Kila mwezi wa tisa kampuni ya Apple ya Marekani hutangaza simu mpya za iphone
Katika uzinduzi apple huanisha vitu vipya simu zinazokuja nazo na bei zake kwa kila toleo
Kwa mwaka 2024 apple wamezindua simu za iphone 16, simu hizo ni
- Apple iPhone 16
- Apple iPhone 16 Plus
- Apple iPhone 16 Pro
- Apple iPhone 16 Pro Max
Kwenye hizi iphone mpya zimekuja na mabadiliko madogo sana
Kiasi cha kwamba kwa mtumiaji wa kawaida wa iPhone 15 Pro anaweza asione haja ya kununua iPhone 16
Sababu kubwa hakuna tofauti ya kimuundo na wala hata vipya vya kusisimua
Hata yapo mambo mapya kwenye hizi simu
Vitu vipya vinavyopatikana
Kwanza simu zote zinatumia processor mpya kabisa
Processor hizo ni Apple A18 na Apple A18 Pro
Apple A18 na Apple A18 Pro zinatarjiwa kuwa na nguvu na ufanisi mzuri wa matumizi ya betri
Hii inamaanisha nini?
Simu matoleo ya iPhone 16 zinatarajiwa kukaa na chaji muda mrefu
Katika uzinduzi, apple walianisha kuwa chip mpya zitakuwa na uimara wa kiutendaji na ufanisi wa betri kwa zaidi ya 30% ukilinganisha na toleo lilopita
Kitu kikubwa ambacho kinaonekana kipya sana ni uwepo wa akili mnemba(Artificial Intellignece-AI)
Apple wanaibrand kama Apple Intelligence pamoja na uwepo wa ChatGPT
Moja ya vitu utakavyoweza kufanya ni kuondoa kitu ambacho hukitaki kilichotokea kwenye picha
Hiki sio kitu kigeni kwenye simu za Android
Tayari zipo kwenye simu za Google Pixel, Samsung, Infinix, Oppo na nyinginezo
Pia kuna ongezeko la batani mbili zinaoitwa action button na camera control button
Action button inakusaidia kufungu baadhi ya app kama shazam, app za kutafsiri lugha nk
Camera control kama neno linavyoonesha inaweza kuzoom kamera, kubadilisha aina ya lensi, kurekodi video na mengineyo
Na uwezo wa kurekodi video za 4K kwa kiwango cha fremu 120fps
Sasa tuangalie kwa ufupi simu moja baada ya nyingine
Apple iPhone 16
Apple iPhone 16 kimo chake ni inchi 6.1
Ndio iphone 16 yenye kimo kidogo zaidi inafaa kwa wanaopenda simu portable
Ina matoleo ya GB 128, 256 na 512 huku ukubwa wa RAM ni GB 8
Simu ina kamera mbili zenye lenzi za wide na ultrawide na zinaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 120fps
Inatumia chip ya Apple A18
Na bei yake iliyotangazwa ni shilingi milioni 2.3 za kitanzania
Apple iPhone 16 Plus
Apple iPhone 16 Plus haina tofauti na iPhone 16
Sifa zao zinafanana na zinatofauitiana katika eneo moja tu
Eneo hilo ni kimo, iPhone 16 Plus ni ndefu sana kuliko mwenzie
Urefu wa iPhone 16 Plus ni inchi 6.7
Apple iPhone 16 Pro
Apple iPhone 16 Pro inakuja katika matoleo manne kwenye ukubwa wa memori
Kuna ya GB 128, 256, 512 NA TB 1 yaani GB 1020
Urefu wa iPhone 16 Pro ni inchi 6.3
Na kiutendaji ina nguvu sana kwa sababu inatumia chip ya Apple A18 Pro
Bei ya kuanzia ya hii simu ni shilingi milioni 2.9
Apple iPhone 16 Pro Max
Apple iPhone 16 Pro haina tofauti kisifa na iPhone 16 Pro
Tofauti yao kubwa ni urefu
iPhone 16 Pro Max ina kimo cha inchi 6.9
Hii ndio iphone ndefu zaidi kuwahi kutokea
Bei ya iPhone 16 Pro Max ni shilingi milioni 3.5