |
Kamera | Kamera NNE
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 786,760/= |
SAMSUNG GALAXY A22 5G
Sifa kubwa nzuri ya samsung galaxy a22 5G ni kuwa na network 5G.
Hii inachagizwa na kutumia processor yanye uwezo mkubwa kiutendaji ya MediaTek Dimensity 700 5G ambayo ina modem ya 5G inayosapoti aina zote za mtandao wa 5G.
Galaxy A22 5g ni kati ya simu nzuri za samsung za bei nafuu zinazokubali mtandao wa 5G
Sifa zingine ni za kawaida lakini bado ni zimu nzuri ya samsung.
Kamera yake kubwa ina megapixel 48 lakini inakosa teknolojia za kuboresha picha na video za dual pixel na OIS.
Kioo chake si kizuri kwa sababu ni aina TFT.
TFT huwa na tatizo la kuonyesha rangi kwa usahihi na kufanya vitu kutoonekana vizuri ukilinganisha na vioo vya IPS LCD.
A22 5G zipo zenye memori ya 64GB, 128GB na RAM za 4GB, 6GB na 8GB.
Betri yake inapeleka umeme mdogo wa wati 15 hivyo betri lake lenye ujazo 5000mAh litachukua muda wa takribani masaa matatu kujaa.
Simu hainz IP67 wala IP68. Ikiingia kwenye maji basi maji yanaweza kupenya ndani ya simu.
Ni simu nzuri ya bajeti ya chini upande wa samsung
Sifa za samsung galaxy a22 5g kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | TFT, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | , 128GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 543,790/= |
SAMSUNG GALAXY A32 5G
Simu ya samsung galaxy a32 5g inafanana vitu na samsung a22.
Ila kuna ambavyo ubora umepungua na ambao umeongezeka.
Kwa mfano galaxy a32 ina glasi ya gorilla 5.
gorilla 5 ni kigumu kuvunjika kulinganisha na glasi zingine zinazowekwa kwenye screen.
Kioo chake ni cha TFT kilichopunguzwa ubora wa refresh rate.
Mengineyo mengi yako sawa na simu iliyotangulia.
Ila Samsung galaxy a32 inatumia Chipset ya MediaTek Dimensity 720 5G ambayo ina nguvu kuliko mtangulizi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | TFT |
Softawre |
|
Memori | , 64GB,128GB na RAM 8GB,4GB,6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 370,240/= |
SAMSUNG GALAXY NOTE20 ULTRA 5G
Samsung galaxy note20 ultra 5g ni simu yenye kamera inatoa megapixel nyingi kiasi cha megapixel 108.
Japokuwa picha kwenye bado huonekana vizruri kwa megapixel 12, picha ya megapixel 108 inafaa zaidi kwenye screen kubwa mfano televisheni za inchi 75.
Kamera zake mbili zina OIS na zinaweza kuchukua video za ubora wa 4k na pia zina HDR10+ ambazo husaidia picha zilizopigwa kwenye mwanga mdogo hasa usiku kuonekana vizuri.
Kioo(display) yake ni AMOLED 2X ambacho huonesha picha kwa uhalisia hasa rangi nyeusi.
Na screen ni ndefu na pana kwani ina inchi 6.9
Kama ilivyo kawaida ya simu ya bei ghari, ina uwezo wa kuzuia maji kuingia endapo simu imetumbukia kwenye maji au inatumika kwenye mvua. Sababu ina IP68.
Simu ina mfumo wa chaji unaopleka umeme wa kutosha wa wati 25.
Hivyo betri lake la 4500mAh linaweza jaa kwa ukamirifu ndani ya dakika 80.
Pia Note20 Ultra inaweza kuchaji vifaa vingine kwani ina mfumo wa reverse charging unaopeleka umeme wa 4.5W.
Simu ya Galaxy note20 ultra inatumia processor ya Snapdragon 865 kwa simu zinazouzwa Marekani.
Na processor ya Exynos 990 kwa simu zinazouzwa mataifa mengine nje ya USA.
Hizi processor zina nguvu ya kiutendaji hivyo zinatumia umeme mwingi.
Na hii inasababisha simu kukaa na chaji masaa 88 ikiwa haitumiki ama ikiwa kwenye matumizi ya kawaida.
Memori ni kubwa kwa kuhifadhi mafaili na apps nyingi.
Zipo note 20 ultra zenye 128GB, 256GB na 512GB.
Sifa za samsung galaxy note20 kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.0, 128GB,256GB,512GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.9inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,084,914/= |
SAMSUNG GALAXY M32
Samsung galaxy m32 ni simu yenye betri kubwa la 6000mAh kwa simu zinazouzwa India.
Sifa za M32 ina ufanano na simu za infinix kwa asilimia kubwa.
Kwa mataifa mengine betri lake ni 5000mAh, bado ni betri kubwa.
Betri yake inaweza kuwahi kujaa haraka kwa sababu galaxy m32 inapeleka umeme mwingi wa wati 25
Simu inatumia kioo cha super amoled ambacho husifika kuonyesha vitu kwa ubora kutokana na kuonyesha rangi nyingi.
Kioo pia kina glasi gorilla 5 ambacho huwa ni gumu hivyo huna haja ya kuwa na screen protector.
Simu ya samsung galaxy inatumia processor ya ubora wa kati ya MediaTek helio G80.
MediaTek helio G80 imeundwa kwa muundo wa Cortex A75 na Cortex A55.
Hivyo utendaji wa processor ni kawaida na hautumiii umeme mwingi na kufanya betri kukaa na chaji muda mrefu.
Simu ya samsung galaxy m32 zipo za 64GB na 128GB.
Mfumo wake wa memori hauna spidi kubwa kwani unatumia eMMc.
Hivyo ukikopi vitu kwenda kwenye simu vitachelewa kumalizika kukopi ukilinganisha na simu zinazotumia memori aina ya UFS.
Galaxy M32 haina 5G ila ina 4G yenye kasi kubwa ya kudownload.
Kamera zake nne zote hazina OIS na dual pixel PDAF.
Japo kamera kuu ina megapixel 64 ila binafsi wingi wa megapixel si ubora kamera.
Kamera yake haina uwezo wa kuchukua video za 4k.
Na pia simu haina IP68 wala IP67 hivyo inapitisha maji pindi ikiingia ndani ya maji.
Sifa za samsung galaxy m32.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMc 5.1, 64GB, 128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 668,746/= |
SAMSUNG GALAXY M52 5g
Samsung galaxy m52 5g ni simu pana na ndefu kwani urefu inchi 6.7
Simu ina glasi ya gorilla 5 na haina IP ya aina yoyote
Inatumia processor ya Snapdragon 778 hivyo simu inakubali mtandao wa 5G wa aina zote.
Kuanzia NSA, SA, Sub-6 na mmWave.
Snapdragon 778 ina ubora wa kati na uwezo kufungua application za kila aina bila kukwama kutokana na kutumia muundo wa Kryo 670
Pamoja na chip kuwa na nguvu kubwa lakini imeundwa kwa kuzingatia ulaji mdogo wa betri.
Hivyo betri lake la 5000mAh linatunza chaji muda mrefu wa masaa 123 simu ikiwa imezimwa data ama ikiwa haitumiki.
Na mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa kutosha wa 25W.
Umeme wa kasi hufanya betri kujaa kwa haraka lakini pia fast charge ina madhara yake.
Kioo chake kinaonyesha vitu kwa ubora na chepesi pale unapotachi simu kwani ni display ya amoled yenye refresh rate ya 120Hz
Kamera zake zote tatu hazina OIS, dual pixel na hazichukui video ya 4K wala video na picha za HDR10+
Changamoto itakuwepo ukipiga picha nyakati za usiku hasa kwenye mwanga mdogo.
Sifa za samsung galaxy m52 5G.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED Plus, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,076,010/= |
SAMSUNG GALAXY M22
Samsung galaxy m22 inafanana sifa nyingi na Samsung M32 hivyo hutaitazama kiundani.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB,128GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera NNE
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 624,780/= |
Hitimisho
Bei za simu nzuri za samsung zinatofautiana kulingana na sifa za simu husika.
Baadhi ya simu za samsung A-series huuzwa bei nafuu kwa sababu zina vitu vingi vyenye ubora mdogo.
Kiujumla muhitaji wa samsung inabidi azingatie bajeti kwa sababu si kila simu ya samsung ni nzuri.