Kampuni ya Apple imeingiza matoleo mapya ya iphone
Moja ya iPhone hiyo ni iPhone 16 Pro, ina ufafanano kwa sehemu ya kimuundo na iPhone 15 Pro
Yapo mazuri lakini yapo yatakayofanya ujiulize maswali.
Hata bei ya iPhone 16 Pro ni milioni mbili na laki tisa kwa bei rasmi ya Apple
Ila kwa hapa Tanzania bei yake inaanzia milioni 3.5 ya GB 256
Ukifuatilia sifa zote zilizopo hapa utaweza kugundua kama inakufaa ama unasubiria toleo lijalo
Sifa za iPhone 16 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB, 1TB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.3inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,500,000/= |
Uwezo wa network
Kwa matoleo ya Marekani simu inakuja bila kuwa na sehemu ya kuweka laini yaani SIM CARD
Mnunuaji lazima awe anatumia laini za eSIM
eSIM ni laini zinakuwa ndani ya simu na hazihitaji laini ya plastiki
Ni simu ya 5G za aina zote ikiwemo ile yenye kasi sana za mmWave
Pia kasi yake ya 4G inafika spidi ya 10000Mbps kupakua mafaili
Hata hivyo spidi lazima uwe kwenye mazingira yanayosapiti kasi ambapo kwa Tanzania ni ngumu kwa sasa
Ubora wa kioo
Kioo cha iPhone 16 Pro ni cha LTPO OLED
Apple wanakiita LTPO Super Retina XDR OLED
Hiki kioo bwana kina HDR10, Dolby Vison na uwangavu unaofika nits 1000
Hivi vinavyafanya skrini kuwa na kina kikubwa cha rangi hivyo vitu vingi vinaonekana kwa ustadi hata juani
Na kiwango cha resolution ni 1206 x 2622 pixels
Resolution kubwa ya kuonyesha vitu vizuri
Nguvu ya processor ya Apple A18 Pro
Upande wa utendaji umewepewa maboresho makubwa kwa karibu simu zote za iphone mpya
Kama ninavyosema mara, chip za apple huwa na nguvu sana
Na ukiwa na chip nzuri na yenye nguvu, vitu vingine vitakuwa na ufanisi mzuri
Iko hivi, . .
Apple A18 Pro ina alama zaidi ya 3000 kwenye app za kupima nguvu ya processor ya Geekbench
Pia chip ina ufanisi mzuri wa matumizi ya betri ukilinganisha na iphone 15 pro
Hivyo utaweza kucheza magemu yenye nguvu kama Call of duty Mobile season 8 kwa muda mrefu na bila kukwama kwama
Uwezo wa betri na chaji
Ukinunua kwa mara ya kwanza simu haiji na chaji
Ila ina uwezo wa kupeleka umeme wa wati 25 kwa njia ya waya
Haichukui muda mrefu sana kujaa ijapokuwa simu nyingi siku hizi zinakuwa na chaji kubwa zaidi ya hii (wati 30 na kuendelea)
Kwenye matumizi mbalimbali ya mara kwa mara simu inadumu kwa takribani masaa 11
Hii inamaanisha ukiwa unamatumizi ya kawaida utadumu na chaji muda mrefu
Hata Samsung Galaxy S24 Ultra inaizidi hii simu kwa mbali tu
Ukubwa na aina ya memori
Hii simu ina matoleo manne upande wa memori na zote zina RAM ya GB 8
Unaweza ukapata ya GB 128, 256, 512 au 1TB
Na bei zinatofautiana kulingana na ukubwa wa memori
Mfumo wa memori wa simu za iphone huwa ni NVMe
Hii huwa ina kasi kubwa ya usafirishaji wa data
NVMe ndio protoko inayotumika na kompyuta matoleo ya kisasa
Uimara wa bodi
iPhone 16 Pro ina bodi imara na ina waterproof ya IP68
Inaweza kustahimili ndani ya maji ya kina cha mita 6 kwa muda wa nusu saa
Bodi yake kiujumla imeundwa kwa madini ya titanium
Kwa siku za mbeleni utakuja kujua uiamara wa titanium kiundani
Kwa sasa ni ngumu kusemea uimara wake
Kwenye skrini simu imewekewa protekta ya seramiki
Ubora wa kamera
Kwanza kabisa simu ina kamera zipatazo tatu
Kamera za wide na ultrawide zina ukubwa wa megapixel 48
Na zote zinatumia ulengaji wa dual pixel pdaf
Ubora wa picha wa hii simu ni mzuri kwa nyakati zote
Texture, usahihi wa rangi na muonekano wa vitu kwa uhalisia ni wa kiwango kikubwa
Maboresho makubwa yapo katika uchukuaji wa video
Kwa mara ya kwa iPhone inaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 120fps
Wakati wa kurekodi video iphone inakupa uwezo kuifanya video itoe sauti za wale wanaorekodiwa kama wakiwa wanaongea
Kama kuna mtu wa pembeni alikuwa anaongea sauti yake haitosikika
Ubora wa Software
Ubora mkubwa kama apple wanavyopromoti ni hiki kitu kinaitwa Apple Intelligence
Kabla ya kuangalia Apple Intellignce, simu zote za iphone 16 zinakuja na mfumo endeshi wa iOS 18
Apple Intelligence itaanza kupatikana baadae kidogo
Ila vitu ambavyo vipo vingi tayari vipo kwenye simu za samsung na google pixel
Baadhi ni uwezo wa kuondoa kitu kilichotokea kwenye kamera ambacho wewe hukihitaji
Pia kuna uwepo wa Chatgpt
Na pia kuna uwepo wa mfumo unaofanana kama na google lens
Yaani unapata taarifa za kitu kwa kukipiga picha
Washindani wa iPhone 16 Pro
Mshindani wa kwanza iPhone 16 Pro ni simu za iPhone 15 Pro
Kuna mabadiliko madogo sana baina ya hizi simu
iPhone mpya bei yake ni kubwa wakati huo iphone 15 bei zake zimeanza kushuka
Hivyo mtu anaweza kununua iphone ya zamani kuliko hizo mpya
Na pia watumiaji wa iphone 15 pro wanaweza wasishawishike kununua hii simu
Kuna taarifa mauzo ya awali ya simu matoleo ya iPhone 16 yamekuwa madogo kuliko ilivyotarajiwa
Unaweza pitia hapa: Mauzo madogo ya iphone 16 Pro
Mbali na hao, mshindani mkubwa wa iPhone ni Samsung Galaxy S24 Ultra
Kwenye samsung kuna matumizi makubwa ya AI kuliko hata iphone
Neno la Mwisho
Kiujumla toleo jipya la iphone kwa mwaka 2024 yalipaswa kuja na mambo mengi na maboresho makubwa
Kwa sababu bei ya iphone 16 pro ni kubwa lakini wakati huo kuna vitu kama hdr10 ni ya standard
wakati kuna simu chini ya hiyyo bei unakuta ina kioo cha hdr10+
Hata hivyo hii ni simu nzuri kwa mwaka 2024 na mwaka ujao 2025