Kuna simu hutengenezwa kwa kulenga aina ya watumiaji ambao wana bajeti ndogo.
Mara nyingi simu za bei nafuu huwa zinaundwa kwa vitu vichache vyenye ubora wa wastani lakini vinasaidia pakubwa.
Infinix hutengeneza simu za aina hii.
Ubora wa simu za infinix upo sana kwenye betri na ukaaji wa chaji muda mrefu.
Simu bora za infinix mara nyingi hutumia processor zenye ubora wa kati(mid-range) za MediaTek G-Series.
Kuna simu kali za infinix ambazo zina vitu vizuri baadhi na huuzwa kwa bei ya kueleweka(nafuu).
Hizi ni baadhi.
Orodha ya simu zilizopo hapo juu zinaweza zikawa zina ufanano lakini kuna idara ambazo zinafanya simu kutofautiana ubora.
Ni vizuri ukazichimba simu za infinix kiundani.
INFINIX HOT 11 PLAY
Simu ya infinix hot 11 play ni simu ya bajeti ya chini.
Inasapoti mtandao wa 4G lakini simu haina 5G, 4G yake sio ile yenye kasi kubwa yaani Cat-12.
Inatumia processor ya ubora wa chini ambayo inatumia mdogo unaofanya simu kukaa na chaji muda mrefu.
Processor yake ni MediaTek Helio G35.
Ubora wa infinix hot 11 play umejikita sana kwenye betri.
Betri yake ina ukubwa wa 6000mAh lakini chaji yake inapeleka umeme kidogo na kufanya simu kujaa chaji kwa muda mrefu.
Display(Kioo) yake si ya kuvutia, resolution ni ndogo na inatumia IPS LCD ambayo huwa ina rangi chache kulinganisha na AMOLED.
Kamera zake mbili na zenyewe si nzuri hazina vitu vizuri vya kamera.
Hot 11 play haina viwango vya IP vinavyoonyesha uimara wa simu kutoingia maji hata ikizamishwa kwenye maji.
Pitia hapa uzitazame simu bora zenye IP68
Simu hii inatumia muundo wa memori aina ya eMMc hauna kasi kubwa ya kuhifadhi vitu ukilinganisha na UFS.
Ni simu nzuri kwa wenye bajeti ndogo na wasio na matumizi makubwa ya simu.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMc 5.1, 64GB, 128GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.82 |
Chaji na Betri |
|
INFINIX NOTE 11
Infinix note 11 ni moja ya simu bora ya infinix hasa upande wa kioo na chaji inayojaza simu kwa kasi.
Kioo chake kinaonyesha picha kwa uhalisia na vitu vinaonekana vizuri hata ukiwa juani.
Ubora wa kioo ni kutokana na kutumia kioo cha amoled na nits 600.
Chaji ya infinix note 11 inapeleka umeme mwingi wa 33W.
Simu nyingi za wati 33 hujaza betri ndani ya dakika 80.
Karibu simu za infinix huwa zina 4G bila kuwa na 5G.
Kamera yake haina uwezo wa kuchukia video zenye ubora mkubwa wa 4K.
Na imewekewa glasi upande wa mbele lakini si gorilla na plastiki upande wa nyuma.
Plastiki huwahi kuchakaa mapema simu inahitaji kava.
Kamera zake tatu zote hazina OIS na HDR10.
Mfumo wa kamera si mzuri kiujumla.
Memori yake ina ukubwa wa 64 GB na 128G.
Na RAM zike zipo za matole ya 4GB na 6GB.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED |
Softawre |
|
Memori | 64GB na RAM 4GB, 128GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
INFINIX HOT 11s
Infinix hot 11s ni simu ya kawaida kwa mtu ambaye si mtumiaji wa vitu vingi.
Ina kamera tatu ila kamera inayopiga picha ni moja yaani kamera kuu.
Nyingine depth sensor hutumika kuscan kiundani kitu kinachpigwa picha.
Ni kamera ambayo inaweza isitoe picha nzuri kwenye mwanga hafifu.
Haina fast charge hivyo betri yake yenye ujazo wa 5000mAh inacgukua muda kujaa.
Inatumia teknolojia ya zamani ya memori inayofahamika kama eMMc.
Kwa mtumiaji wa kawaida bado ni smartphone nzuri na ukubwa wake ni 128GB na 64GB
Zenye RAM ya 4GB na 6GB.
Kioo chake ni chepesi ila hakitumii AMOLED bali ni IPS LCD.
Simu haina 5G bali ina 4G.
Simu hii haina ulinzi dhidi ya maji kutokana na kutokuwepo kwa IP68.
Zipo baadhi ya simu za oppo ambazo zina amoled pamoja na IP68 ila kwa infinix zilizopo hapa zote hazina.
Kiufupi ni simu ya infinix nzuri kwa watu wasio hitaji mambo mengi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMc 5.1, 64GB, 128GB na RAM 4GB kwa 6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
INFINIX ZERO X PRO
Hii ni simu nzuri yenye mfumo bora wa kamera.
Infinix zero x pro ina kamera tatu.
- Wide ina megapixel 108
- Telephoto
- Ultrawide
Kamera mbili za kwanza zina OIS.
Ukiwa na OIS kamera hutulia wakati unachukua video huku unatembea.
Kwa kitu kinachotembea huonekana vizuri.
Kikubwa kizuri kabisa kuhusu kamera ya simu ya infinix zero x pro ni kutumia teknolojia ya dual pixel kwenye kamera kuu na telephoto.
Mfumo wa dual pixel unasaidia kamera kurenga kwa usahihi kitu kinachopigwa picha.
Lakini pia dual pixel huongeza ubora wa picha zinazopigwa kwenye mwanga hafifu.
Kamera yake ina uwezo wa kupiga video ya 4k.
Memori ya infinix zero x pro ina kasi kwa sababu inatumia UFS 2.2.
Na ina ukubwa wa 128GB na 256GB na RAM yake ni 8GB.
Mfumo wake wa chaji unajaza betri lake la 4500mAh kwa asilimia 45 ndani ya dakika 15.
Chaji inapeleka umeme wa 45W.
Kioo chake ni cha AMOLED ambacho huonyesha picha hata video kwa usahihi mkubwa.
Ni kioo chenye 120Hz inayofanya simu kuwa nyepesi.
Simu haina 5G kwa sababu inatumia processor ya Mediatek Helio G95.
Chip ya helio g95 ni nzuri ila infinix walipaswa waweke chip yenye ubora zaidi ya hii ili itumie kamera za hii simu kwa ubora.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB, 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
INFINIX NOTE 11 PRO
Infinix note 11 pro inatumia processor nzuri yaney uwezo wa kati ya MediaTek Helio G96.
Hivyo network yake haina 5G bali 4G ambayo ina spidi kubwa ya kudownload ya 390Mbps.
Kioo chake kinatumia teknolojia ya IPS LCD ambacho ubora wa picha si mkubwa sana ukulinganisha na AMOLED.
Kwa mfano IPS LCD haionyeshi rangi halisi nyeusi.
Ila kioo ni chepesi kwa sababu kina refresh rate 120Hz.
Memori ni ya kasi na ina ukubwa 128GB na RAM ya 8GB.
Mfumo wake wa kamera unaweza kuonyesha picha mbaya hasa nyakati za usiku.
Hili linachangiwa na kamera kukosa teknolojia ya dual pixel.
Pia kamera zake tatu hazina OIS na zinapiga picha za ubora wa HD na sio 4k ambayo ni bora zaidi.
Mfumo wake wa chaji wa 33W unaweza kujaza betri lake la 5000mAh ndani ya dakika 90 kimakadirio.
Infinix note 11 pro ni simu pana na ndefu ambayo inaweza kudumu kwa muda mrefu kutokana na kutengenezwa kwa glasi upande wa mbele na nyuma ila pembeni plastiki.
Simu hii haina waterproof ni vizuri kuwa makini uitumiapo wakati wa mvua.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.95inchi |
Chaji na Betri |
|
INFINIX ZERO X
Simu ya infinix zero x inafanana kwa kila kitu na infinix zero x pro
Pitia Hapa: Sifa za infinix zero x pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
INFINIX ZERO X NEO
Infinix zero x neo simu ambayo inakupa utendaji mkubwa kutokana na kutumia chip yenye ubora wa kati ya MediaTek Helio G95.
Hivyo simu haina 5G bali ina 4G yenye kasi kubwa ya kudownload.
Spidi ya juu kabisa ya modem iliyopo kwenye SoC ya helio G95 ni 600Mbps.
Kioo chake yaani display ni kizuri kwa kiasi hasa wakati wa kutachi ni chepesi sababu ya kuwa na refresh rate ya 90Hz.
Kwa bahati mbaya kioo hakijawezeshwa HDR10.
Video za HDR10 huwa zinaonekana vizuri sana.
Memori yake ina kasi kubwa pale unapokopi vitu kwa sababu ya kutumia UFS 2.2
UFS 2.2 hufanya sababu kuwahi kuwaka chini ya sekunde tano applikesheni za simu kufunga kwa haraka pasipo kukwama kwama.
Ukubwa wa memori ni 128GB na RAM ya 6GB.
Kamera kuu ina ukubwa wa megapixel 48 ila haina OIS wala dual pixel.
Wakati wa usiku picha zinaweza zisitokee vizuri.
Kamera ya telephoto inayoweza kupiga picha za mbali bila kupoteza ubora ina OIS.
Kwa hiyo video itatokea bila kutingishika.
Kamera ya ininix zero x neo haiwezi kupiga picha za 4K.
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kama ukiizamisha sababu haina IP68.
Chaji ya infinix zero x neo hupeleka umeme wa kawaida wa 18 hivyo betri yake yenye ujazo wa 5000mAh inaweza chukua muda wa takribani masaa mataty kujaa.
Sifa za infinix zero x neo kwa ufupi.
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g na 4G |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Maoni 3 kuhusu “Simu Nzuri za Infinix na Bei Zake 2022”
nataka infinix hot 8 napa taje nipo ukerewe mwanza
Infinix hot 8 ni simu ya 2019 upatikanaji wake 2023 ni changamoto
Nataka kujua bei ya infinix zero pro