eSIM ni aina ya laini ambayo inakuwa ndani ya simu huku ikifanya kazi bila kuwa na laini zilizozoeleka za muundo wa plastiki (PVC)
Kifaa cha mwanzo kuwa na eSIM ni saa ya Samsung Gear S2 Classic 3G mwaka 2016 kabla ya makampuni mengine kuanza kutumia
Umaarufu wa huu muundo umekuwa mkubwa hasa baada ya kampuni ya Apple kuzindua iphone 14 ambazo hazina sehemu ya kuweka laini nchini Marekani.
Umuhimu wake mkubwa hutohutaji kutembea ni kibati cha laini ama kuwa na wasi wa sim card yako kupotea
eSIM inaweza kuhifadhi namba mpaka nane ila zinazotumika huwa ni mbili
Kuna simu nyingi zenye teknolojia hii hivyo jifunze jinsi ya kutazama kama simu yako inasapoti eSIM
eSIM nchini Tanzania
Teknoljia hii inategemea kama mtandao wa simu una mfumo unaokubali kutumia eSIM
Kwa Tanzania kuna kampuni moja mpaka kufika leo april 2023 inayosopati embeded SIM(eSIM)
Kampuni hiyo ni Airtel
Kama ni mteja wa Airtel unaweza kutembelea ofisi zao na kisha wakakupa utaratibu wa kupata huduma hii
Ila usiende kabla ya kuangalia iwapo simu unayotumia inasapoti eSIM
Jinsi ya kutazama eSIM kwenye simu
Kuna njia chache ya kujua kama simu inaweza kutumia aina hii ya laini
Njia ya kwanza ni kwa kupiga namba *#06#
Baada ya kupiga utaona namba nyingi zenye lebo za IMEI, ICCID na EID
EID ni kitambulisho kuwa simu inayo eSIM
Kirefu chake eSIM ID, kama kifaa chako haina hii basi jua kuwa huwezi tumia muundo huu wa laini
Njia ya pili ni kwenda kwenye settings kisha kwenye sehemu ya search andika “IMEI”
Bonyeza sehemu ya imei itakuja sehemu inayoonyesha taarifa za imei zilizopo kwenye simu yako
Moja ya taarifa ya imei inayotakiwa kuwepo ni ya eSIM tofauti na hapo kifaa chako hakina muundo huu
Jinsi ya kuwezesha eSIM
Iwapo umegundua kuwa simu yako inayo, hizi ni hatua unazopaswa kufuata
Kitu cha kwanza lazima upate code kutoka kwenye kampuni ya simu unayotumia
Mara nyingi hizi huwa zipo kwenye muundo wa QR Code
Kisha washa simu yako (kwa upande wa android samsung)
Ingia kwenye Settings na chagua Connection halafu chagua SIM Card Manager
Itatokea orodha ya laini zilizopo kwenye simu ikiwamo eSIM
Kwa chini utaona pameandikwa Add mobile plan bonyeza hiyo sehemu
Simu ita-load ikicheki kama kuna simu kadi baada ya muda itakuja kitufe kinachosema “scan carrier qr code”
Inabidi uichague hiyo sehemu na kisha uanze ku-scan qr code ambayo umepewa na mtandao husika
Kisha kitakuja kitufe kikisema “add and use it now” chagua na hapo utakuwa umeiwezesha simu yako na eSIM
Kwa upande wa iPhone kuna hatua chache.
Nenda kwenye settings halafu data plan kisha chagua add data plan
Baada ya hapo itakuja screen ya kuscan qr code halafu utaendelea na hatua zingine
Simu zenye uwezo wa eSIM
Iwapo umeshafamu kuwa simu yako haina kabisa eSIM hizi ni baadhi ya simu janya unazoweza kuwa nazo
- Google Pixel 3
- iPhone XR
- Samsung Galaxy S20 Ultra
- iPhone 13 Pro Max
- Google Pixel 4
- iPhone 14
- iPhone 14 Pro
- iPhone 14 Pro Max
- Samsung Galaxy S21 Ultra
- Samsung Galaxy S21
- Samsung Galaxy S23 Ultra
- Samsung Galaxy S23 Plus
- Google Pixel 3a
- Google Pixel 4 XL
- Xiaomi 12T Pro
- Google Pixel 6
- Samsung S20 Plus
Yapo matoleo mengi kikubwa ni kuicheki kwa kufuata hatua zilizoelezewa hapa
Jinsi eSIM inavyofanya kazi
Embed Subscriber Identity Module yaani eSIM inakuwa ndani ya simu kama “chip”
Jina la hiyo chip huitwa eUICC inakuwepo ndani ya simu milele na haiwezi kutolewa
Chip ya eUICC inawekewa programu kiwandani programu itakoyoweza kusoma taarifa zinazohitajika na mtandao wa simu
Taarifa hiyo ikiwemo namba yako ya simu
Hivyo simu ikishascan qr code eUICC itazisoma taarifa na kuzihifadhi na kisha kukuanganisha na mtandao husika
Na itaanza kufanya kama laini za kawaida plastiki
Taarifa za laini hii inaweza kuondolewa ama kuongezwa nyingine kikawaida eSIM inaweza kuhifadhi mpaka laini nane
Hitimisho
Natumai maelezo haya mafupi yameweza kukupa mwangaza wa maana ya eSIM
Hutokuwa na haja ya kujiuliza eSIM ni nini isipokuwa kazi kubwa ni kukagua kama kifaa unachotumia kinayo hiyo teknolojia
Maoni 72 kuhusu “eSIM ni nini? Fahamu kama simu yako inayo”
Naomba kuuliza ikiwa simu yangu ina uwezo wa kuingia line moja pekee je naweza kuadd yapili ya esim?
Ndio inawezekana
Nna swali kama simu itapotea laini iliyosajiliwa kwa esim inaweza kufutwa?
Kabisa unaweza ukaiblock
Je kwa simu nyingne janja kama tekno cammon 11 au hizi vivo na xiomi azina hy kitu
Kwa tecno sijabahatika kuona simue yenye esim, kwa xiaomi zipo baadhi kama xiaom 12t pro na vivo ipo vivo x90 pro
Infinix hot 10 lite haina hii eSIM
Haina
Ninaweza kupata sm ya mkopo
Simu ya Aina gani?
Nawezaje kupata code ya google pixel 4a ili niruhusu eSIM
Tembelea ofisi za Airtel, Wana hii huduma
Galaxy A04s haina?
Haina
Ongereni kwa kuboresha uduma
Naomba kuuliza kwanini baadhi ya google pixel hazikubali?/
Esim?
Tangu pixel 3 na matoleo yaliyofuta Yana eSim, pixel ipi imegoma kwako.
Sumsung A13 inauwezo wa Esim?
pixel 3XL
Pixel 3xl inayo
nina samsung s8 plus lain moja ni kiangalia inakuja MEID je mnatusaidiaje na sisi ambao hazisom EID
Kama haina huwezi kutumia esim
Kwa mfano unatumia eSIM,halafu simu imeibwa au kupotea na huna Hela ya kununua simu kubwa Kwa wakati huo,unaweza kuirenew kama laini ya kawaida na kutumia kwenye kiswaswadu?
Inawezekana
Je hakuna simu za infinix zenye mfumo wa eSIM ?
Sijabahatika kuziona
Daah hongera sana ndugu kwa elimu yako nzuri ya matumizi ya si janja, nilikua sijui kama iyo uduma ya eSIM kama inapatikana hap inchini kwetu, nilikua naskia redioni tu
Naikiwa imeandikwa MEID itakuwa na esm
Hapana namba ya esim inaitwa EID
Naomba kuuliza je nikiwa nishaaweka esim kwenye sim yangu naweza kutumia laini nyengine ya kuchomeka kwa trey ?
Ndio inawezekana
Je ninaweza tumie 1Sim na 2Esims yani jumla zinakuwa 3 kwa wakat mmoja?
Ndio inawezekana
Habari, naomba kujua kwa samsung a04e je inaweza kuwa na uwezo wa esim
Hii haina esim
Kam sim inayo esim na hutaki kuitumia kunauwezekano wa kutumia lin ya kawaida tu coz me inanisumbua san
Samsung note 10 plus inayo esimu
Hapana S10 plus haina esim
iPhone seven plus ina support eSIM!?
Haisapoti
Nina s21ultra Ina mfumo eSim nafanyaje
Nina s21ultra ina mfumo wa esim nafanyane
Inayo hiyo, nenda kwenye Duka mtandao husika utapata utaratibu
How i can add another sim card??
Becouse my phone is using 1 sim card
Which phone are you using?
Naweza kuadd esim mpaka laini ngap?
Nadhani mpaka nane
Vp aquos zero5g ina huo uwezo
Haina hii kitu
Simu yangu ni samsung s20 ultra 5G mbona najalibu kuunganisha kwenye ESIM inagoma au kuna setting nyingine tofauti na hii
Nina aguos sense5 hii haina uwezo nayo
Ndio haina
Aquos sense5 vip unauwezo wa kuwa na esim
Haina
Mm ni wakala wa Airtel je naweza kupata mafunzo ya kuwaunga wateja huduma ya Esm maana wateja wengine wanaona tabu kwenda ofisin kama Kuna namna utanielekeza naomba unipigie uku nitakulipa0615327756
Ni vizuri ukaomba kazini kwako wakupe maelekezo zaidi
Je hatua za kuunganisha sim ya google pixel 3a ni zip maana sijaelewa hapo msaada please
Kama inayo tembelea Duka la mtandao unayotaka esim wakupe profile ya kuweka kwenye simu
Asante kwa elimu nzuri, naomba kuuliza, kama una laini ambayo ni hardcopy na unaitumia kwenye simu ndogo, je namba hiyohiyo unaweza kutumia kweny eSIM na zote zikafanya kazi?
Hii haiwezekani
KWANINI simu Yangu iphone 15 haisapot na a inagoma kuubganisha wasap,,,,pia haioneshi kuwaka KK wa data,,,ila ukiwassh data unaona vitu vinafunguka?
Hebu nitumie picha WhatsApp nione ujumbe unaoaema
KK wanini simu Yangu iphone 15 haitaki kusuport wasap?
Inakataa hata Kwa kupakua kwenye app store?
Aquos zero 6 unaweza kuweka e-sim ngap? Yaani naweza kuweka e SIM mitandao zaidi ya moja?
Je naweza kupata eSIM online au mpaka nitembelee mawakala wa mtandao husika
Inaibidi uwatembelee
Sorry,naomba unsaidie kujua bei ya sasa ya pixel 3a na pixel 4
Naweza kuunganisha line mbili kwenye e-sim na bado nkaweka line ya kawaida pale sim1 na zote 3 zikawa available hewani? Ama hizo zilizo kwenye e-sim zitakuwa za ku switch muda tofauti tofauti?
Sijaelewa swali vizuri, Ila eSIM unaweza tumika na Laini ya kawaida
1. Umesema mfumo wa eSIM unaweza ukatumia line zaidi ya 7 ( hadi 8), Maana yake unaweza eSIM kwa line hizo zote kwa wakati mmoja na zote zikafanya kazi kwa ufasaha??.
2. Chapicho lako ni la mwaka jana, ambapo mtandao mmoja tu wa Airtel ndio ulikua na huo mfumo, je sasa ni 2024 Kuna mtandao wa simu uliokua na mfumo wa eSIM ukiachana na Airtel??.
mpaka sasa kuna vodacom na tigo, ndio unaweza kufanya hivyo