Mwaka 2026 kuna simu kali nyingi zimetoka
Simu bora zaidi bei zake huanzia milion mbili na kuendelea
Lakini unaweza kupata simu bora chini ya laki tano
Inastaajabisha
Ndio maana hapa nimekuwekea simu duniani zaidi katika makundi matatu
Kwa maana hata kama hauna mamilioni ya pesa, chini ya laki tano inaweza kukupa simu bora duniani
Tuanze na vigongo vyenyewe
Daraja la juu
Hapa tumeorodhesha simu tano ikiwemo ambazo hazifahamiki na watu wengi
Samsung Galaxy S26 Ultra
Hii ilitoka rasmi mwezi wa tatu
Na kwa Tanzania bei yake ni shilingi milione nne ya GB 256
Hii ni simu yenye utendaji mkubwa na mfumo imara wa software
Hakuna simu inayofikia kwa kamera nzuri na yenye vitu vingi
Mifumo yake AI imewekwa katika maeneo mengi yanayorahisisha matumizi
Kwa mfano kufanya tafsiri ya lugha kama mtu anayeongea lugha tofauti na yako akipiga simu
iPhone 18 Pro Max
iPhone 18 Pro Max imetoka mwezi wa tisa
Na bei yake kwa hapa Tanzania ni shilingi milioni 4.5
Hii simu imepewa nguvu na prosesa mpya ya Apple A20 Pro
Hii prosesa imeifanya iphone kuwa na nguvu kubwa sana kiutendaji
Kiasi cha kwamba inasapoti AI zilizowekwa ndani simu kwa ufanisi
Hivyo mbeleni AI za offline zinaweza kutumika kwa ustadi kwenye simu
Vivo X300 Ultra
Naloweza kusema hii ni bonge la simu kwa mtu wa kamera
Na sio kamera tu mpaka utendaji
Ila bei yake ni kipengele maana inauzwa shilingi milioni nne na laki tano
Nini hasa spesho kwa hii simu
Kwanza hii simu ina kamera kubwa na zinapiga picha zenye utajiri wa data
Hivyo picha ya mtu inaonyesha kwa undani sana kila kitu
Hii simu ina nguvu kubwa ya kufanya vitu kwa haraka bila kuganda
Pia ina kasi sana ya kujaza betri kwa haraka maana chaji yake ina wati 100
Oppo Find X9 Ultra
Oppo Find X9 Ultra utendaji wake unafanana na Vivo X300 Ultra
Mbali na utendaji kamera yake ina vitu vingi vinavyofanya simu itoe picha nzuri
Kioo chake ina kina kikubwa cha rangi kutokana na uwepo wa dolby vision
Kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za 8k ambazo ni angavu mno
Hii ina fast chaji ya bila kutumia waya
Ambayo kasi yake ni kubwa inafika 50W
Mbali na hilo unaweza kuitumia hii simu kama power mfano kuchaji earphone ya bluetooth
Google Pixel 11 Pro XL
Japokuwa mfumo wa kamera Google Pixel 11 Pro XL haupo kama wa Vivo X300 Ultra ila ina kamera kali
Kwa miaka mingi Google Pixel 11 Pro XL imekuwa kinara upande wa kamera
Hata hili toleo la 2026 liko hivyo pia
Kwa sababu ukitazama picha za kwenye mwanga hafifu zipo safi sana
Kwa maana hata ukiizoom picha ni ngumu kuona chengachenga
Kubwa zaidi ni mfumo wa Android wa pixel ni mrahisi mwepesi na hauna mambo mengi
Bei ya Google Pixel 11 Pro XL ni shilingi milioni nne
Tuangalie sasa simu bora kwenye kundi lingine
Daraja la kati
Hapa kuna makundi ya simu za China na Korea kama ilivyo ada
Samsung Galaxy A57
Imetoka mwezi wa pili 2026
Bei yake ni shilingi milioni moja na laki mbili
Utendaji na kioo pia kamera ndio eneo linalong’aa zaidi kwenye hii simu
Pia chaji yake inasapoti umeme wa wati 45 kiwango cha juu
Hii simu inapokea matoleo mapya ya Android kwa muda wa miaka sita
Hivyo ulinzi na uimara wa simu hautoshuka thamani kwa muda mfupi
Redmi Note 17 Pro
Hii simu imetoka mnamo mwezi August 2026
Ubora wa hii simu ni kuwa ina betri kubwa sana
Hivyo inadumu na chaji masaa mengi
Na ina utendaji mkubwa na ni imara
Kwa maana ina uwezo wa kuzuia maji kama ikizama kwenye maji mengi
Ina kamera mbili na kamera kuu inapiga vitu kwa ustadi
Simu inayofuata baadhi ya watu watanibishia
Simu hiyo ni hii
Infinix Note 60 Pro
Ndio hii ni moja ya simu bora duniani
Na bei yake kwa hapa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki mbili
Utendaji wa Infinix Note 60 Pro unachuana kabisa Redmi Note 17 Pro
Hii simu infinix wameikea vitu vingi vikubwa ambavyo huwa ngumu kukuta kwenye simu za Infinix
Tazama ubora wa kioo, nguvu ya chaji, ubora wa kamera na sapoti ya muda mrefu
Utajua ni namna gani Infinix wamezingatia thamani ya pesa
Halafu kuna hii simu
Realme P4 Power
Hii ni moja ya simu yenye bonge la betri
Inachukua zipatazo siku mbili mpaka chaji kuisha ukiwa unaperuzi muda wote
Kamera yake ubora ni ya kawaida
Lakini jambo lingine hii ni simu kama power bank
Inaweza kuchaji simu nyingine kwa kasi kubwa mno
Ndani ya dakika 80 inaweza kujaza iPhone 18 Pro
Itakuwa tumevunja heshima tukiacha simu kutoka oppo
Oppo Reno 15
Oppo Reno 15 ilitoka rasmi mwaka 2026 mwezi Januari
Ina utendaji mzuri na kamera zake tatu ziko vizuri pia
Kamera yake inajitahidi kuonyesha vizuri na kwa usahihi mkubwa wa rangi
Nyakati za usiku inaweza kuchukua picha na vitu kuonekana kwa uzuri
Betri yake ni kubwa ila kama Realme P4 Power
Betri yake inawahi kujaza simu kwa muda mfuoi kwani ina kasi ya 80W
Bei yake ni shilingi milioni mbili na nusu
Sasa twende kwenye upande
Daraja la mwisho
Huu upande watu watakataa na kusema simu zifuatazo hazistahili
Lakini sio kwani kuna simu za daraja la kati zinaweza kumridhisha mtumiaji bila shida
Na hizi ni baadhi ya hizo simu kati ya nyingi
Redmi 17C
Redmi 17C bei yake ni shilingi laki nne
Ni simu inayosapoti mtandao wa 5G
Na utendaji wake wa wastani unaipa simu uwezo kufanya kazi muda mrefu bila kuganda
Ina kamera yenye ukubwa wa 50MP picha inatokea vizuri katika mazingira yote
Tecno Spark 50 Pro
Hii ni simu ya laki nne yenye waterproof ya IP68
Inamaanisha simu inauwezo wa kuzuia maji ikizama kwenye maji mengi
Pia ina kuja na ukubwa wa memori tofauti tofauti kuanzia 128GB
Chaji yake inapeleka umeme hadi wa wati 60
Ni nadra kwa nyakati hizi kukuta Samsung ya bei hii ikiwa na hizo sifa
Lakini utendaji wake ni wa wastani na unaweza kucheza kila aina ya gemu
Samsung Galaxy A17
Kwa sehemu kubwa Samsung Galaxy A17 inafanana na Spark 50 Pro kiutendaji
Bei ya Samsung Galaxy A17 ni shilingi laki nne
Japo imetoka mwishoni 2025 lakini bado ni moja ya simu nzuri
Honor 8xd
Hii ni simu nyingine bora ya bajeti ya wastani
Honor 8xd ina kioo kizuri chenye kuonyesha kwa kina kikubwa
Betri yake pia inaofanya simu kukaa na chaji takribani siku
Utendaji ni mzuri na hauwezi kuifanya simu kuganda ganda
Kwa Tanzania hii simu unaweza kuipata kwa shilingi laki nane