SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Bora za Xiaomi na bei zake 2022

Brand

Sihaba Mikole

February 7, 2022

Xiaomi ni kampuni namba tatu duniani kwa uuzaji wa simu nyuma ya Samsung na Apple.

Sifa kubwa ya simu za xiaomi ni kutengeneza simu zenye vitu vinavyoptikana kwenye simu za bei juu kwa bei inayovumulika.

Mfano mzuri ni xiaomi redmi note 10 na note 10 pro.

Bei zake ni za chini lakini ni simu bora kwenye mengi, simu hii ingekuwa inauzwa na kampuni zingine basi bei ingekuwa juu.

Simu za xiaomi na bei zake kwa ujumla zinakupa smartphone yenye sifa ya utendaji mkubwa na kamera nzuri

Hivyo hapa kuna orodha ya baadhi ya simu nzuri za  xiaomi upande wa brand za redmi na pocco.

Kwa sifa za xiaomi, utajua ubora wake na bei zake na utaona jinsi simu zao zilivyo na bei rahisi.

Kila simu iliyopo kuna idara yenye vitu vikali ambavyo kwa watumiaji wa simu ni vya muhimu.

Ni vizuri ukapitia kila simu kiundani kujua ubora wake.

XIAOMI 12 PRO

Xiaomi 12 pro ni simu bora ambayo ina mfumo wa chaji unaojaza simu kwa 100% ndani ya dakika 8 tu.

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi mno wa 120W.

Haishangazi betri yake ya ujazo wa 4600mAh kujaa kwa haraka hivyo.

Kiuwezo, unaweza linganisha simu hii na simu za oppo matoleo ya reno

simu-nzuri-ya-xiaomi-12-pro

Xiaomi 12 pro inatumia processor mpya ya Snapdragon 8 Gen 1 hivyo simu inasapoti 5G ya kila aina(sub-6, SA, NSA na mmWave).

Snapdragon 8 Gen 1 ni boresho la snapdragon 888 ambayo ina changamoto ya simu zake kukaa na chaji muda mrefu.

Maboresho yamefanya snapdragon kutumia miundo mitatu Cortex-X2, Cortex-A710 na Cortex A510.

Ni mifumo yenye utendaji mkubwa na utunzaji chaji wa ufanisi.

Kioo chake LTP AMOLED  ni ang’avu kinachoonyesha vitu kwa uzuri.

Na kina uwezo wa kuonyesha video za ubora wa HDR10+

Pia kioo kina glassi ngumu kuvunjika ya Gorilla Victus.

Memori yake aina ya UFS 3.1 zenye ukubwa wa 128GB na 256GB zina kasi kubwa inayochangia intaneti kudownload vitu kwa haraka sana simu kuwahi kuwaka kama uliizima.

Simu ina sensa ya kamera kubwa na kamera imewekewa mfumo wa dual pixel hivyo picha huonekana vizuri zikipigwa nyakati za usiku.

Lakini pia video zake hutulia endapo mchukuaji wa video anachukua huku akiwa anatembea kutokana na kamera kuu kuwa na OIS.

Simu haina IP68 hivyo ungarifu ni muhimu uitumiapo kwenye mvua.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 8 Gen 1
  • Core Zenye nguvu(2) – 1×3.0GHz Cortex X2, 3×2.50GHz
  • Core Za kawaida(6) – 4×1.8GHz Cortex-A710
  • GPU-Adreno 730
Display(Kioo) LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • MIUI 13
Memori UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB, 12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP(Main)
  2. 50MP(TelePhoto)
  3. 50MP(Ultrawide)
  4. 32MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.73inchi
Chaji na Betri
  • 4600mAh-Li-Po
  • Chaji-120W
Bei ya simu(TSH) 2,080,286/=

XIAOMI REDMI NOTE 11

Ni simu ambayo imeingia sokoni mwaka 2022 mwezi februari.

Xiaomi redmi note 11 inatumia processor ya ubora wa kati ya snapdragon 680.

Hivyo note 11 haina mtandao wa 5G bali wa 4G  wenye kasi kubwa ya kudownload.

simu nzuri ya xiaomi RedmiNote11

Kutokana na kutumia SoC ya snapdragon 680, simu inaweza kukaa na chaji masaa mengi kwa sababu chip imetengenezwa kwa muundo wa Kryo 265 wenye ufanisi mkubwa wa moto na uwezo wa kawaida.

Betri yake ya 5000mAh inajaa chaji kwa asilimia 100 ndani ya dakika tofauti na redmi note 10 ambayo hujaa kwa dakika 75.

Kioo chake cha Super Amoled kina IP53 kwa maana maji yanayotiririka(mvua) na vumbi haviwezi penya ndani ya simu.

Video na picha huonekana vizuri sana kwenye vioo vya amoled.

Memori yake za ukubwa wa 64GB na 128GB ina kasi kubwa kutokana na kutumia muundo wa UFS toleo 2.2

Kamera zake nne hazina OIS wala dual pixel ikiwemo kamefa kubwa ya megapixel 50.

Hivyo si nzuri ukiwa unapiga picha huku unatembea au eneo lenye mwanga mdogo sana.

Sifa za xiaomi redmi note 11 kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g na 4G
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680
  • Core Zenye nguvu(2) – 4×2.4GHz kryo 265
  • Core Za kawaida(6) – 4×1.9GHz kryo 265
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 13
Memori UFS 2.2, 64GB, 128GB na RAM 4GB, 6GB
Kamera Kamera nne

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(ultrawide)
  3. 2MP(macro)
  4. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.43inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 370,240/=

XIAOMI REDMI NOTE 11 PRO

Xiaomi redmi note 11 pro ni simu ndefu kidogo kulinganisha na redmi note 10 kwani ina urefu wa inchi 6.67.

Sifa zote zinafana na mtangulizi wake ila utofauti upo kwenye aina ya processor,kamera na mfumo wa chaji.

Mfumo wa chaji wa redmi note 11 umeboreshwa kwa kuongezewa kiwango cha umeme kiendacho kwenye betri.

simu nzuri ya xiaomi redmi note 11 pro

Chaji yake ni ya wati 67, kiasi cha umeme kinachoweza kujaza betri kwa asilimia 51 kwa dakika 15 tu.

Processor iliyopo kwenye redmi note 11 pro ni MediaTek Helio G96 ambayo ina nguvu kuliko Snapdragon 680 kiutendaji.

App zinazohitaji nguvu kubwa zitafunguka kwa wepesi na haraka kwenye note 11 pro kuliko kwenye redmi note 11.

Kamera kubwa ya megapixel 108 ina dual pixel PDAF.

dual pixel PDAF husaidia kamera ya simu kwa haraka na usahihi kitu kinachpigwa picha na pia hukusanya mwaka mwingi ambao unafanya picha iliyopigwa kwenye mwanga hafifu kuonekana kwa ustadi.

Mengineyo yanafanana kama unavyoweza kuona sifa za hii simu kwa ufupi,

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G96
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05GHz Cortex A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0GHz Cortex A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 13
Memori UFS 2.2, 64GB,128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera nne

  1. 108MP,PDAF,dual pixel
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 2MP(Macro)
  4. 2MP(Depth)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-67W
Bei ya simu(TSH) 711,125

XIAOMI 12X

Xiaomi 12x ni simu yenye urefu na upana wa wastani wa kimo cha inchi 6.2

Inatumia processor yenye ubora wa juu ya Snapdragon 870 5G hivyo simu inasapoti mtandao wa 5G.

Kioo chake cha oled kinakupa nafasi ya kuona vitu kwa ungavu na ubora lakini hakiwekewa ulinzi wa kuzuia maji kwa maana hakuna IP68.

simu bora ya xiaomi 12x

Na kipo fasta(Chepesi) ukiwa unatachi simu kwenda juu ama chini(ku-scroll) sababu ya kuwa na refresh rate ya 120Hz.

Memori zake za 128GB na 256GB huifadhi vitu(mafaili) kwa haraka kwa sababu ya kutumia mfumo wa UFS 3.1 na kufanya simu kufunga kwa sekunde chache sana ukiwa unaiwasha.

Betri yake yenye ujazo wa 4500mAh hujaa ndani ya dakika 37 kwa sababu mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi wa 67W

Kamera zake tatu ni moja tu yenye OIS ambayo ni kamera kubwa yenye megapixel.

Ukiwa na OIS video inatokea ikiwa imetulia hata ukipiga huku ukiwa unatembea.

Sifa za xiaomi 12x kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 870 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 1×3.2GHz kryo 585, 3×2.42GHz kryo 585
  • Core Za kawaida(6) – 4×1.8GHz kryo 585
  • GPU-Adreno 650
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • MIUI 13
Memori UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB,12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF,OIS
  2. 13MP(Ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 32MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.28inchi
Chaji na Betri
  • 4500mAh-Li-Po
  • Chaji-67W
Bei ya simu(TSH) 1,640,625/=

XIAOMI REDMI 10

Simu ya xiaomi redmi 10 inatumia chip ya ubora wa kati ya MediaTek Helio G88.

Helio G88 ina modem inayosapoti mtandao wa 4G.

Ni chip ambayo simu nyingi za infinix hutumia

Kwa kuwa chip ni ya kawaida xiaomi redmi 10 inakaa na chaji muda mrefu (masaa 127) sababu chip hii imeundwa kutumia umeme mdogo na uwezo wa wastani.

simu nzuri xiaomi redmi-10

Muundo wa chip wa Cortex A75 na Cortex A55 una kawaida wa kufanya nyingi kwa uwezo wa kawaida na matumizi madogo ya betri.

Hivyo betri lake la 5000mAh litadumu.

Na mfumom wake wa chaji unapeleka umeme wa 18W. Kiwango hiki cha umeme kinajaza betri muda mrefu.

Kioo chake ni cha LCD kipo fasta ukitachi lakini kinaonyesha picha kwa ubora mdogo ukilinganisha na vioo vya amoled.

Kioo chake kinalindwa na glasi ya gorilla 3, ni imara kuzuia michubuko.

Kamera zake nne zote hazina OIS na dual pixel na hazichukui video zenye ubora wa 4K ikiwemo kamera kubwa yenye megapixel 50.

Mfumo wake memori una kasi ya kawaida ya kuhifadhi vitu na kufungua apps.

Kasi yake ni ndogo kwa sababu memori yake ni aina ya eMMc.

Kwa kuzingatia bei, ni simu nzuri ukilinganisha na simu zingine zenye sifa zinazofanan na xiaomi 10.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g na 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G88
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0GHz Cortex A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8GHz Cortex A55
  • GPU-Mali-G52
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12.5
Memori eMMc 5.1,64GB 128GB na RAM 6GB, 4GB
Kamera Kamera nne

  1. 50MP,PDAF
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 2MP(Macro)
  4. 2MP(Depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 1,234,780/=

XIAOMI REDMI NOTE K40 GAMING

Xiaomi redmi K40 Gaming ni simu maalumu inayofaa wapenzi wa magemu ya simu.

Gemu nying huitaji processor yanye nguvu kubwa ili kucheza bila kukwama.

Hivyo redmi k40 inatumia process yenye nguvu ya MediaTek Dimensity 1200.

simu-nzuri-xiaomi-k40-gaming

Simu ina betri kubwa na mfumo unaopeleka chaji kwa haraka kwa sababu gemu humaliza betri kwa kasi.

Betri lake la 5065mAh linajaa kwa asilimia 100 ndani ya dakika 47 kutokana na chaji inayopleka umeme wa 67W kwa kasi.

Simu ni kwa ajili hivyo mfumo wa kamera zake tatu hauna OIS wala dual pixel lakini kamera inaweza chukua video zenye ubora wa 4K.

Gemu pia huhitaji display(kioo) chepesi na ambacho kipo fasta pale kinapoguswa.

Kasi wa kioo hupimwa kwa refresh rate ambayo kwneye simu hii yenye kioo cha OLED ina refresh rate ya 120Hz.

Memori kasi pia inahitajika na yenye ujazo mkubwa kwa sababu gemu huwa zinatumia nafasi kubwa.

Zipo redmi k40 zenye 128GB na 256GB na zote zina mfumo wenye kasi wa UFS 3.1

Sifa zingine za redmi k40 kiundani.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 1200 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 1×3.0GHz , 3×2.6GHz Cortex A78
  • Core Za kawaida(6) – 4×2.0GHz Cortex A78
  • GPU-Mali-G77 MC9
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12.5
Memori UFS 3.1, 128GB,256GB na RAM 8GB,12GB
Kamera Kamera TATU

  1. 64MP,PDAF
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 2MP(Macro)
  4. 16MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 5065mAh-Li-Po
  • Chaji-67W
Bei ya simu(TSH) 1,133,836.86/=

XIAOMI REDMI NOTE 11 PRO 5G

Simu ya xiaomi redmi note 11 pro 5g ni simu ndefu na pana kwa kimo cha inchi 6.67

Inatumia processor yenye ubora wa kati ambayo inasapati network ya 5G.

Processor Snapdragon 696 5g na ina ufanisi mkubwa wa matumizi madogo ya nishati.

simu-nzuri-xiaomi-redmi-note-11-pro

Simu ina betri la 5000mAh, na ina chaji yenye kupeleka umeme mwingi wa 67W.

Hivyo betri hujaa yote ndani ya dakika 42.

Ni kamera moja kati ya kamera zake nne yenye dual pixel na kamera zote hazina OIS.

Hakuna kamera inayochukua video za 4K.

Kamera kubwa ina megapixel 108.

Display(kioo) chake ni kikali sana ukilinganisha note 11 zingine.

Ni angavu na kinaweza kuonyesha picha na video za HDR10

HDR10 huonyesha vitu kwa usahihi wa rangi zake kama zinavyoonekana kwenye mazingira halisi.

Memori yake ni aina ya UFS 2.2, bado ina kasi kubwa kufungua apps kwa haraka.

Zipo Redmi note 11 5G za 64GB na 128GB.

Redmi note 11 5G ni simu nzuri ya xiaomi ukilinganisha na redmi note 11 na pro kisifa.

Sifa za redmi note 11 5G kiufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 695 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2GHz kryo 660
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.7GHz kryo 660
  • GPU-Adreno 619
Display(Kioo) Super AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 13
Memori UFS 2.2, 64GB,128GB na RAM 8GB6GB
Kamera Kamera tatu

  1. 108MP,PDAF(Main)
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 2MP(Macro)
  4. 16MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-67W
Bei ya simu(TSH) 763,900/=

XIAOMI POCO F3

Simu ya xiaomi poco f3 inatumia chip ya Snapdragon 875 yenye nguvu na yenye matumizi ya wastani ya betri.

Snapdragon 875 inasapoti mtandao wa 5G.

Ni simu yenye uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kwa takribani masaa 114 ikiwa haitumiki.

simu-nzuri-xiaomi-poco-f3

Betri yake ukubwa wa 4520mAh linaweza kujaa ndani ya dakika 52 kwa sababu chaji ya poco f3 inapeleka umeme mwingi wa 33W.

Memori zake ni aina ya UFS 3.1 inayosaidia simu kuwaka kwa haraka na application kufunguka kwa haraka na simu kuwa fasta.

Zipo poco f3 za 128GB na 256GB. Zinahifadhi vitu vingi mno ikiwemo apps za kutosha.

Kioo chake ni cha amoled na kina protekta ngumu kuvunjika aina ya gorilla glass 5.

Amoled ya poco f3 ni chepesi na kinaonyesha vitu vizuri sababu kubwa ni kuwa na refresh rate ya 120HZ na HDR10+

Pamoja na kuwa na sifa bora lakini upande wa kamera si mzuri kwa sababu kamera zote hazina OIS na dual pixel japokuwa zinaweza chukua video za ubora wa 4k

Sifa za Poco f3 kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 870 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 1×3.2GHz kryo 585
  • Core Za kawaida(6) – 4×1.8GHz kryo 585
  • GPU-Adreno 650
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12.5.6
Memori UFS 3.1, 128GB,256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera moja

  1. 48MP,PDAF
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 2MP(Macro)
  4. 20MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 4200mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 715,026/=

XIAOMI REDMI NOTE 10 5G

Ubora wa simu ya redmi note 10 5g ni kuwa na processor yenye nguvu ambayo inasapoti mtandao wa 5G.

Inatumia chip ya MediaTek Dimensity 700.

Kwenye chanja ya kamera ina IPS LCD, ubora wake haufikii amoled kwenye kuonyesha vitu kwa usahihi.

xiaomi-redmi-note-10-5g

Redmi note 10 5G ni ngumu kupata michubuko(scratch) sababu inatumia Gorilla glass 3.

Memori zake zina kasi za wastani kwenye kufungua apps na kuhifadhi vitu, ni aina ya UFS 2.2

Zipo redmi note 10 5G za 64GB, 128GB na 256GB.

Kamera zake tatu zinakosa vitu kama OIS na dual pixel.

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa wastani wa 18W hivyo betri lake la 5000mAh litachukua muda kujaa.

Sifa za simu ya xiaomi redmi note 10 5G kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 700 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2GHz Cortex A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0GHz Cortex A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12
Memori UFS 2.2, 64GB,128GB,256GB na RAM 8GB,6GB,4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 48MP,PDAF
  2. 2MP(Macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 8MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 1,234,780/=

XIAOMI POCO M4 PRO 5G

Simu ya poco m4 pro 5G inatumia processor nzuri ya MediaTek dimensity 810 ambayo inasapoti 5G.

M4 pro 5g ina betri lenye ukubwa wa 5000mAh na linatunza chaji muda masaa mengi.

Kwa bahati mbaya kamera za nyuma zipo mbili na zote hazina OIS wala dual pixel.

simu-nzuri-xiaomi-poco-m4

Ina chaji yenye kasi kwani inaweza kujaza betri kwa asilimia 100 ndani ya dakika 60.

Kioo chake ni aina ya IPS LCD ambavyo huwa havitumii umeme ukilinganisha na amoled japokuwa ubora wa picha ni wa kawaida sana.

Mfumo wake wa memori ni aina ya UFS 2.2 ambao una kasi kiasi wa kufungua simu na apps kwa haraka.

Zipo poco m4 pro 5g za 64GB na 128GB.

Simu inaweza kuzuia maji yanatiririka(mvua) na vumbi kupenya ndani ya simu.

Ni simu nzuri ya bei nafuu kulingana na sifa zake.

Sifa za xiaomi poco m4 pro 5g.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Dimensity 810 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4GHz Cortex A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0GHz Cortex A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12.5
Memori UFS 2.2, 64GB,128GB na RAM 8GB,6GB
Kamera Kamera mbili

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 8MP(Ultrawide)
  3. 16MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 525,000/=

Wazo moja kuhusu “Simu Bora za Xiaomi na bei zake 2022

  • Nahitaji kuwa nayo simu ya Xiaom Redmi note 11. Naipataje mimi niko kasulu mkoa wa kigoma.

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Bei ya Google Pixel 9 na Sifa zake muhimu

Google Pixel 9 ni simu mpya kabisa ya pixel kwa mwaka 2024 Ni simu kali sana upande wa utendaji, kamera na software hasa katika matumizi ya AI(akili mnemba) Maboresho makubwa […]

iphone thumbnail

iPhone za bei rahisi za kumiliki kwa sasa(2024-2027)

Katika pitapita zangu na kuchunguza simu bora za bei ndogo na ya chini nimekuja kugundua kitu cha kustahajabisha kidogo Wapenzi wa iPhone wenye bajeti ndogo wananunua iphone used hazipokei maboresho […]

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

Simu bora duniani na bei zake 2024

Leo tuzungumzie kuhusu simu bora duniani na bei zake kwa mwaka 2024 Kuna matoleo mapya ya simu kali yenye ubora wa kiutendaji na wenye nguvu madhubuti katika maeneo mengi Ubora […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company