Vivo Y19s ilitoka mnamo mwezi wa kumi mwaka 2024
Ni simu ya daraja hivyo gharama yake sio kubwa sana
Kwa Tanzania, bei ya Vivo Y19s ni shilingi LAKI NNE
Hii simu ina vitu vichache vikubwa ikizangatiwa inawalenga zaidi watumiaji wa kawaida
Hivyo katika hii post kuna maelezo ya kina katika vipengele kadhaa
Vipengele vilivofafanuliwa vitakupa muongozo juu ya uwezo wa hii simu na mahitaji yako
Sifa za Vivo Y19s
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1,128GB,64GB,na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.68inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Uwezo wa Network
Vivo Y19s ni simu ya 4G inayosapoti laini za kawaida
Kwa maana haisapoti teknolojia za eSIM
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 7
Kasi ya LTE Cat 7 ni 300Mbps upande wa kudownload
Kwa maana kama mtandao unakupa hii kasi basi vitu vikubwa vitakuwa vinamalizika kwa muda mfupi
Kwa bahati sehemu kubwa ya mitandao Tanzania watu wanapata kasi ya chini ya Mbps 100
Ubora wa kioo cha Vivo Y19s
Kioo chake ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo
Hata hivyo kinaambatana na refresh rate ya 90Hz, ambayo ni kubwa
Uzuri mwingine ni kuwa kioo chake ni angavu kinafika nits 1000
Hivyo unaweza tumia simu katika mazingira yoyote na kioo kikawa kinaonyesha vitu vizuri
Nguvu ya processor Unisoc Tiger T612
Kama ilivyotanguliwa kuelezwa ni kwamba hii ni simu ya daraja la chini
Na inaambatana na vitu vingi vyenye ubora wa kawaida
Hivyo hata processor iliyopo sio kwa ajili ya kufanya vitu vikubwa kama magemu makubwa kubwa
Kwa sababu processor yake unisoc tiger t612 ina muundo wa cortex a75 kwenye core zenye nguvu
Na hivyo basi utendaji wake sio mkubwa
Uwezo wa betri na chaji
Hii simu betri yake ina ukubwa 5500mAh
Ni betri hivyo lazima simu itakuwa na ukaaji wa chaji wa muda mrefu
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 15
Umeme wa wati 15 unachukua muda mrefu kujaza betri kubwa
Kwa sasa baadhi ya simu za laki nne huwa na chaji za wati 30
Ukubwa na aina ya memori
Vivo Y19s inatumia muundo wa memori wa eMMC
Ni muundo wa kitambo kizamani kutokana na kasi yake kuwa ndogo
Tofauti na muundo unaotumika sana sasa wa UFS
Upande wa memori, zipo vivo za aina mbili ambapo kuna ya GB 64 na GB 128
Huku mgawanyo wa RAM ukiwa wa GB 4 na GB 6
RAM kubwa ndio inafaa kukupa ufanisi zaidi
Uimara wa bodi ya Vivo Y19s
Hii simu imeundwa kwa bodi ya plastiki upande wa nyuma na mbele
Ila ni imara kuzuia vumbi na maji ya kunyunyulizika katika pande zote
Kwa maana inaambatana na viwango vya IP64
Hata hivyo ni muhimu kuiwekea kava japo ina uthibitisho wa MIL-STD-810H
MIL-STD-810H inaamanisha simu inaweza kutumika kwenye mazingira yote korofi
Ila hata hivyo umakini unatakiwa
Ubora wa kamera
Vivo Y19s ina kamera moja yenye lenzi ya megapixel 50 ikiwa na teknologia ya autofocus aina PDAF
Hii simu inaweza kurekodi video za full hd pekee kwa kiwango cha 30fps
Japo lenzi ni kubwa ila processor yake hawezi kuchakata resolution kubwa
Kiujumla ni kwamba mfumo wake kamera ni wa kawaida
Ubora wa Software
Vivo Y19s inatumia android 14 na haijaainishwa popote kama itapokea Android 15
Mbali na Android 14, mfumo mwingine ni Funtouch 14
Kwa wapenda kamera, funtouch 14 inakupa filters zaidi ya 14
Kwa hiyo utaboresha muonekano wa picha kwa namna inavyokupendeza
Na kitu kingine ni uwepo wa app ya smart mirroring inayokuwezesha kushea skrini ya simu yako kwenye kifaa kingine
Washindani wa Vivo Y19s
Yapo matoleo mengi sana ya daraja hili ambayo yametoka mwaka
Matoelo hayo kuna Infinix hot 50, Tecno Spark 30, Redmi 14C na hata Samsung Galaxy A06
Hayo matoleo yana sifa nyingi zinazofanana na Vivo Y19s
Neno la Mwisho
Bei ya Vivo Y19s ni ya wastani ila inaweza kuwa ina changamoto kwa kutazama simu nyingine za madaraja ya kati na ya chini
Maana kwa bei hii mtu anaweza akapata simu kali inayotumia vioo vya amoled, yenye kamera ya ultrawide na chaji ya wati zaidi ya 25
Lakini ni simu inayoweza kukidhi mahitaji mengi kwa mtumiaji asiyehitaji mambo mengi