Umeshawahi kujikuta unatumia simu ila inakuwa ya moto hata kwa kazi ndogo
Unaweza ukajiuliza kwa nini
Kuna vitu vingi vinavyosababisha simu kupata moto ambavyo huna budi kuvifahamu
Kwani simu kuwa joto jingi muda mrefu kunaathiri utendaji wa simu na betri inaweza kufa
Hivyo hapa kuna maelezo yanayofafanua jinsi simu inavyopata moto na jinsi ya suluhisho zake
Hizi ni baadhi
Kutumia apps nyingi wakati mmoja
App zikiwa nyingi zinatumika wakati mmoja zinakuwa zinatumia moto mwingi wa betri
Na hivyo inailazimisha mfumo wa simu nzima kutumia nguvu kubwa
Kitu kinachopelekea kuongezeka kwa joto
Moja ya app ambayo inakamua sana betri ni kivinjari cha Google Chrome
Kudhibiti tatizo hili ni kufunga baadhi ya apps ambazo huzitumii wakati huo
Zifunge zote na utumie ile yenye umuhimu
Betri ya bovu
Mara nyingi betri bovu hupata joto sana hata kwa app isiyohitaji nguvu kubwa
Kama una simu inayowahi kuisha chaji kwa haraka na kupata joto haraka kuna uwezekano kuwa betri yake ni mbovu
Kupata uhakika kuna apps ambazo zinaonyesha afya ya betri
App nzuri kabisa ni AccuBattery
Hii app itakuonyesha afya betri yako na uwezo wake wa sasa
Kama unamiliki simu yenye betri 5000mAh app itakuonyesha kiwango kilichopungua
Iwapo upunguaji ni wa kiwango kikubwa basi betri ni bovu na ndio inasbabisha joto kwenye simu
Hivyo huna budi kutafuta betri jingine na ubadirishe
Mfumo wa simu kuji-update
Wakati mwingine mfumo endeshi mfano Android unaweza ukawa unafanya maboresho yaani upgrading
Upgrading huwa inakuja na vitu vingi
Vitu ambavyo vitakuwa vinawekwa kwenye simu
Uwekaji ambao utailazimisha simu kufanya kazi kubwa
Unaweza kwenda kwenye settings kisha kutafuta update na kuizima
Kama update ni ya muhimu basi vumilia kwa muda mfupi simu imalize huo mchakato
Uwepo wa Virusi(Malware)
Malware kwenye simu mara huwa inalenga kuchota data zako ama kuharibu simu
Ila siku hizi virusi huwa zinalenga kuchota data zako bila wewe kujua ama kuweka matangazo mengi kwenye simu
Unaweza kujikuta kila wakati “notification” za matangazo zinatokea mara kwa mara
Virusi huwa zinajaribu kutuma data kila wakati hata kama intaneti ikiwa imezimwa
Kitendo cha app aina ya aina hiyo inailazimisha simu kufanya kazi kubwa na kusababisha matumizi makubwa ya betri na hivyo simu kuanza kupata moto
Ili kudhibiti app ya namna hiyo, inakupasa uguse sehemu ya settings kisha utafute sehemu ya betri na ubonyeze
Ukibonyeza utaona kiwango cha matumizi ya betri na app zinazotumia na app zinazokula moto sana
Ukiona app ambayo huifahamu kuna uwezekano kuwa hiyo app ni kirusi
Baadhi ya kufunguka bila wewe kujua
Baadhi ya app huwa zinajufungua pasipo wewe kuona hii inaitwa “opening in background”
Mfano wa app hizo ni whatsapp, instagram, chrome, tiktok na nyingine
Iwapo app nyingi zinajifungua kwa muundo huo basi simu inaweza pata moto
Hivyo huna budi kupunguza app ambazo zitakazokuwa zinajungua zenyewe
Ili kufanya hivyo unaenda kwenye settings kisha sehemu ya app halafu unachgua app unazotaka kuzifunga
Kutumia simu maeneo ya joto sana
Ukiwa unatumia simu kwenye eneo lenye joto sana mfano juani inafanya simu kuchemka
Joto jingi hufanya kila kitu kupata cha simu kupata moto
Na kadri unavyoitumia simu kwenye mazingira na ndivyo simu inavyozidi kuchemka
Ni si vizuri kuitumia simu kwenye jua kali
Suluhisho la tatizo hili ni kupunguza kuitumia simu kwenye mazingira hayo
Mwanga mwingi wa Screen
Moja ya kitu kinachokamua sana ni kioo cha simu hasa kikiwa kina resolution kubwa
Na pia kuweka mwanga wa kioo mpaka mwisho kunasababisha kutumika kiasi kikubwa cha betri
Hivyo inasababisha simu itumie nguvu kubwa kufanya kazi
Kiwango kikubwa cha mwanga kunaonheza joto
Joto linalosababisha simu nzima kuchemka
Hivyo unapopata tatizo la simu kuchemka jaribu kupunguza mwanga wa simu
Aina ya Processor ya Simu
Baadho ya simu kupata moto kunasabishwa na uwezo wa processor yenyewe
Watengenezaji wanaweza kuwa hawakiunda chip vizuri au uwezo wa chip si mkubwa
Hivyo simu inaweza kuwa inapata shida hata kwa kazi ndogo
Processor yenye nguvu ndogo hulazimika kufanya kazi kubwa kwa app ya aina yoyote hasa magemu
Huna budi kujua nguvu ya simu yako
Na hivyo uanze kupunguza matumizi ya simu hasa yale ambayo yanatumia nguvu kubwa
Kutumia chaji isiyo sahihi
Kila simu ina muundo wake saketi kwa ajili ya kupeleka
Baadhi ya simu zimeundwa kupokea chaji inayopeleka taratibu tu
Hivyo ukiweka chaji yenye kasi sana na mfumo wa simu ukawa hauna uwezo wa kupunguza kiwango cha umeme wa chaji basi itaenda kuharibu betri kwa kadri utakavyokuwa unachaji
Na betri ikiwa mbovu basi simu itaanza kuwa inapata moto
Ni vizuri ukazingitia matumizi ya chaji sahihi ili kuepuka uharibifu wa simu
Maoni 17 kuhusu “Sababu na Jinsi ya Kudhibiti Simu Kupata Moto Sana”
Simu yangu ina peleka charge taratibu sana kwa sasahiv ila mwanzo ilikua haipo hivyo
Umejaribu kubadili chaji kujua kama tatizo chaji au betri
simu yang nikiwasha data t inapatamoto
Pole Sana, simu yako ya Aina gani
Simu yangu nikiwasha data au kucheza game inachemka Dana?
Simu yangu Infinix smart 7 shida nikiwasha data au kucheza game inachemka sana
Smart 7 sio simu yenye nguvu kubwa Kwa kucheza gemu
Samsung A03CORE inachemka nkiingia social networks tofauti na mwanzo imeanza ghafla tu
Dali za betri kuharibika
sim yangu haipelek chaj nimejalibu kubadilisha sstim chaj lakin bado samsung a10s
Jaribu kuweka betri linguine pia
Simu yangu Infinix Smart 7 plus inapata moto sana hata ukiwa ujawasha data ukiwa na matumizi ya kawaida tyu
Ina muda gani tangu umenunua?
Simy yangu inatatizo la kupata moto Sana wakati wa kuweka chaji (kuchaji cm)sijuh shida nini
Simu yangu SMART 5 inatatizo la kupata moto Sana wakati wa kuweka chaji (kuchaji cm)sijuh shida nini wakati mwanzoni haikuwa hivyo
Kuna uwezekano betri imeanza kuharibika
Simu yangu inachemka Sana aina ya Simu ni Quantum 3