Simu ya redmi 9a ni simu ya daraja la mwisho iliyotoka mwaka 2020.
Japokuwa ni miaka miwili imepita ila inabaki kuwa moja ya simu nzuri ya bei rahisi kwa mwaka 2022
Ukichungulia sifa zake upande wa memori, betri na display utaona ina ubora wa kukidhi mahitaji ya mtumiaji wa kawaida wa simu
Bei ya redmi 9a ni chini ya laki tatu na inaendana kabisa kwa ubora na sifa zake
Bei ya Redmi 9A Tanzania
Bei ya redmi 9a yenye ukubwa wa GB 32 na ram ya GB 2 ni shilingi 280,000/= kwa maduka ya simu ya mitaa ya Kariakoo
Simu hii inauzwa bei kubwa kwa Tanzania
Kwa sababu bei halisi ya redmi 9a ya gb 32 ni shilingi 210,000/= aliexpress
Na redmi yenye ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4, aliexpress inauzwa 242,000/=
Ukiwa na muda wa kutosha nunua simu aliexpress kuokoa pesa
Kama ilivyosemwa, bei inaendana na sifa zake na usitarajie maubwa kiubora
Sifa za Redmi 9A
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB,32GB na RAM 4GB,2GB |
Kamera | Kamera moja
|
Muundo | Urefu-6.53inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 242,000/= |
Upi ubora wa simu ya Redmi 9A
Ubora wa redmi 9a upo kwenye ukubwa wa memori
Kwani inaruhsu kuhifadhi mafaili mengi kwenye simu
Na betri yake inakaa na chaji muda mrefu
Ikizingatiwa utendaji wake hautumii umeme mwingi
Kioo chake kina resolution yenye unafuu ukilinganisha na simu nyingi zinazouzwa chini ya laki mbili na nusu
Uwezo wa Network
Redmi 9a inakubali aina zote za mtandao wa intaneti isipokuwa 5G
Aina ya 4G ya simu ni LTE Cat 7
Network ya LTE cat 7 inaweza kudownload faili kwa spidi inayofikia 300Mbps sawa na 37.5MBps
Ni spidi kubwa kama mtandao unakupa kasi ya namna hii
Ina network bands za 4G zipatazo 13
Simu inakubali intaneti za 4G za mitandao yote ya simu Tanzania
Ubora wa kioo cha Redmi 9A
Ni simu inayotumia kioo cha IPS LCD.
Kiubora, vioo vya IPS LCD huonyesha rangi chache ukilinganisha na vioo vya amoled
Hilo linasabababishwa na contrast ndogo
Kiasi kinachofanya screen kutokuonyesha baadhi ya vitu kwa rangi halisi mfano rangi nyeusi
Uangavu wa kioo sio mkubwa kwani unafikia 460nits
Unaweza ukapata shida kuona vitu kwenye screen ukiitumia simu kwenye jua kali(ukiwa nje juani)
Nguvu ya processor Helio G25
Ubongo wa simu ya redmi 9a ni processor ya Helio G25
Ni chip ya daraja la mwisho
Ina core nane zilizogawanyika sehemu mbili.
Kiuhalisia core zote zina nguvu ndogo
Kiasi cha kwamba inailazimu simu kucheza gemu kali kwenye resolution ya chini
Si kitu cha kuvutia kwa mpenzi wa magemu
Hii inasababishwa na kitendo cha core zote kuundwa kwa Cortex A53.
Kama umewahi pitia makala zetu nyingi, utakuwa unajua kuwa Cortex A53 ni core maalum kwa kazi ndogo ndogo
Jifunze: Jinsi ya kujua ubora wa processor za simu.
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya redmi 9a ni kubwa na ni aina ya Li-Po
Ukubwa wake ni 5000mAh.
Hii simu inaweza kukaa na chaji masaa mengi sana
Kwa sababu chip yake inatumia umeme kidogo mno
Na haina fast chaji
Hivyo basi itachukua masaa si chini ya matatu kujaza betri kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Simu inatumia memori aina ya eMMC 5.1
Hii ni memori inayoifanya simu kuwa na kasi ndogo ya kuwasha simu kwa haraka na kufungua app kwa spidi.
Kwa sababu eMMC ina kasi ndogo ya kusafirisha data ukilinginasha na memori za UFS
Kuna redmi ya 32GB, 64GB, 128GB na ram 2GB, 3GB, 4GB na 6GB
Kadri memori inavyokuwa kubwa na bei yake inaongezeka
Uimara wa bodi ya Redmi 9A
Bodi yake sio imara na inaweza kupasuka kwa urahisi.
Hiyo inatokana na upande wa nyuma kuwa na plastiki
Na kwenye screen hakuna kioo cha gorilla
Kwa hiyo utahitaji kuweka protector na kava
Hivyo vitu viwili vitaimarisha ulinzi wa bodi ya simu na kuchunika kwa rangi
Simu ni ndefu na ni pana kiasi.
Na ina uzito unaozidi gramu 190
Ubora wa kamera
Simu ina kamera moja upande wa nyuma
Kamera inatumuia teknolojia ya ulengaji aina ya PDAF.
PDAF inafaa ukizingatia na aina ya simu na bei yake
Kamera yake ina HDR japo haiboreshi muonekano wa picha kwa ubora wa juu ukilinganisha na HDR10 au HDR10+
Kamera inaweza kurekodi video za full hd kwa spidi inayofikia 60fps
Ni simu chache sana za laki mbili zenye kamera ya ubora huu upande wa video
Ubora wa Software
Redmi 9a ni simu ya android 10 yenye mfumo wa MIUI 12.
Kuna matoleo mawili mapya ya android 11 na 12, lakini android 10 ina uzuri wake.
Android 10 ina app inayoweza kukuza sauti(sound amplifier)
Huu ni mfumo unaoweza kukata makelele na kukupa usikivu mzuri wa sauti
Kwenye app ya video ya android 10 kuna mfumo unaobadilisha sauti kuwa maandishi (Live Caption)
Video ikiwa inaplay maandishi yanatokea chini ya screen
Redmi 9a inakubali kuwekewa mfumo endeshi wa android 11
Yapi Madhaifu ya Redmi 9A
Simu ina kasoro nyingi kiujumla.
Lakini kumbuka simu za daraja la mwisho huwa ni za bei nafuu zanye ubora wa chini
Ukitazama display, kamera, network, bodi ya simu, spidi ya chaji, aina ya memori na uwezo wa processor na gpu
Utagundua kuwa ni simu ya kiwango cha chini sana
Neno la Mwisho
Kwa mtu mwenye bajeti ndogo kabisa ya simu hii ni simu yenye unafuu kiasi.
Na mtumiaji mpya wa smartphone atafurahia kuwa na hii simu.
Ila kama unataka kamera bora basi hii ni simu ya kuiepuka
Kwa sababu kamera nzuri inahitaji simu yenye utendaji wa juu
Kitu ambacho kinakosekana kwenye simu hii
Mshindani wa redmi 9a ni simu ya Samsung galaxy a13
Ila kiubora galaxy a13 ina utendaji wa juu zaidi na bei yake ni kubwa kiasi
Maoni 3 kuhusu “Ubora na bei ya simu ya redmi 9a (2022)”
Sikujua kipindi na nunua sku soma ila ni nzuru
Napataje kioo cha redmi 9a
Aliexpress vipo vingi hivi