Kama umekuwa ukijiuliza 5G ni nini na maana yake ni ipi
Basi jibu lake ni hili hapa chini
5G ni teknolojia ya kizazi cha tano cha network za simu za mkononi ambayo kasi yake ni kubwa kuliko aina za network za simu za mkononi zilizowahi kutangulia
Utendaji wa 5G umejikita kwenye kasi kubwa sana na kutumia muda mchache kwenye mwitikio wa data (Low Latency) kati ya vifaa mbalimbali
Kikawaida kiwango cha chini cha spidi ya mtandao huu inaanzia 50Mbps
Kuna aina tatu za 5G ambazo zinatofautiana kasi
Kwenye posti hii utafahamu mambo ya msingi yote yanayohusiana na 5G ikiwemo mwanzilishi wake
Nani mwanzilishi wa 5G?
Hakuna taasisi, wala mtu au kampuni moja ambayo imetengeneza 5G
Bali 5G imeundwa kwa ushirikiano wa makampuni ya mabara yote duniani
Umoja ambao umekutanisha hayo makampuni ni 3GPP
Kirefu cha 3GPP ni Third Generation Patnership Project
Kwenye 3GPP kuna kampuni kama Qualcomm, Nokia, Huawei, Samsung, Cisco, Ericson, AT&T, TTC na mengineyo mengi
Kiufupi 3GPP ina wanachama wanaofikia 700 kwa mwaka 2022
Hii ndio jumuiya inayoseti vigezo (standards) vya network kuwa 5G
Aina za 5G
Kuna aina tatu za mtandao wa 5G
Si kila 5G ina kasi kubwa, bali kuna aina nyingine haina tofauti na 4G linapokuja swala la kasi
Kwani kasi za 5G zinatofautiana kulingana na aina ya masafa
Hizi ndizo aina zake
- Masafa mafupi (Low Band)
- Masafa ya kati (Mid Band)
- Masafa marefu (High Band au mmWave)
5G ya Low Band masafa yake yanaanzia 600 MHz mpaka 900 MHz
Spidi yake haitofautiani sana na mtandao wa 4G
Kwani inaweza kusafirisha kwa kasi inayoanzia 30Mbps mpaka 250Mbps
Nchi nyingi duniani zinatumia 5G ya Masafa ya Kati (Mid Band 5g) pia inafahamika kama sub-6
Masafa ya mid band yanaanzia 1.7GHz mpaka 4.7 GHz na spidi ipo kati ya 100Mbps mpaka 900Mbps
Na masafa marefu yanaanzia 24 GHz mpaka 40 GHz
Haya ni masafa yanayoweza kusafirisha data kwa kasi kubwa inayofika 1Gbps
Pia hufahamika kama mmWave (milimetre Wave)
Changamoto za 5G
Mawimbi ya High Band (Masafa marefu) huwa yanapata shida kupenya kwenye ukuta na wakati wa mvua
Hivyo ukiwa unatumia intaneti ndani ya nyumba spidi inapungua
Mawimbi yake pia hupatikana eneo dogo
Hivyo inalazimisha kampuni za simu kuweka minara mingi ili network ipatikane
Minara mingi inaongeza gharama kitu kinachofanya intaneti yake kuwa sio rafiki kutokna na bei kubwa
Ndio maana nchi nyingi za Afrika hazijaweka huu mtandao
Gharama kubwa zinalazimisha wauzaji wa huduma za intaneti kujikita mijini kuliko vijijini
Vifaa vingi vya 4G hasa smartphone vinauzwa kwa bei ya juu
Utofauti wa 5G na 4G
Utofauti wa 4G na 5G ni spidi tu
Japokuwa 5G inaweza ikatumia miundo mbinu ya 4G kusafirisha data
Aina hii ya muundo hufahamika kama NSA (Non Stand Alone)
Kikubwa ni kuwa 5G inaanzia 50Mbps wakati 4G inaanzia 18Mbps
Lakini kuna ufanano kwa sababu 4G pia inatumia masafa ya mafupi na ya kati
Simu za 5G
Baadhi ya simu za daraja la kati huwekewa uwezo wa kutumia 5G ya low band na mid band
Mfano wa simu hizo ni Vivo T1, Infinix Zero 5G, Redmi Note 10 5G, Samsung Galaxy A73 5G, Oppo A96 5G nk
Lakini bei ya hizi simu ni zaidi ya laki tatu na nusu
Pia simu zote za daraja juu lazima iwe na uwezo wa network ya 5G
Mfano wa hizo simu ni Samsung Galaxy S21 Ultra 5G, iPhone 13 Pro Max, Xiaomi 12 Pro, Oppo Find x3 Pro, Sony Xperia Pro-I, Vivo X70 Pro na nyingenezo nyingi
Ili utumie 5G unahitaji simu yenye uwezo huo ikiwemo na laini ya 5G
Kama sehemu haina mtandao huo basi hautoweza kupata kasi yake kubwa
Mitandao yenye 5G Tanzania
Mwaka 2020 Vodacom Tanzania ilianza mipango ya kuweka 5G wakati wa maazimisho ya miaka 20 tangu wameanza biashara Tanzania
Lakini hakuna taarifa zozote mpya
Kiufupi, hakuna mtandao wa simu ambao umewekeza kwenye hii teknolojia mpya ya mawasiliano
Lakini matumaoni yapo
Kwani mkutano uliandaliwa na ubalozi wa marekani chini ya udhamini wa United States Telecommunications Training Institute (USTTI) na Wizara ya Teknolojia ya habari na mawasiliano waligusia suala hilo
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya ubalozi wa Marekani ambayo imechapishwa Mei 9, 2022
Ipitia hapa kuisoma yote, Mkutano wa ubalozi wa USA na Wizara ya tehama Tanzania
Update septemba 2022
Vodacom imekuwa kampuni ya kwanza Taznania kuzindua mtandao wa 5G
Aina ya 5G ambayo vodacom inatumia ni Non Stand Alone
Kwa maana 5G yake itakuwa inatumia miundo mbinu ya 4G
Jifunze zaidi hapa: Vodacom na uzinduzi wa 5G Tanzania
Kwa nini simu za 5G zina bei kubwa
5G inahusisha mtandao ambao una kasi kubwa ya kusafirisha data
Kitu kinachoifanya simu iwe na processor yenye utendaji mkubwa
Chip zenye nguvu kubwa huwa na teknolojia bora ambayo inatumia pesa nyingi
Mwisho wa siku gharama za simu zinakuwa juu
5G na Ugonjwa wa Uviko (Covid)
Mtandao wa 5G ulikutana na changamoto ya kuhusishwa na kusambaa kwa kirusi cha corona
Corona ni kirusi ambacho kinasababisha uviko
Haya madai yaliegemea kwenye dhana za kufikirika zaidi kuliko taifiti za kisayansi
Kiuhalisia ni mawazo ambayo hayana mantiki
5G ya masafa ya chini na ya kati yanatumia miundo mbinu ya 4G
4G pia inatumia baadhi masafa yanayotumika na 5G
Sasa kwan nini covid haikusambazwa na 4G ije isambae leo hii