Kampuni ya apple imetoa matole manne ya simu mpya za iphone kwa mwaka 2022
Simu hizo ni iPhone 14, iPhone 14 Plus, iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max
Kwa kutazama muundo, hizi simu zinafanana kwa kiwango na matoleo ya iPhone 13
Ila kuna maboresho mapya ambayo hayakuwepo kwenye matoleo yaliyopita
Vitu vipya vilivyopo kwenye iphone 14 zote
Matoleo mapya ya apple yameweka maboresho kwenye chip (processor), kamera, kioo (display) na software kwa maana mfumo endeshi
Kamera
Kwa mara ya kwanza apple wamekuja na kamera yenye megapixel kubwa
Kamera hii ipo kwenye iPhone 14 Pro Max na iPhone 14 Pro na kamera ina 48MP
Kikawaida simu za apple huwa zinatumia kamera zenye megapixel 12
kubwa huo ni kawaida sana kwenye simu za Android ambazo kwa miaka mbili zimekuwa zinakuja na megapixel za kutosha
Kwa mfano camera ya Samsung Galaxy S22 Ultra ina kamera ya 108MP inayoweza kurekodi video za 8K kwa frem 30fps
iPhone zingine zimeendelea kutumia kamera za 12MP
Kumbuka wingi wa megapixel si kitu pekee kinachotambulisha ubora wa kamera ya simu
Ndio maana hata simu zenye megapixel kubwa huwa zinapiga picha za 12MP
Ni mpaka ubadirishe settings ndio zinapiga picha za megapixel 48 (au kubwa yoyote)
Mfumo Endeshi
iPhone mpya za 2022 zinakuja na mfumo endeshi wa iOS 16
Huu ni mfumo unaoruhusu always on display kwa mara ya kwanza kwenye iPhone
Hivyo mtumiaji ataweza kuangalia muda simu ikiwa imejilock
Kwa mtumiaji wa simu za Android sio kitu kigeni kwani kimekuwepo kwenye simu nyingi kwa muda sasa
Ila upande wa iOS zilizopita hazikuwa zinatoa hiko kitu
Display (Kioo)
Mara hii apple wametumia kioo kilichowezeshwa LTPO
Samsung pia wamekuwa wakitumia vioo vya aina hii kwa miaka mingi
Kitu kingine ni kwamba kamera ya selfie ipo ndani ya kioo na sio kwa juu kama zamani
Hivyo display imekava urefu wa simu yote
Kwenye kamera kuna kitu kimeongezwa kinaitwa dynamic island
dynamic island inaonyesha icon za app pindi unapoifunga
Ukiboonyeza upana wa dynamic island uongezeka na unaweza kuifungua app
Hii kitu inafanya animation nzuri
Processor
Maboresho makubwa yamefanyika kwenye utendaji kwa kuweka chip yenye nguvu kubwa
Kwa mujibu wa kampuni ya apple, Apple A16 Bionic ina nguvu zaidi ya 40% ya washindani
Kwa maana Snapdragon 8+ Gen 1 inaachwa nyuma na Apple A16 Bionic
Snapdragon 8+ Gen 1 ni processor ya inayotumika kwenye simu a daraja za juu za android
Ndio chip yenye nguvu kwa sasa lakini bado imeshindwa kuifikia Apple A15 Bion achilia mbali Apple A16
Kwa mujibu wa data za geekbench zilizovuja hivi karibuni zimeonyesha processor apple ina alama 1800 kwenye core moja
Ila iPhone 14 na iPhone 14 Plus zinakuja na Apple A15 Bionic
Hazina tofauti na simu za iPhone 13
Sifa za simu za iphone mpya
iPhone 14
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,400,000/= |
iPhone 14 Plus
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,681,800.00/= |
iPhone 14 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB,1020GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,915,000.00/= |
iPhone 14 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB,1020GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,381,400.00/= |