Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024
Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa
Ndio maana bei ya Samsung Galaxy A35 kwa Tanzania inafika shilingi laki tisa na nusu kwa yenye GB 128
Na bei inaweza kuzidi hapo kutegemeana na mabadiliko mengine
Sasa swali la kujiuliza kwa nini bei yake inaonekana kuwa ni kubwa?
Sababu kubwa ni sifa zake hasa upande wa utendaji, kamera, kioo, software, uimara wa bodi na mengineyo
Fuatilia kufahamu namna zitakavyokufaa kwa matumizi yako
Sifa za Samsung Galaxy A35
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 950,000/= |
Uwezo wa Network
Samsung Galaxy A35 inasapoti mpaka mtandao wa 5G
Na inasapoti aina zaote tatu za 5G ikiwemo masafa ya kati ambayo yanatumika na mitandao mingi hapa Tanzania
5G ina kasi kubwa japo kwa Tanzania usambaaji wake haujaenea meaneo mengi
Na kwa kiasi kikubwa inapatikana maeneo machache ya Dar es Salaam
Hata hivyo simu ina 4G pia aina ya LTE Cat 18 yenye kasi inayofika 3790Mbps
Ambayo ni kubwa ila usitarajie kupata kasi hii ya 4G kwa hapa nchini
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A35
Kioo cha Samsung Galaxy A35 ni cha super amoled chenye resolution ya 1080×2340 pixels
Kioo chake kina refresh rate ya 120Hz kitu kinacholeta muonekano wakati wa kuperuzi ama ukiwa unacheza gemu
Uzuri wa kioo hiki cha samsung ni dynamic, kwa maana kasi ya refresh rate itaongezeka kulingana na aina ya matumizi kwa wakati huo
Unajua kuwa refresh rate kubwa hutumia umeme mwingi hivyo betri inaweza isha haraka
Hivyo sio nyakati zote refresh rate ya 120Hz inaweza ikawa inahitajika
Pia kioo kina uangavu mkubwa hivyo utaweza kuitumia hata juani na ukawa unaona vitu vizuri
Nguvu ya processor Exynos 1380
Samsung Galaxy A35 inatumia chip yenye utendaji wa wastani ya Exynos 1380
Hii ni processor imeundwa na samsung wenyewe
Inaweza kucheza gemu nyingi bila kusababisha simu kupata joto jingi
Haya ni maboresho makubwa kwani kipindi cha nyuma Exynos zilikuwa na changamoto ya kupata moto sana
Kwenye App inayopima nguvu za processor yaani Geekbench 6, Exynos 1380 ina alama 999
Ukitazama ni kuwa nguvu yake inaachwa mbali sana na Snapdragon 8 Gen 3 hata hivyo Exynos 1380 ni chip inayopiga kazi kubwa kwenye vitu vingi na unaweza usione tofauti
Uwezo wa betri na chaji
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inasapoti kupeleka umeme wa wati 25
Hii simu inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa 12 ukiwa unaperuzi intaneti
Hivyo kwa matumizi ya kawaida simu inaweza kukaa na chaji hata siku nzima
Kwenye kasi ya kukaa na chaji hii simu inaweza kuchukua takribani dakaika 86 kujaa kwa asilimia 100 kutoka 0
Ni muda mdogo na pia unaweza kuitumia simu kwa masaa mengi
Ukubwa na aina ya memori
Kuna mtoleo ya aina mbili upande wa memori na RAM
Zipo Galaxy A35 za GB 128 na RAM ya GB 6 au GB 8
Na pia zipo zenye ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 8
Hizi memori zote zinahifadhi mafaili mengi na zinatosholeza kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja bila kukwama
Uzuri ni kuwa hizi simu zinatumia memori aina ya UFS ambazo kasi yake ya kusafirisha data huwa kubwa
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A35
Bodi ya Samsung Galaxy A35 ni imara kwenye kuzuia maji kwani ina waterproof
Inakuja na viwango vya IP67 vinavyoashiria simu kutoingia maji kama ikizama kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu
Kwa maana kama kama simu ikizama kwenye ndoo ya maji ukirudi utaikuta na ikiwa inafanya kazi
Galaxy A35 inakuja na skrini protekta ya kioo cha Gorilla Glass Victus+
Kiuzoefu ni kuwa Gorilla Glass Victus+ huwa ni kioo kigumu kupasuka ila huwa vinaweza kuchunika kirahisi ikigusana na coin(sarafu)
Hii ni kwa mujibu ya waliowahi tumia simu zilizoekewa hivi vioo
Kiujumla Samsung Galaxy A35 ni simu yenye bodi imara
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera zipatazo tatu na kamera kubwa ina megapixel 50
Simu inapiga picha nzuri katika nyakati zote yaani kwenye mwanga hafifu(usiku) na kwenye mwanga mwingi
Kamera zake zinajitahidi kwa kiasi kikubwa kutoa picha zenye rangi halisi
Hazizidishi uangavu unaofanya kinachopigwa picha kung’aa sana kuliko uhalisia
Kamera zina mfumo wa OIS unaotuliza video wakati ukirekodi huku ukiwa unatembea
Na cha kuvutia zaidi ni kuwa kamera yake inarekodi mpaka video za 4K ambazo zinakuwa na muonekano mzuri zaidi
Ubora wa Software
Samsung Galaxy A35 inatumia Android 14 na One UI 6
One UI 6 inakuja na mifumo mingi ya akili bandia, kwa mfano kwenye kuedit picha
One UI 6 inakupa uwezo wa kuindoa baadhi ya vitu vilivyotokea kwenye picha iwapo uvihitaji vioonekano
Kwa mfano umepiga picha baa bia zikaonekana na wewe unataka uondoe zile picha
Basi One UI 6 inakupa huo uwezo bila kuathiri ubora wa picha
Kitu cha kufurahisha ni kuwa hii simu itakuwa inapokea matoleo mapya ya Android kwa muda wa miaka minne
Yaani mmiliki wa hii simu atakuja kutumia mpaka Android 18 kitu kinachoipa thamani simu muda mrefu
Washindani wa Samsung Galaxy A35
Pamoja na uzuri wote wa hii simu, kuna kampuni za China ni tishio kwa samsung kwenye kipengele hiki
Simu kutoka china zinauzwa kwa bei ya chini hapa na huku zikiwa na ufanano mwingi kwenye vipengele mbalimbali
Mfano mzuri ni Redmi Note 13 Pro+, vitu vingi unavyoviona kwenye Galaxy A35 vinapatikana kwenye Redmi Note 13 Pro+ ya 2023
Haitoshi ni kuwa Redmi Note 13 Pro+ inakuja na chaji yenye kasi ya 12oW na kioo chenye teknoljia za ziada kama HDR10+ na simu ina water proof ya IP68
Lakini cha kufurahisha na kustajaabisha Redmi bei yake ni shilingi laki nane na nusu
Huu ni mfano mmoja kati ya mifano mingi, hivyo Samsung ana kazi ya ziada kupambana na simu kutoka China
Neno la Mwisho
Bei ya Samsung Galaxy A35 inaendana kwa kiasi kikubwa na sifa zake katika nyanja nyingi
Kwa mtumiaji wa simu ambaye anataka kununua toleo la Samsung Galaxy S20 used hana haja ya kufanya hivyo
Kwa Ubora wa Galaxy A35 unaizidi S20 ambayo kwa sasa ina miaka minne
Ila kama unataka kitu kizuri zaidi yapo matoleo yenye ubora zaidi ya hii kwa bei ya chini
Maoni 5 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake”
Naomba kujuzwa infinix note 40pro+ na samsung A35 niipi bola???
Samsung a35 ni nzuri zaidi
Samsung a35,na Samsung s21,kavu ipi simu kali zaidi
Ni somu gani ina bei duniani
Nimependa Samsung A25 GB 256 cjui kwa Sasa Tanzania nitaipata kwa bei gang?