Kuna matoleo mengi ya simu za oppo zenye ubora tofauti tofauti
Zipo ambazo zina ubora wa kati, wa juu na wa chini
Katika hizo, nyingi zinajitahidi kuwa na kamera zinazotoa picha na video nzuri ila kuna toleo kinara
Kiufupi ni kuwa Oppo yenye kamera nzuri kwa sasa ni Oppo Find X6 Pro ambayo imetoka mwaka 2023 mwezi januari
Bei yake ni kubwa na inazidi milioni, kwenye hii post utaona ubora wa picha na aina ya kamera za Oppo Find X6 Pro
Idadi na Aina ya Kamera
Upande wa nyuma find x6 pro ina kamera zipatazo tatu (macho matatu) na upande wa mbele(selfie) kuna kamera moja
Simu ina kamera aina ya periscope telephoto maalumu kwa kuchukua vitu vilivyopo umbali mrefu kidogo na kamera
Kwa mfano kitu kipo mita 20 na unataka kitokee vizuri basi kamera ya telephoto ndio hustahili kufanya kazi hiyo
Aina ya kamera iliyopo ni Ultrawide ambayo hutumika kupiga picha kwenye eneo pana
Kwa mfano upo uwanjani na unataka uwanja wote utokee kwenye picha, camera ya ultrawide itaifanya hiyo kazi
Na aina nyingine ya kamera ni kamera kuu ambayo ndio hutumika mara kwa mara, aina hii hujulikana kama wide
Kamera zote zinakuja zikiwa na megapixel 50
Ukitaka kujua kamera nzuri ya simu anagalia teknolojia zinazoambatana nazo hata kabla kuangalia muonekano wa picha wa hizo kamera
Teknolojia zilizopo kwenye kamera
Mfumo wa kamera za Oppo Find X6 Pro unakuja na vitu vingi vya uboreshaji wa kamera kati upigaji picha na kurekodi video
Hivi vinahusisha
Mult-directional PDAF, ni aina ya teknolojia inayosaidia kamera kurenga kitu moja kwa moja bila mpigaji kupoteza kukilenga anachotaka kukipiga picha
Zipo teknolojia za ulengaji nyingi ila kisasa zaidi ni hiii mult directional pdaf ambayo huchukua data nyingi ili iweze kukilenga na kukitambua kitu kinachopigwa picha
Iko fasta na inasaidia simu kupiga vizuri palipo na mwanga hafifu
Kitu kingine ni OIS, hii hutuliza kamera wakati ukirekodi video huku ukiwa unatembea
Ni kamera mbili ndizo zilizowekewa OIS kwenye hii simu
Pia kamera zake mbili zina Laser AF, inafanya kazi kama PDAF yaani kuisaidia kamera kukitambua kitu kinachopigwa picha ila laser af inatumika zaidi kwenye mwanga mdogo
Teknolojia zingine ni Dolby Vison, gyro Eis , optical zoom
Kutokana na uwepo wa hivyo vitu muhimu, oppo ina mfumo mzuri unaoweza piga picha nzuri kwenye mazingira tofauti
Ubora wa Picha Kwenye Mwanga Mwingi
Moja ya kitu ambacho hutokiona kwenye hii oppo ni noise(chenga chenga)
Kamera zinakusanya data za kutosha hivyo muonekano wa picha kiubora ni mkubwa
Tukianza na kamera kuu, inaonyesha rangi za vitu kwa usahihi wa kiwango cha juu
Hii inamaanisha kuwa kamera inaweka mlinganyo sahihi kwenye utofautishaji wa eneo lenye kivuli na lisilo na kivuli
Vitu vinaonekana kwa uhalisia hakuna kuzidisha kwa muangaza ambao unaweza mfanya mtu kuonekana kwa kung’aa sana
Ukiizoom picha hii bado ubora wa muonekano wa picha haupungui
Ubora wa picha wa kamera ya Ultrawide na Telephoto
Kwenye mwanga mwingi bado hizi kamera zinatoa picha nzuri
Rangi za vitu zina usahihi na “dynamic range” inafanya kazi vizuri
Kwa maana balansi ya mwanga na vivuli kamera inafanya kwa usahihi
Mwanga mwingi hauthiri eneo lenye kivuli kidogo
Ukitazama muonekano wa anga uhalisia ni wa kiwango cha juu kwenye mawingu meupe yanaonekana kama yalivyo
Ukiizoom hii picha unaweza usione kiwango cha noise kwa sababu kamera ina uwezo wa kukusanya data za kutosha
Upande wa ubora wa picha kwenye telephoto pia utendaji ni kuridhisha
Kumbuka kuwa telephoto ni maalumu kwa ajili ya kupiga kitu ambacho kipo mbali
Kwenye simu nyingi ambazo hazina hii kamera ubora wa picha unapungua ukiizoom kamera ili upige hiko kitu
Ila kwenye oppo ubora unabaki palepale hasa ukikuza mara tatu
Kama unavyoweza kuona kuwa hakuna upotevu wa pixel kama ilivyo kwenye digital zoom
Usahihi wa rangi za vitu ni wa kiwango cha kuridhisha
Na ukiikuza picha zaidi bado vitu vinaonekana na kiwango cha noise ni kidogo vilevile
Ubora wa Picha kwenye mwanga hafifu
Kwenye mwanga hafifu ndio eneo la muhimu zaidi kujua ubora wa kamera za simu
Simu zenye kamera nzuri zinapiga picha zinazoonyesha vitu kwa ustadi mkubwa kwenye mwanga mdogo
Utendaji wa kamera za oppo zote tatu ni mzuri
Kiwango cha chengachenga(noise) ni kidogo na kama una jicho la haraka unaweza usigundue
Chukulia mfano wa hii picha.
Kwenye eneo la kuria upande wa mti kuna mwanga mdogo sana lakini unaweza ukaona rangi ya majani ya mti
Utofautisha wa vivuli na mwangaza umejitahidi kwa kiasi kikubwa
Ukizoom eneo gorofa vitu vinaonekana japo kiwango noise unaweza ukakiona
Kamera za hii simu zinajitahidi nyakati za usiku kwa sababu ya uwepo Laser AF inayosaidia simu kurenga vizuri hata palipo na kiwango cha chini cha mwanga
Ubora wa selfie kamera
Kwa mpenzi wa kujipiga picha kamera ya mbele ni kipaumbele kikubwa sana kuliko hata kamera za nyuma
Kamera ya selfie ya oppo find x6 pro haina mambo mengi sana kama ilivyo kwa selfie ya iphone 14 pro max
Hivyo ubora wake ni wa kawaida ila bado kiwango cha picha ni kizuri tena inaizidi Tecno Spark 10 Pro
Kama uonavyo ni kuwa picha imechukuliwa kwenye mwanga mdogo
Ubora wa picha ni mzuri na pia kuna kiwango cha chenga chenga kwa mbali hasa kwa vitu ambavyo vipo mbalimbali
Hivyo kamera inajikita zaidi kupiga picha uso ukiwa karibu sana
Ubora video
Kamera za Oppo Find X6 Pro zinaweza kurekodi mpaka video za 4K
Na zina teknolojia ya utulizaji wa kamera pindi ukirekodi huku ukiwa unatembea
Teknolojia hufahamika gyro-EIS
Ni kweli inatuliza ila mitikisiko ipo kwa kiasi fulani bado anayerokidi atalazimika kutuliza mkono pindi akiwa anatembea
Video ya 4K inarekodi video ya ubora sana nyakati zenye mwanga wa kutosha
Nyakati za usiku noise(chengachenga) kwa mbali zinaweza kuonekana
Tazama hii screenshot toka kwenye video ya 4k kwa kiwango cha 30fps
Hata hivyo kamera inajitahidi kuonyesha rangi za vitu na kiza hakijaathiri muonekano wa sehemu zenye mwanga mwingi
Kila kitu kinaweza kuonekana kama kinavyoonekana kwenye mazingira halisi
Kamera za Ultrawide na Telephoto pia utendaji wake ni wa kiwango kizuri unaporekodi video
Ila kamera ya ultrawide haina OIS (Optical Image Stabilization) na hivyo basi kuliza mkono unaporekodi video kwa kutembea kunahitajika
Bei ya Oppo Find X6 Pro
Kama ilvyo ada simu yoyote yenye kamera kali sana bei yake huwa ni kubwa vilevile
Hivyo basi bei ya oppo find x6 pro ni zaidi ya shilingi milioni mbili za Tanzania
Kwa sasa hii simu inapatikana ndani ya mipaka ya china tu
Ila unaweza ukaagizia na ikakufikia ulipo
Hitimisho
Opoo Find X6 Pro ni moja ya simu bora kabisa duniani kwa sasa zinazoongoza kuwa na kamera nzuri
Inakupa uwezi wa kurekodi na kupiga picha vizuri iwe usiku ama mchana
Mfumo wake wa kamera unasaidia kutoa picha zenye ubora mzuri
Kwa mtu mwenye bajeti ya kutosha anaweza akaimiliki hii simu
Kumbuka ubora wake haupo kwenye kamera pekee yake na kwenye mambo mengine pia.
Maoni 4 kuhusu “Oppo Yenye Kamera Nzuri na Ubora wa Picha”
tangu nifatilie simunzuri nimejifuza mambo mengi sana kuhusu simu ipi bora ipi ina mapugufu
Akika hii ni simu bora sana ya oppo
Kabisa kabisa
Bei ya oppo find x6 pro ni sh ngapi za kitanzania.