Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple
Tukio hili litarushwa moja kwa moja kupitia youtube
Kwa wafuatiliaji watakuwa wanafahamu kuwa apple mpya mpaka sasa ni matoleo ya iPhone 14
iPhone 14 yalitoka mwaka 2023
Hivyo basi mwaka 2023 kutakuwa kuna uzinduzi toleo jipya kabisa la iphone
Bidhaa zitakazoingia sokoni
Kwenye uzunduzi, kampuni ya apple itatangaza matoleo ya manne ya iphone, saa janja na pia tetesi zinasema kutakuwa na uzinduzi wa ipods.
Kwa hapa tutaangazia simu tu zitakazoingia sokoni
iPhone 15
iPhone 15 ndio simu ambayo itakuwa na bei ya chini zaidi kati ya simu zingine nne
Bei tarajiwa ya iphone 15 ni zaidi ya milioni mbili
Ni simu ambayo kimo chake itakuwa na urefu inchi zisizozidi 6.1
Ukubwa wa memori wa iphone 15 unatarajiwa kuanza 128GB hadi kiwango cha 512GB
Kwenye ram simu hii itakuwa na ukubwa wa RAM ya GB 6
iPhone 15 itatumia chip iliyotumika kwenye iPhone 14 ambayo ni Apple A16 Bionic
Kwenye kamera ya mbele kuna dynamic island
iPhone 15 Plus
Urefu wa iPhone 15 Plus unatarajiwa kuwa ni inchi 6.7
Na yenyewe RAM itakuwa na ukubwa wa GB 6
Ukubwa wa memori unaanzia GB 128 hadi GB 512
Inakadiriwa kuwa bei ya iphone 15 plus ya GB 512 itakuwa ni shilingi milioni mbili na laki nne
Pia simu itatumia processor ya mwaka 2022 ya Apple A16 Bioni
Apple hawajaweka processor mpya kwenye simu za iphone 15 na iphone 15 plus
iPhone 15 Pro
iPhone 14 Pro bei yake inatarajiwa kuanza kwa kiasi cha shilingi 2,800,000 kwa bei ya dunia
Kwa hapa Tanzania bei inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo
Kwenye memori simu inatarajiwa kuanza na ukubwa wa gb 128 hadi ukubwa wa 2TB
Zinatoa nafasi kubwa ya kuhifadhi vitu vingi bila kuwaza kuwa simu inaweza kujaa haraka
Ukubwa wa RAM pia unatarajiwa kuwa ni GB 6
iPhone 14 Pro itatumia processor mpya yenye nguvu zaidi ya Apple A17 Bionic
iPhone 15 Pro Max
Hili ndio litakuwa toleo la gharama zaidi na lenye betri kubwa
Kwa maana ndio itakuwa na uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu kuliko matoleo mengine
Ukubwa wa memori wa iPhone 15 Pro Max unaanzia GB 128 hadi TB 2
Ram na yenyewe itakuwa ni GB 6
Simu itatumia processor yenye nguvu kubwa ya Apple A17 Bionic
Kwa wapenda simu zenye nguvu zisizo kwama kwama hata kwa mazingira gani iphone 15 pro max ndio inafaa
Kisanga kinaanza kwenye bei
Bei ya iphone 15 pro max inatarajiwa kuanzia shilingi milioni 3.3
Bei kubwa inatokana na sifa kubwa simu inatarajiwa kuwa nazo
Vitu Vipya vinavyotarajiwa
Kwa mara ya kwanza simu za iPhone zinatarajiwa kutumia waya wa kuchaji aina ya USB Type C
USB Type C ni zile waya zenye vichwa vipana
Apple kwa miaka mingi wamekuwa wakitumia aina tofauti kabisa ya chaji
Chaji zao iphone zinatambulika kama Lightning Port
Kutokana na sheria za Umoja wa ulaya kuzitaka kampuni za simu ziwe na muundo mmoja wa chaji, apple inaonekana watafuata mapendekezo ya hiyo sheria
Kitu kingine kipya ni kuwekwa kwa fremu za Titanium upande wa pembeni
Matoleo yaliyopita fremu ilikuwa ni stainless steel(chuma)
Titanium huwa ni ngumu hivyo uimara wa simu utakuwa mkubwa
Kitu kingine ni kuwa hizi simu zinatarajiwa kutumia kioo cha LIPO Display
Faida ya hii kioo ni kuwa inawezesha kioo kuchukua sehemu kubwa ya skrini na matumizi ya umeme ni madogo
Hitimisho
Kuna mabadiliko yapo ila sio makubwa ya kutofautisha na matoleo ya iPhone 14 Pro
Na pia apple inaungana na simu nyingi za android kwenye matumizi ya USB Type C
Unahitaji kuwa na bajeti ya kutosheleza kumiliki toleo lolote la iphone mpya
Maoni 2 kuhusu “Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023”
Leteni na za mtumba(used)
Nimeipenda