Hivi karibuni simu mpya ya Samsung Galaxy S23 Ultra imeingia sokoni huku bei yake ikiwa haitofautiani sana na Apple iPhone 15 Pro Max
Kwenye soko la dunia bei ya samsung galaxy s24 ultra inaanzia shilingi milion tatu na laki mbili
Na kwa hapa Tanzania bei yake ya GB 256 inafika mpaka milioni tatu na laki tano kutegemea na duka
Simu za milioni tatu huja na vitu vingi sana vyenye ubora mkubwa kwenye nyanja nyingi
Kikubwa ambacho Samsung wamekipromoti sana na matumizi ya AI(Artificial Intelligence) kama ilivyo kwa Google Pixel 8 Pro
Tuitazamie kila kipengele cha hii simu kwa kuzingatia sifa zake zilizoambatana nazo
Sifa za Samsung Galaxy S24 Ultra
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic LTPO AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 4.1, 256GB,512GB,1TB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,300,000/= |
Ubora wa kamera
Kama una muda zitazame picha ambazo ambazo zimepigwa na samsung galaxy s24 ultra kupitia hapa
Utaona picha iliyopigwa kwenye mwanga hafifu(kiza kingi)
Kamera ya hii simu ina ubora mkubwa katika kuonyesha vitu
Pamoja na kwamba mwanga ni mdogo maandishi ya jengo, rangi za majani na rangi ya jengo zinaoonekana na hajiathiriwa na kiza kingi kilichopo kwenye eneo husika
Usahihi wa rangi ni mkubwa hata nyakati za mchana, vitu vingi vinaonekana kwa muonekano wake wa asili
Hakuna muangaza uliopitiliza
Kamera za hii simu zinaweza kurekodi mpaka video za 8K kwa kasi ya 30fps
Na tena kamera yake inaweza kurekodi kwa HDR10+ ambayo inaongeza kina cha rangi
Hivyo kuipa kamera uwezo wa kuzalisha rangi nyingi zaidi
Uwezo wa network
Samsung Galaxy S24 Ultra inasapoti network zote ikiwemo 5G
Inasapoti 5G za aina zote tatu hata ile yenye masafa marefu ambayo yana kasi kubwa ya kupakua na kupakia mafaili
Kwa maana hiyo simu inaweza kutumika popote duniani
Ni jambo zuri kuwa na simu ya 5G kwa sababu 5G imeshaanza kupatikana kwa baadhi ya maeneo
4G yake ni aina ya LTE Cat 24 ambayo kasi yake inafika 10000Mbps ambayo ni kubwa sana kwa 4G
Kama miundombinu ya mtandao husika inasapti kasi hii ya intaneti basi simu itakuwa inadownload vitu kwa sekunde
Ubora wa kioo
Samsung Galaxy S24 Ultra inatumiaa kioo cha Dynamic LTPO AMOLED 2X
Vioo vya LTPO huongeza ama kupunguza kasi ya refresh rate kutokana na aina ya matumizi
Kwa sababu refresh rate kubwa hutumia sana moto mwingi
Na kiwango kikubwa cha refresh rate hufanya simu kuwa nyororo unapotachi
Ila si mara zote utahitaji refresh rate ya 120Hz, apo ndipo umuhimu wa LTPO unapokuja
Uangavu wa kioo cha samsung s24 ultra unafika mpaka nits 2400 kwa kiwango cha juu za zaidi
Hii inafanya kioo kuonyesha kwa uangavu kwenye mazingira yoyote, iwe juani ama ndani
Nguvu ya processor Snapdragon 8 gen 3
Samsung Galaxy S24 Ultra inatumia prosesa ya snapdragon 8 gen 3 kufanya kazi zake
Hii ni chip yenye na ufanisi mkubwa wa matumizi ya umeme
Kwa baadhi ya app za kupima nguvu za prosesa snapdragon 8 gen 3 inaizidi hata Apple 17 Pro ambazo zinatumiwa na simu za iPhone 15 Pro
Snapdragon 8 gen 3 imegawanyika katika sehemu nne, sehemu mbili inahusisha core zenye nguvu ambazo huwa ni mahususi katika kufanya kazi zinazohitaji nguvu kubwa
Na pia core zilizobaki ni kwa ajili ya ufanyaji kazi zinazotumia nguvu ndogo
Moja ya vitu utakavyonufaika navyo kuwa na simu yenye snapdragon 8 gen 3 ni utendaji wake kwenye mambo ya akili bandia yaani Artificial inteligence(AI)
Snapdragon 8 Gen 3 inakuja na kitu kinaitwa Stable diffusion ambacho kinakupa uwezo wa kutengeneza picha kwa kuipa simu maneno ya jinsi picha unavyotaka iwe
Ndio maana samsung wameweka mifumo mingi ya AI kwenye hii simu
Uwezo wa betri na chaji
Kama ilivyo kwa simu nyingi siku hizi, betri ya galaxy s24 ultra ina ukubwa wa 5000mAh
Hivyo ukaaji wa chaji ni wa kiwango kikubwa
Ukiwa unacheza gemu muda wote, betri inaweza kudumu kwa muda wa masaa tisa
Wakati wa kucheza gemu simu hutumia nguvu kubwa na kioo cha simu kutumika muda mwingi pia kunawahi kumaliza betri ya simu
Ndio maana simu inaweza kudumu kwa muda wa masaa tisa
Ukiwa unaperuzi intaneti simu inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 11
Kiwasatani samsung hii inazidiwa na Apple 15 Pro Max kwa takribani masaa matatu katika ufanisi wa betri
Simu haiji na chaji ila inasapoti kasi ya wati 45
Mpaka simu ijae kwa 100% kutoka 0% inachukua takribani dakika 65 (muda mfupi huu)
Ukubwa na aina ya memori
Samsung Galaxy S24 Ultra ina matoleo matatu upande wa memori
Kuna ya GB 256, 512 na 1TB na zote ukubwa wa RAM ya GB 12
Memori ni kubwa zinazoweza kutosheleza kujaza mafaili na RAM ni kubwa inayosaidia kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja
Mfumo wa memori wa hii simu ni ule mpya wa UFS 4.0 yenye uwezo wa kusafilisha data zaidi ya mara mbili ya mifumo iliyotangulia
Hii inaongezea simu utandaji mkubwa katika maeneo mengine pia.
Uimara wa bodi ya simu
Samsung Galaxy S24 Ultra ni simu yenye waterproof kwani ina viwango vya IP68
Hii ina maanisha kuwa simu haiwezi pitisha maji kama ikizama kwenye kina cha mita 1,5 kwa muda wa nusu saa
Yaani hata simu ikizama kwenye diaba maji hayaingii kwa huo muda
Pia upande wa skrini kumewekewa kioo cha gorilla armor, kampuni ya gorilla wanadai hiki kioo ni kigumu mara nne ya toleo lilopita
Kwa maana ni kigumu kuvunjika na kuchunika, uthibitisho zaidi unahitajika
Hata hivyo vioo vya gorilla huwa ni vigumu hasa gorilla 6 na kuendelea mbele
Ubora wa Software
Ni zama za Akili bandia yaani AI ndio hype iliyopo kwa sasa
Kabla ya yote, Samsung Galaxy S24 Ultra inakuja na android 14 na One UI 6.1
Mfumo wa hii simu unaweza kutafsiri simu unayopigiwa na mtu mwingine ambaye anatumia lugha nyingine
Yaani inafanya Live Translation ya maongezi kati yako na mtu mwingine
Hii ni inaondoa ugumu wa mawasiliano kati ya watu wawili
Yaani kama hujui kiingereza unaweza kuwasiliana na mtu huyo ukiwa na hii samsung
Kitu kingine cha kufurahisha kinaitwa circle to search
Circle to search inakupa uwezo wa kugoogle kitu kwa kutumia picha kwa kuchora duara kwenye kitu unachotaka kutafuta
Washindani wa Samsung Galaxy S24 Ultra
Ni ngumu kuiona simu inayoweza kushindana na samsung hii kwa sasa
Ila Google Pixel 8 Pro, iPhone 15 Pro Max na Sony Xperia 5 V na simu zingine toka China
Washindani wengine ni Oppo Find X7 Ultra na Realme GT5 Pro ambazo zina utendaji unaochuana
Hitimisho
Kwa wapenzi wa Samsung na simu za daraja juu basi jua kuwa ubora wa hii samsung umeweza kugusa nyanja nyingi
Hii inaweza ikawa moja ya simu bora kwa mwaka huu 2024
Bei yake haishtui kwa mtu anaelewa ubora wa kina uliopo kwenye simu
Ila unahitaji bajeti ya kutosha kumiliki Samsung Galaxy S24 Ultra
Maoni 17 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy S24 Ultra na Sifa zake”
Nahitaji simu samsung s24 ultra je imefikia sh ngapi kwa sasa 2024
samsung galaxy S24 ultra, je imefika sh ngapi kwa mwaka 2024 mimi nipo mkowa wa (RUKWA) wilaya ya (NKANSI) namayere/ jilan na jiji la sumbawanga
Bei yake ndio hiyo iliyotajwa hapo
Wekeni bei ambayo mtu wa kawaida anaweza kuafford
Zipo simu za bei nafuu zinazowezwa nunuliwa na mtu wa kawaida
Kwasifa nilizozisoma hapa iyo sim nzuri sana naipataje na niko mkowan??
Je s24 ultra inapokea matoleo mangapi yajayo
Kama Saba hivi
S24 ultra inapokea matoleo mangap
Mpaka 2031iko powa
Hivi kati ya s24 plus na s24 ultra utofauti uko upande gan
Imekaaje mbona kwenye alibaba inauzwa laki 4 Tena kwapisi moja tuuu.
Kuwa Makini kiongozi
Simu nzur sana Ila nataka ya Bei ndogo ya laki 6 kushuka
Samsung A35
Mbona kunamtu anauza 250000
Kuwa Makini kabla ya kununua