Simu za Tecno Spark 4 na Spark ni simu za daraja la chini za mwaka 2019
Spark 3 ilitangulia kabla ya spark 4
Kiteknolojia, hazina vitu vizuri na hivyo basi bei ya tecno spark 4 na spark ni ndogo kwa kiasi kikubwa
Ni muhimu kujua kila kipengele cha sifa zake ili ujue iwapo inaendana na mahitaji yako
Kumbuka ina miaka minne tangu itoke
Bei ya spark 4 na spark 3 Pro (GB 32)
Tecno spark 3 Pro ya GB 32 kwa sasa inauzwa shilingi 140,000
Wakati huo spark 4 inauzwa kwa kima cha shilingi 150,000
Kwa sasa hizi simu janja nyingi zilizopo ni used
Kuna ugumu wa kupata matoleo mapya
Kwani kuna matoleo mengi ya Spark yametoka kuanzia mwaka 2020
Sifa za tecno spark 4 na spark 3 pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 32GB na RAM 2GB |
Kamera | Kamera spark 4 tatu
Spark 3 mbili
|
Muundo | Urefu-6.52inchi(spark 4)
-6.2inchi (spark 3) |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 150,000/= |
Upi ubora wa spark 3 na 4
Ubora mkubwa hizi simu ni kuwa na kupata mtandao wa 4G
Vitu vingi vilivyopo haviendani na nyakati za sasa
Ukizingatia kuwa spark 4 na 3 hazina uwezo wa kupokea matoleo mapya ya android
Kitu kinachochangia kuishusha simu thamani
Maana software huboresha baadhi ya vitu kwenye simu na kuipa maisha marefu ya kutumia apps nyingi kwa miaka mingi
Uwezo wa Network
Simu zote zinasapoti mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7
Kasi ya LTE Cat 7 kwenye kudownload inafika 300Mbps
Kwa maana kama unapakuwa faili la lenye ukubwa wa MB 75 kama whatsapp basi simu itamaliza baada ya sekunde mbili
Kitu cha kuzingatia ni kuwa swala la spidi hutegemea na uwezo wa kampuni ya mawasiliano unayotumia
Kwa hapa Tanzania hakuna mtandao wa simu unaotoa kasi 300Mbps
Maana kwa sasa hii ni kasi ya 5G kwenye mtandao wa vodacom
Ubora wa kioo
Kioo cha tecno spark 3 na spark 4 ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ya 720×1500 pixels
Ni resolution ndogo kwani kwa sasa zipo simu za daraja la chini zenye resolution kubwa zaidi ya hiyo.
Muonekano wa vitu hautokuwa wa kuvutia ukilinganisha na vioo vya amoled
Changamoto ni kuwa ujazo wa rangi kwenye vioo vya LCD sio mkubwa
Refresh rate yake pia ni ile ya kawaida kwani haifiki 90Hz wala 120Hz
Hata hivyo, bei yake inaendana na ubora wa vitu vilivyomo
Yaani hakuna kutarajia ubora mkubwa sana
Nguvu ya processor
Tecno Spark 3 Pro yenyewe inatumia chip ya Mediatek Helio A22 katika kufanya shughuli zake
Nguvu ya helio a22 ni ndogo kwani zina muundo wenye kutumia nguvu kidogo na umeme kidogo
Idadi ya core kwenye kila simu zipo nne na zote zinaundwa na muundo wenye utendaji hafifu
Usishangae baada ya muda kupita simu kuanza kuwa nzito hasa unapowasha intaneti
Kwenye app ya kupima nguvu ya processor ya Geekbech, helio a22 inazalisha alama 160
Ni ndogo sana kwa miaka hii
Kitu kizuri kwenye hii chip ni matumizi madogo ya umeme
Hivyo betri inaweza kukaa kidogo
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya Tecno Spark 4 ni 4000mAh
kwa sasa simu nyingi zinakuja na betri kubwa zaidi ya 5000mAh
Ukaaji wa chaji sio mkubwa kiivyo kutokana na betri yenyewe kuwa ndogo
Spark 3 Pro betri yake ina ukubwa wa 3500mAh
Na yenyewe ni ndogo
Kwa mantiki hii ni ngumu kwa hizi simu kufika masaa 13 ukiwa unatumia intaneti muda wote
Ila kwa matumizi ya kupiga simu kutuma sms simu itachukua muda mrefu kukaa na chaji na chaji
Ukubwa na aina ya memori
Hizi simu zipo za aina moja tu kwenye ukubwa wa memori
Zote zina ukubwa wa GB 32 na RAM ya GB 2 ila spark 4 ipo ya ram ya gb 3
Ukubwa wa memori unaweza kuhifadhi vitu vichache
Kama utakuwa ni mtumiaji sana apps za whatsapp na telegram simu itawahi kujaa
RAM ndogo ni kizingiti wakati unapotumia apps nyingi kwa wakati mmoja
Simu inaweza kuwa na utendaji wa chini
Uimara wa bodi
Hizi simu zimetengenezwa kwa bodi za plastiki upande wa nyuma
Baadhi ya bodi za plastiki huwa na kawaida ya kuchunika rangi japo inategemea na utunzaji
Ni vizuri ukawa unaweka kava mara kwa mara ili ubora wake usipungue kwa haraka
Hazina uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani
Ni tofauti na simu kama za iphone ambazo zikizama ni ngumu maji kupenya
Ubora wa kamera
Spark 3 pro ina kamera zipatazo mbili
Huku spark 4 ikiwa na kamera tatu
Kamera kubwa ya spark 3 pro na spark 4 zinafanana, ni kamera ya aina moja yenye MP 13
Kamera za hizi simu kiujumla hazina ubora mkubwa hasa ukipiga kwenye mwanga hafifu
Zote zinaweza kurekodi video za full hd pekee yake
Ubora wa Software
Kwa sasa toleo jipya kabisa la android ni android 13
Spark 4 na 3 pro zenyewe zinatumia android 9
Na hazipoeki sapoti yoyote ya kupata toleo jipya
Android 9 bado inaweza kutumia app za aina zote
Maana waundaji wa app bado wanatoa sapoti kwa toleo hili
Ukizingatia ni 30% tu simu za android ndio zinatumia toleo la android 12
Washindani wa Tecno Spark 3 Pro na Spark 4
Kama ilivyotanguliwa kuelezwa mwanzoni, hizi ni simu zenye muda mrefu
Zinashindana na simu nyingi za bei ndogo
Mshindani wa kwanza ni matoleo ya spark yote yaliyokuja baadae mfano ni tecno spark 8C
Haya yameboreshwa kwa kiasi fulani na yana matoleo ya android ya hivi karibuni
Mshindani mwingi ni Redmi 9A na Redmi 10C bila kusahau Samsung Galaxy A104
Na hata simu used ya google pixel 3 ina ubora zaidi ya spark 3 na inapatikana kwa bei nafuu.
Hitimisho
Kiushauri zaidi ni kuwa hizi sio simu za kuwa nazo kwa sasa labda kama bajeti imebana sana
Tayari ina mambo mengi ambayo yameachwa na wakati
Ni vizuri ukajichanga kuongeza pesa ili ununue matoleo mapya zaidi yenye ubora wa ziada.