Kama wewe ni mtu wa kusoma mabox ya TV utakuwa umeshwawahi kuona neno limeandikwa 4K
Hivyo utakuwa unajiuliza hasa nini maana ya 4k
4K ni aina ya ni aina ya resolution ambayo yenye idadi ya pixels zaidi ya milioni nane
Kwa maana inakuwa na idadi ya pixels 3800 kutoka kushoto kwenda kulia
Na pixels 2600 kutoka juu kwenda chini
Nini maana ya Pixels
Pixel ni nukta ndogo ambayo huwa na mchanganyiko wa rangi msingi tatu
Rangi hizo ni nyekundu, kijani na bluu
Mchanganyiko wa rangi wa hizo nukta ndio unatengeneza picha na video ambazo unaziona kwenye screen ya TV, Projector au Simu
Hizi nukta zikiwa nyingi ndivyo ubora wa muonekano wa picha au video unakuwa mzuri
4K kwenye kamera za simu
4K kwenye simu hutumika na kamera kurekodi video
Simu nyingi zina resolution za aina mbili tu
Huwa hazina screen za 4K kwa sababu kwenye haina umuhimu sana kutokana na udogo wa smartphone
Kwa hiyo simu hurekodi video hizo kwa ajili ya kutazama kwenye TV
Simu nyingi za madaraja ya kati na ya juu zinaweza kurekodi video za 4K kwa kasi ya 30fps, 60fps na hata 120fps
Kwa nini simu za bei rahizi hazirekodi 4k?
Kwanza unaporekodi video za 4K processor ya simu huwa inatumia nguvu kuchakata data za video
Kwa sababu inafanya mahesabu ya uchanganyaji wa rangi wa pixels zaidi ya milioni nane
Hivyo simu inahitajika kutumia chip yenye nguvu kubwa
Kwa bahati mbaya simu za bei rahisi huundwa na kamera zenye ubora haififu
Na pia zinatengenezwa na processor ambazo zina utendaji wa chini
Hivyo mwisho wa siku kamera za simu zinashindwa kabisa kurekodi video za 4K
Je video ya 4K inachukua nafasi kubwa?
Jibu la haraka haraka ni ndio
Kadri video inapojuwa na resolution ndivyo inavyochukuwa nafasi kubwa ya memori
Hii inatokana na resolution kubwa na pixels nyingi
Kwa maana nafasi kwenye kamera ya kawaida ni ndogo
Wakati ukirekodi kwa 4K inaweza kuchukua nafasi mara mbili zaidi
Tena memori inayochukuliwa inakuwa kubwa kama 4K inarekodiwa kwa frames zaidi ya 60 fps kama 120 fps
Je 4K ni bora kuliko Full HD na HD?
Jibu la kiujumla 4K ni bora kuliko aina zingine za video ikiwemo full hd
Lakini hii inategemea na vitu vingine vya zaidi
Iwapo kamera inayorekodi kwa full hd inaweza kurekodi ikiwa inatumia HDR10+
Basi hiyo kamera ya simu itatoa video yenye ubora wa juu kuliko kamera ya 4K ambayo haina HDR10+
Jina lingine la 4K
4K pia hufahamika kama Ultra HD (UHD) pia inafupishwa Ultra
Kwa hiyo ukiona neno UHD basi jua kuwa ni kitu kimoja na 4K
Simu zenye kamera za 4K
Hizi ni baadhi ya simu kutoka makampuni mbalimbali ambazo zimewezeshwa kamera zinazoweza kurekodi video za 4K (UHD)
Samsung Galaxy S21 Ultra
Simu ya samsung galaxy s21 ultra ina jumla ya kamera tatu
Kamera kuu zake zinaweza kupiga video za aina zote ikiwemo 8K na 4K pia
Pia kamera ya selfie ya samsung galaxy s21 inaweza kurekodi video za 4K vilevile
iPhone 13 Pro Max
iPhone 13 pro max ni simu ambayo ina kamera tatu kama ilivyo kwa galaxy s21 ultra
Kamera zake na zenyewe zinaweza kurekodi video za 8K na 4k
Pia selfie kamera na yenyewe inaweza kurekodi video za 4K vilevile
Redmi Note 10
Hii ni simu ya kamera nne
Inaweza kurekodi video za 4K kwa spidi ya 30fps
Ila selfie kamera haina uwezo kutoa video ya 4K
Oppo Find X3 Pro
Kamera za oppo find x3 pro zinarekodi video za ubora wa 4K kwa kasi inayofikia 60 fps
Kwa bahati mbaya kamera yake ya selfie zinarekodi video za full hd pekee
Tecno Camon 18 Premier
Hii pia ni simu yenye kamera ya 4K inayoweza kurekodi kwa kasi ya 30 fps
Ila selfie inarekodi video za 1080p pekee
Simu zingine za 4K ni Infinix Zero X Pro, Vivo X80 Pro, Xiaomi 12 Pro, OnePlus 10 Pro, Realme GT2 Pro
Maoni 5 kuhusu “Maana ya 4K [Upande wa kamera ya simu].”
Je camon 19 pro
Ni simu nzuri kiasi chake Ila hairekodi video za 4k
Tecno Sipak 10
Hairekodi video za 4k
Simu yangu ni finix hot12 camera yake inageuza picha kama unapinga mtu miguu inakuwa juu kichwa chini je nifanyeje ikae sawa msaada