Simu ya Oppo A96 5G ni boresho la Oppo A96 ambayo ilitumia kioo chenye uwezo wa kuonyesha rangi chache.
Ni simu ya android inayokubali mtandao wa 5G
Oppo A96 5G ina thamani inayokaribiana na Oppo A96.
Simu hii ilizinduliwa kwa kulenga soko la china
Hivyo kwa kuagizia toka china bei inashuka.
Lakini matoleo ya china huwa hayana app za google.
Japokuwa sifa za oppo A96 5G zinafana na A96, ila kuna tofauti kiubora hasa upande wa software
Sifa za OPPO A96 5g kiufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | OLED |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.43inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 718,152.29/= |
Upi ni ubora wa simu ya OPPO A96 5G?
Kutumika kwa processor yenye nguvu ni moja ya ubora wa simu aina ya Oppo A96 5G
Kioo cha oppo a96 5g kinaonyesha rangi nyingi hivyo vitu huonekana kwa uhalisia kwa kiasi kikubwa.
Ni simu ya 5G yenye kukubali aina zote tatu za 5G
Chaji ya OPPO A96 5G inapeleka umEme mwINGI unaojaza betri kwa dakika chache.
Sifa za hii simu kwenye nyanja zingine zinavutia pia .
Network
Simu inakubali mitandao ya aina yote ikiwemo 4G na 5G.
4G iliyomo kwenye simu ni ya kundi la kundi la 18 (cat 18).
Cat 18 inadownload faili kwa kasi inayoweza kufikia 1174Mbps
Kama oppo a96 5g inadownload file la ukubwa wa 1174MB basi kudownload kunamalizika ndani ya sekunde nane
Hii inategemea na mtandao na eneo ulilopo
4G ya oppo a96 5g inakubali network bands 11.
Mitandao yote ya Tanzania inakubali pale 4g inapotumika kwenye intaneti.
Upande wa 5G unafanya kazi kwa aina zote.
Network bands za 5G zipo sita kwenye oppo a96 5g.
Hatutuiangalia 5g kiundani kwa sababu hakuna mtandao wenye aina hii ya network hapa Tanzania.
Ubora wa kioo cha oppo A96 5g
Kioo cha oppo A96 5G ni kioo cha OLED.
Display ya OLED husifika kwa kuonyesha rangi halisi hasa rangi nyeusi.
Kwa sababu simu haitumii taa aina ya LED ili display ionyeshe.
Kioo cha oled kilichopo kwenye simu kina resolution kubwa.
Resolution yenye vipimo vya 1080 x 2400 pixels
Kadri resolution inavyokuwa kubwa ndivyo display ya simu inaonyesha vitu kwa ustadi.
Kina uangavu wa kutosheleza.
Uangavu wake unafikia 600nits.
Ni kiwango kinasaidia kioo kuonyesha vitu vizuri simu ikiwa inatumika juani.
Uwezo wa processor Snapdragon 695 5G
Processor inayoipa nguvu oppo a96 5g ni snapdragon 695 5g
Snapdragon 695 5g ni chip ya kundi la kati.
Ina core nane yaani octacore.
Core zenye nguvu kubwa zipo mbili
Na core zenye nguvu ndogo zipo sita
Simu zenye snapdragon 695 5g zinaweza kufungua applikesheni yeyote bila kukwama
Ikiwemo gemu zinazohitaji nguvu kubwa
Core zenye nguvu kubwa
Core mbili zenye nguvu kubwa zina kasi ya 2.2GHz kwa kila core
Core zote zinatumia muundo Kryo 660 Gold.
Qualcomm hutumia neno Gold kuwakilisha core zenye nguvu kubwa
Kryo 660 Gold imeundwa kwa kutumia Cortex A78
Processor za simu zenye Cortex A78 huwa na utendaji mkubwa ukilinganisha na matoleo ya chini ya A72, A73, A76 na Cortex A77.
Cortex A78 inafanya kazi kubwa zinakula umeme mwingi wa betri.
Lakini munndo huu umeboreshwa kwa matumizi madogo ya betri na utendaji mkubwa
ARM Holding wanadai Cortex A78 inaziba tofauti ya smartphone na laptop kiutendaji
Core zenye nguvu ndogo
Snapdragon 695 5g imeundwa kwa Kryo 660 Silva kwa core zenye nguvu ndogo.
Kryo 660 Silva ni Cortex A55 iliyoboreshwa.
Katika core sita zenye nguvu ndogo kila core ina spidi ya 1.7GHz
Cortex A55 inakula umeme mdogo sana ukilinganisha na Cortex A53.
Pamoja na kutumia betri kidogo utendaji wake ni mkubwa tofauti na Cortex A53
Hizi core sita huwa zinafanya kazi ndogo ndogo.
Kwa mfano ukiwa unasikiliza radio au mziki ama kutuma meseji
Alama za Antutu na Geekbench
Antutu na geekbench ni applikesheni ambazo hupima nguvu ya processor.
Uwezo wa processor hutambuliwa kwa alama
Alama kubwa inamaanisha processor ina nguvu kubwa.
Snapdragon 695 5g kwenye alama zinafikia 692 kwa utendaji wa core moja.
Wakati alama za antutu processor inafikia 124,557
Wakati processor za Helio G96 iliyomo ndani ya Infinix note 11 pro na Snapdragon 675 iliyomo ndani ya Redmi note 10 alama zake za utendaji hazifiki 600 kwenye core moja.
Hii inamaanisha Oppo a96 5g ina utendaji wa kuweza kufungua app yoyote kwa urahisi
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya oppo a96 5g ina ukubwa wa 4500mAh aina ya Li-Po
Simu inakuja na fast chaji.
Kwani chaji ya oppo a96 5g inapeleka umeme wa wati 33
Oppo wanadai chaji hii inaweza kujaza betri kwa 100% ndani ya dakika 63
Kwa maana simu inajaa kwa lisaa.
Betri sio kubwa sana lakini linaweza kukaa na chaji muda mrefu
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya Oppo a96 ni aina ya UFS 2.2
Memori za UFS 2.2 hufanya simu kufungua app kwa haraka bila kukwama
Sifa kuu ya UFS 2.2 ni usafirishaji wa data kwa spidi kubwa
Simu ya oppo a96 5g ipo yenye ukubwa 128GB na 256GB
Huu ni ukubwa unaokuwezesha kuweka app na mafaili mengi kwenye simu
Ram yake ina ukubwa wa 8GB aina ya LPDDR4x
LPDDR4x inafanya ram kutumia umeme mdogo na kusafirisha data kwa spidi kubwa
Uimara wa bodi ya oppo a96 5g
Bodi ya oppo a96 5g imeundwa kwa plastiki
Plastiki si imara sana ukilinganisha vioo vya Gorilla
Simu ni nyembamba na nyepesi sababu ina uzito wa gramu 171
Urefu wake wa inchi 6.4 unafiti kwa asilimia kubwa kwenye kiganja
Kwa bahati hakuna viwango vinonyesha uwezo simu kuzuia maji na vumbi kupenya
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera mbili
Kamera hizo ni wide na depth
Wide(kamera kuu) ina resolution ya 48MP wakati depth 2MP
Ubora wa picha kwa vitu vilivyo kwenye mwendo unaweza usivutie.
Kwa sababu simu haijatumia teknolojia nzuri ya autofocus(kulenga) kama dual pixel pdaf
Jifunze: Vitu vya kuzingatia unapochagua simu yenye kamera nzuri
Ubora wa video
Kamera ya oppo a96 5g inarekodi video zenye ubora wa aina moja.
Video zenye ubora wa full hd(1080) ndizo zinaweza rekodiwa na hii simu.
Na spidi ya kurekodi ni ndogo ambayo ni 30fps
fps ni nini?
Unapoangalia video jua kuwa unaangalia mkusanyiko wa picha zinazoongozana
Video ni picha nyingi zilizorekodiwa mfululizo, kila picha moja huitwa frame.
Jicho la binadamu huona kitu kinachotembea pale picha 24 zinapopita ndani ya sekunde
Kitendo cha picha nyingi kupita ndani ya sekunde huitwa Frames Per Second(fps)
Kamera ya oppo a96 5g inarekodi picha 30 kwa sekunde (30fps) kwa ubora wa full hd
Ni kiwangoo cha chini.
Ubora wa Software
Oppo a96 5g ni simu ya Android 11
Simu inapewa nguvu na software ya oppo inayoitwa ColorOS 12
Imoji za coloros 12 zina kautofauti na imoji ambazo umezizoea.
Ukiwa na corolos 12 huhitaji kudownload app ya ziada kuunganisha simu na kompyuta.
Mfumo wa oppo unaruhusu kupokea simu kwa kompyuta.
Hata screenshot ya simu inaweza kupigwa na laptop
Ukiwa na Color OS unaweza kukopi maandishi kwenye simu na kuyapesti kwenye software ya kompyuta
Kufupisha, ColorOS 12 itakufanya ufurahie kutumia Oppo a96 5g kwa sababu ya utajiri wa vitu.
Bei ya oppo a96 5g Tanzania
Bei ya oppo a96 5g inaanzia shilingi za kitanzania 718,000/=
Hii ni bei ya china.
Kwa Tanzania hasa maduka ya kariakoo Oppo a96 5g inaweza fika 760,150/=
Simu mbadala za hii inaweza ikawa toleo jipya la Samsung A53.
Na Xiaomi Redmi Note 11 Pro 5g bila kuacha Vivo T1 5G
Bei ya Xiaomi Redmi Note 11 Pro 5g ni shilingi 893,007 amazon
Vivo T1 5G inafika 464,621.83
Yapi Madhaifu ya oppo a96 5g
Simu inakosa kamera ya kupiga eneo pana na kitu ambacho kipo mbali.
Kwa sababu simu haina kamera aina ya Telephoto na Ultrawide
Simu haina viwango vya IP53, IP67 na IP68 vinavyooanisha uwezo wa simu kuzuia maji
Simu ya oppo a96 inakuja na android 11 wakati simu mpya za mwaka 2022 zinakuja na Android 12
Oppo walipaswa kuwekea simu glassi za gorilla ili kuongeza uimara
Neno la Mwisho
Kama mnunuaji ni mimi ningeinunua hii simu ya oppo a96 5g.
Ina maboresho ya software ambayo hayakuwepo kwenye Oppo a96
Kwa mpenzi wa kamera hii simu sio nzuri.
Kwa sifa za kiujumla Oppo a96 5g ni simu nzuri kuwa nayo