Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni
Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 Pro+ ni shilingi laki sita, hii ikiwa na ukubwa wa GB 256
Kuzijua sifa za spark 20 Pro+ itakupa picha ya jumla na sababu ya simu kuwa na bei hiyo
Na hivyo pia kuwa na ufahamu iwapo simu ina vigezo vinavyokizi mahitaji yako
Hivyo basi kitu cha kwanza tutazame sifa zake.
Sifa za Tecno Spark 20 Pro+
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 650,000/= |
Tutazamie ubora na udhaifu wa sifa muhimu za hii Tecno
Uwezo wa Network
Tecno Spark 20 Pro+ ni simu ya 4G kwa maana haina mtandao wa 5G
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 13 ambayo kasi yake ya juu kabisa ni 650Mbps
Iwapo kuna mtandao wa simu unaotoa kasi hii basi simu itakuwa inapakuwa mafaili kwa muda mfupi
Ila kwa sasa kasi kubwa zaidi utaipata ukiwa unatumia 5G kwa hapa Tanzania
Kwa mfano 5G ya Tigo ina kasi mpaka 1Gbps (zaidi ya 1000Mbps)
Kwa bahati mbaya 5G imesambaa maeneo machache sana nchini
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 20 Pro+
Kioo cha Tecno Spark 20 Pro+ kina uoneshaji mzuri wa vitu na muonekano mzuri wa rangi
Kioo chake ni cha AMOLED chenye resolution ya 1080×2436 pixels
Mbali na resolution kubwa, kioo kina refresh rate inayofika 120Hz
Uzuri wa refresh rate kubwa huifanya simu kuwa fasta wakati wa kutachi(kuperuzi)
Ila huwa ina ulaji mkubwa wa chaji
Hata hivyo mfumo wa tecno unaruhusu kuzima na kuweka refresh rate ya kawaida
Kwa simu nyingi za gharama za mwaka 2024 zimekuwa zikitumia vioo vya LTPO AMOLED ambazo huwa na uwezo wa kudhibiti kiwango cha refresh rate kulingana na aina ya matumizi
Nguvu ya processor Helio G99 Ultimate
Nguvu ya processor ya Helio G99 Ultimate ni ya wastani
Hii ndio chip iliyotumika na simu ya spark 20 pro plus, na inacheza gemu nyingi kwa ufanisi mkubwa
Njia nzuri ya kupima nguvu ya processor ni namba za fps unapocheza gemu
Zikiwa kubwa zaidi ya 60 basi hiyo chip ni nzuri
Helio G99 Ultimate inazalisha mpaka FPS 80 kwa gemu ya PUBG Mobile ila kwenye setting ndogo za graphics
Haina nguvu kubwa kama Snapdragon 8 gen 3 ila ni processor nzuri kwa simu za daraja la kati
Helio G99 Ultimate ina core mbili zenye nguvu ya wastani zinazotumia Cortex A76
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Tecno Spark 20 Pro+ ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 33
Simu nyingi zenye chaji ya wati 33 hujaza betri ya simu kwa dakika 80 kama muda wa juu kabisa
Na betri ya mAh 5000 inaweza kustahimili kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 10
Ila kwa mpenzi wa magemu ukaaji wa chaji hauwezi kuzidi masaa kumi
Magemu huifanya processor kutumia nguvu kubwa inayotumia umeme mwingi
Chaji yake ni ya USB Type C (zile zenye kichwa kipana)
Ukubwa na aina ya memori
Kuna toleo la aina moja tu la Tecno Spark 20 Pro+ upande wa memori
Ukubwa wake wa memori ni GB 256 na RAM 8GB
Memori hii inatosheleza kuhifadhi mafaili mengi na RAM ya GB 8 inasaidia kufungua vitu kwa wakati mmoja bila kukwama
RAM ndogo inakuwa na changamoto ya kujaa kwa haraka hivyo kuna nyakati unakuta simu inaganda ganda
Aina ya memori ya hii simu ni UFS 2.2 inayoweza kusafirisha data kwa kasi inayofika 1200MBps
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 20 Pro+
Bodi ya Tecno Spark 20 Pro+ imetengenezwa kwa glasi upande wa mbele na nyuma kuna plastiki
Ina viwango vya IP53 vinavyoashilia uwezo wa simu kuzuia maji ya kiwango cha kuchuruzika
Ila maji yanaweza penya kama ikizama kwenye kina kikubwa
Kiujumla umakini ni kitu cha muhimu kwa hii simu
Pamoja na uwepo wa kioo upande wa mbele kununua screen protekta kutaimarisha uimara wa simu
Maana hata vioo vya Gorilla hupasuka pia
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera mbili ila kiuhalisia kamera ipo moja tu
Kamera yake ina megapixel 108 inarekodi video za resolution ya 1440p kwa fremu za 30fps
Kwa picha chache nilizoziona ni kuwa ubora wa picha ni mzuri ila kwenye kamera ya selfie kamera inang’arisha sana kiasi cha kutokutoa muonekano halisi wa kitu
Changamoto hii nimeiona kwenye simu nyingi za infinix
Inawezekana ikawa kwa sababu inalenga watu wanaopenda kuposti mitandaoni
Hivyo inaondoa uhitaji wa filters
Lakini kamera inayotoa vitu kwa muonekano wa asili ndio nzuri zaidi
Ubora wa Software
Tecno Spark 14 Pro inakuja na toleo la Android 14
Kitu kikubwa kwenye toleo la Android 14 ni matumizi ya akili bandia
Ina mfumo wa akili bandia unaotengeneza wallpaper
Kwa bahati mbaya mfumo huu hautengenezi picha kwa kuandika maneno kuelezea namna picha unavyotaka iwe
Ni mfumo ndio unaotengeneza wallpapers kwa namna unavyoamua
Washindani wa Tecno Spark 20 Pro+
Tecno Spark 20 Pro+ inaenda kukutana na ushindani kutoka matoleo ya Samsung Galaxy A55, Samsung Galaxy A35, Redmi Note 13 Pro, Oppo A79
Tukianza na redmi note 13 ina sifa zinazofanana kwenye kioo na kamera
Ila ina kamera mbili za ziada zenye lenzi ultrawide na macro
Na pia inakuja na mtandao wa 5G
Ushindani upo kwenye bei, kwani Redmi Note 13 ina bei sawa na Tecno Spark 20 Pro+
Oppo A79 inazidiwa ubora wa kioo na hata kamera ila sifa nyingine zinafanana ikiwemo utendaji
Ila bei ya Oppo A79 ipo chini na ina 5G, hii inaweza mshawishi mtumiaji kutumia oppo a79 badala ya spark
Neno la Mwisho
Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ inaendana na bei ya simu nyingi za daraja la kati
Na sifa zake nyingi ni za kuvutia ila kuacha kuweka mtandao wa 5G inaweza ikawa ni changamoto hasa kwa kipindi ambapo simu mpya nyingi zinatoka
Japo kwa soko la hapa nchini 5g inapatikana maeneo machache, ila simu ya 5G inampa mtu kujiamini pindi mtandao ukisambaa maeneo mengi
Maoni 9 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake”
Ningependa izi cm angarau zishuke bei kwani nasisi wenyekipato Cha chini tuweze kutumia.
Naipenda Tecno spark20 pro plus sema bei jalibuni kutuangalia na sisi
Ningependa hizo tecno 20 zipunguzwe bei ili na sisi wenye kipato cha chi tupate kutumia
mi naona wapunguza angalau hifke hasta laki 5 hili na sisi watuchini tupate kutumia
Napenda Ila. Sio kama phantomx2 pro
ninzuri sana ila sisi wakipato cha Hali chini tutaishia kuziyamani
Naomba kujua bei halisi ya Tekno spark 20 pro plus mala baada ya kutoka Tekno spark 30 pls
naihitaji iyo cm lakini mpunguze bei ata kwa laki 5
mtupunguzie bei iwe ata lakitano naitaji cm iyo