4G ni aina ya mtandao wa simu za mkononi wenye spidi inayoanzia 10Mbps na inayoweza kufika mpaka 100Mbps
Lakini inapendekezwa zaidi spidi inayoanzia 18Mbps
Kirefu cha 4G ni fourth generation
Kwa maana ni kizazi cha nne cha mtandao wa simu
Kwenye posti hii utafahamu masafa ya 4G ya Tanzania na Maeneo yote ambayo 4G inapatikana hapa nchini
Tuchimbe kiundani.
Aina ya 4G
Kuna aina mbili za mtandao wa 4G
Aina zake zinatofautiana na taasisi ambayo imeweka vigezo vya mtandao kuitwa 4G
Aina hizo ni
- LTE (Long Term Evolution)
- WiMax ( Worldwide Interoperability for Microwave Accesses)
Lakini LTE ndio inayotumika kwa sehemu kubwa duniani ikiwemo hapa Tanzania
Hivyo tutaangazia zaidi LTE
Ndio maana baadhi ya simu zikiwa zinatumia 4G zinaandika LTE, ni kitu kimoja
Long Term Evolution zinatofautiana spidi
Kuna LTE ya kawaida ambayo spidi yale ya juu kabisa ya kusafirisha data inafika 100Mbps
Halafu kuna LTE Advance ambayo spidi yake ya kusafirisha data inafika 1Gbps kwenye kudownload
Kwa maana kama kuna miundombinu ya minara yenye kasi kubwa basi faili la ukubwa 1GB litamalizika kudownload baada ya sekunde nane tu
Sifa za mtandao wa 4G
Mtandao wa 4G huwa na masafa mengi yanayotofautiana kutoka nchi moja na nyingi
Hivyo kifaa chenye aina hii mtandao kinaweza kikatumika nchi moja lakini ikashindikana kutumika kwenye nchi nyingine
Kasi ya 4G huzidi 42Mbps na inaweza kufika mpaka 1Gbps
Kama unatest kasi ya mtandao unaotumia na ukapata chini ya 18Mbps maana yake wewe upo kwenye 3G aina ya HSPA
Tofauti ya 4G na GPRS, EDGE, H na H+
Kabla ya 4G kuna watangulizi wake ambao 3G na 2G
3G (third Generation) imegawanyika kati sehemu nyingi zinazotofautiana kasi
Aina za 3G ni kama zifuatazo
- WCDMA ambayo spidi yake ya kudownload inafika
- UMTS yenye spidi inayoweza kufika 2Mbps
- HSDPA ambayo spidi yake inafika 14.4Mbps
- HSPA (H) yenye kasi ya 14.4Mbps
- HSPA+ (H+) ambayo kasi yake ya juu inafika 28Mbps
Wakati mtandao wa Edge (E) spidi yake ya juu kupakua vitu inafika 473Kbps
Na upande wa mtandao wa GPRS (G) spidi yake ni ndogo zaidi ya edge
Hivyo utofauti mkubwa wa 4G na watangulizi wake ni kasi
Ukiwa na edge na gprs simu inashindwa kufungua hata picha za Whatsapp
Masafa ya 4G Tanzania
Kwa sasa mitandao yote ya Tanzania inakubali network ya 4G
Masafa yanatofautiana kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine
Ni vizuri ukayafahamu masafa yote ili uweze kujua kama kifaa unachotumia kinaweza kukubali intaneti ya 4G nchini
Vodacom – 1800 MHz (B3 au 3)
Tigo – 800 MHz (B20 au 20) na 1800 MHz (B3 au 3)
Airtel – 700 (B28 au 28) MHz na 2100 MHz (B1 au 1)
Halotel – 2600 MHz (B7 au 7)
TTCL – 1800 MHz (B3 au 3) na 2300 MHz (B40 au 40)
Smile – 800 MHz (B20 au 20)
Zantel – 1800 MHz (B3 au 3)
Maeneo ya 4G Tanzania
Maeneo mengi ya mijini yana network ya 4G hapa Tanzania
Ila sehemu kubwa ya nchi hasa vijijini 4G haijafika
Kwa bahati mbaya maeneo mengine yanakosa mpaka 3G
Kama una simu ya ya 4G lakini eneo unaloishi halina, basi hutoweza kutumia network hiyo ya kasi zaidi hapa nchini kwetu
Baadhi ya Simu za 4G
Siku hizi kila simu inawezeshwa aina hii ya network
Ni simu chache ambazo hazina 4G
Mara nyingi ni simu chache za daraja la chini ndizo unaweza kutokuta lte
Wazo moja kuhusu “Maana ya 4G na aina zake”
Thanks