Tecno wameleta toleo jipya la simu ya madaraja ya chini yenye maboresho
Ina maboresho upande wa skrini(kioo) kuwa na refresh rate kubwa ambayo mara hupatikana kwenye simu za daraja la kati kwenda mbele
Pamoja na maboresho hayo, bado bei ya Tecno Spark 30C ni ndogo na ambayo wengi wanaweza kiumudu
Kwani bei yake rasmi kwa Tanzania ni shilingi laki mbili na elfu tisini (290,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4.
Tuzame kiundani zaidi ulewe ubora na changamoto za Tecno Spark 30C ili ufanye uamuzi sahihi
Sifa za Tecno Spark 30C
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB, na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 290,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Spark 30C ni simu ya 4G inayosapoti laini mbili
Haishangazi kutokana na aina ya bei na aina ya wateja inayolenga
Kwa maana ukiwa na hii simu hautoweza kutumia 5G hata kama upo kwenye eneo linalosapoti 5G
Kwa bahati au nzuri 5G imeenea maeneo machache sana hapa Tanzania
Kwani hata wamiliki wa simu zenye 5G mara nyingi kama si mara zote hutumia mtandao wa 4G
Hata mambo yanaweza mabadilika kadri muda utakavyokuwa unasogea
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 30C
Kioo cha hii simu kina refresh rate inayofika 120Hz
Lakini kioo kina resolution ya kawaida ambayo sio full hd
Refresh rate kubwa hufanya kioo kuwa chepesi na muonekano mzuri pale unapokuwa unaskrol ama kucheza gemu
Ila changamoto kubwa ya refresh rate kubwa ni kutumia umeme mwingi
Ni vizuri ukatambua sio nyakati zote utahitaji kutumia refresh rate kubwa
Ni vizuri ukaizima kama una matumizi ya kawaida
Nguvu ya processor Mediatek Helio G81
Nguvu ya processor sio kubwa kivile japo inakuwezesha kucheza baadhi ya gemu kama PUBG Mobile
Ila gemu kama Call of duty au assassin creed itakulazimu kupunguza ubora wa graphics vinginevyo simu inaweza kukwama kwama
Hii inasababishwa na processor ya mediatek helio g81 kuundwa na muundo wa Cortex A75 kwenye core zenye nguvu kubwa
Hata kwenye inayopima nguvu za processor za simu helio g81 ina alama kama 400 hivi
Ambapo ni ndogo
Lakini kumbuka simu inamlenga mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida
Hivyo inakuwa haina haja ya kuweka teknolojia kubwa sana kwenye simu kwani itaongeza gharama na simu kuwa na bei kubwa
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya inapeleka umeme wa wati 18
Ni kasi ya wastani na simu inaweza kuchukua muda kidogo kujaa
Kikawaida cha wati 33 hujaza betri kwa muda wa dakika 80 yaani lisaa limoja na dakika ishiri
Wati 18 inaweza chukua hata masaa matatu kujaza betri kubwa ya mAh 5000
Kwa mtumiaji wa hii simu atanufaika pia na ukaaji wa chaji
Kwa sababu processor iliyopo imeboreshwa pia kwenye matumizi ya chaji
Kiwastani ukiwa kwenye intaneti muda wote simu inadumu na chaji kwa masaa karibu 12
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili upande wa ukubwa wa memori
Unaweza ukapata ya GB 128 na GB 256
Na zote zimagawanyika katika matoleo ya aina mbili upande wa RAM
Unaweza ukapata mojawapo yenye RAM ya GB 4 ama GB 6
Kama ukiweza kuongezea pesa, chukua yenye RAM ya GB 6
RAM kubwa inakupa upana kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja bila kufanya simu kuwa nzito
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 30C
Bodi yote ya Tecno Spark 30C ni ya plastiki
Tofauti ni simu za gharama kubwa ambazo zinaweka bodi za titanium
Katika mazingira yenye maji ya kunyunyulizika, maji hayatoingia ndani ya simu kama utakuwa umejisahau
Ila simu ukiizamisha kwenye kina kikubwa cha maji mengi basi itaharibika
Kwenye skrini simu haiji na protekta
Ni muhimu ukanunua protekta kuepuka na changamoto ya simu kupasuka
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera moja inayokuja na ukubwa wa megapixel 50
Kwa nyuma muonekano wake unashawishi kusema kuna kamera tatu ila hapana ni kamera moja
Ubora wa picha hasa kwenye mwanga simu inajitahidi kupiga picha nzuri
Japo baadhi ya vitu vina uzidisho wa rangi
Kiasi cha kwamba ule muonekano wa asili unaweza potea
Simu inaweza kurekodi video za full hd na haiwezi kurekodi video za resolution kubwa zaidi
Ubora wa Software
Tecno Spark 30C inakuja na mfumo endeshi wa Android 14 na HIOS 14
Muda si mrefu Android 15 itatoka
Lakini hakuna taarifa kama spark 30c itapokea android mpya
Tukiachana na hilo, matumizi ya AI kwa sasa ndio jambo kubwa kwa matoleo mengi ya simu
HIOS 14 inakupa AI ya chatgpt ambayo utaweza kupata taarifa na majibu kwa kuiuliza maswali mbalimbali
Hivyo hutokuwa na haja ya kuidownload au kwenda kufungua chatgpt
Washindani wa Tecno Spark 30C
Simu mbadala zinazoshindana na tecno zipo nyingi
Ila chache zinazoweza leta ushindani mkubwa sana kwa hapa Tanzania ni Samsung Galaxy A06 na Redmi 14C na hata itel S24
Simu tajwa hapo juu zinaendana sana kisifa na mambo mengine
Sema kuna vitu vidogo simu zinazidiana
Kwa mfano itel s24 kamera yake ina megapixel 108 na utendaji wake mkubwa kidogo
Na bei ya itel s24 inaendana kwa sehemu kubwa na tecno
Neno la Mwisho
Kwa watu wenye bajeti ndogo za kununua simu sasa hivi wanapata ya kutumia kioo chenye refresh rate kubwa
Si hivyo na hata ubora wa kamera umeboreshwa kwa kiasi fulani
Kwa hiyo baadhi ya mambo yaliyokuwa yanapatikana kwenye simu za gharama utaweza kupata kwenye tecno spark 30c japo kwa uchache sana
Hivyo bei ya tecno spark 30c imeitendea haki sifa zinazoambatana na hii simu