Apple iPhone 7 Plus ni simu janja ya mwaka 2016
Kwa sasa apple hawatengenezi hizi simu, nyingi zilizopo ni simu used
Kitendo kinachoifanya kuwa na bei nafuu ukilinganisha na simu zinazotengenezwa na kampuni ya apple
Kwa mwaka 2023, bei ya iphone 7 plus inatofautiana hata kama ni ya memori moja ila kwa kiwango kikubwa inazidi laki nne
Unahitaji kuitazama hii simu kiundani kuelewa kama inafaa kwa mwaka 2023 na miaka ijayo
Kwani ina miaka zaidi ya sita tangu ilipozinduliwa, huu muongozo utakupa picha kamili
Bei ya iPhone 7 Plus ya GB 128
Hapa Tanzania hasa Dar Es Salaam bei yake yenye ujazao wa GB 128 ni shilingi 500,000/=
Kama ilivyoilezwa awali, unaweza kuipata chini ya hapa inategemeana na eneo na uhitaji wa simu
Hii bei inaendana na matoleo mapya kama Samsung Galaxy A14 5G
Kuna nyanja hii simu inazikalisha simu zinazouzwa kati ya 400,000 mpaka 500,000
Kwa mfano utendaji wa redmi note 12 na Tecno Spark 10 Pro unaachwa na iPhone 7 Plus japo redmi ni ya 2022 na Tecno ni ya 2023
Hii iphone utendaji wake una nguvu unaoendana na nyakati za sasa
Kitu kinachofanya kuwa ni simu inayofaa kutumika 2023 na ukizingatia inapokea matoleo mapya ya mfumo endeshi
Zitazame sifa zake na utagundua hilo
Sifa za iPhone 7 Plus
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,32GB na RAM 3GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-5.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 500,000/= |
Upi Ubora wa iPhone 14 Plus
Simu inatumia chip yenye nguvu inayofanya simu kuwa nyepesi
Inapatikana kwa bei rafiki hata kwa matoleo yenye memori kubwa
Kamera zake zinatoa picha nzuri japo ni simu ya zamani
Inatumia mfumo wa memori unaosafirisha data kwa kasi kubwa
Ina mifumo karibu mitano ya gps kitu kinachofanya usahihi wa taarifa za eneo kuwa mkubwa
Inasapoti pia kasi kubwa ya mtandao wa 4G
Uwezo wa Network
Mtandao wa juu kabisa unaosapoti ni 4G
Mwaka 2016 hakukuwa na 5g hivyo kama 5g ni muhimu kwako basi simu haitokufaa
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 12 ambayo imetumika kwenye simu ya mwaka 2021 ya Redmi Note 10
Kasi ya LTE Cat 12 ni 600Mbps sawa na 75MB/s
Kama unapakuwa video ya MB 75 simu inachukua sekunde moja kumaliza kudownload
Sio spidi kubwa sana ukifananisha na uwezo wa simu za siku hizi
Hata hivyo bado kwa Tanzania sio rahisi kukuta mtandao wa simu za mkononi ukitoa kasi hiyo
Ubora wa kioo cha iPhone 7 Plus
Kioo cha iphone 7 plus ni cha aina ya IPS LCD
Miaka hii apple hawakuwa wanatumia vioo vya OLED
Kioo cha IPS LCD kikiwa na resolution kubwa muonekano wa vitu unakuwa wa kuvutia kiasi cha kwamba unaweza usione tofauti sana na vioo vya amoled
Ndio maana kioo cha hii simu kina resolution ya 1080 x 1920 pixels wakati baadhi ya simu za 2023 zimeweka vioo vya resolution ya 720p
Kwa nyanja hiyo ni kuwa ubora wake kwenye kioo unaridhisha na uendana na simu nyingi mpya zilizotoka hivi karibuni
Ambacho kinachokosekana hapa ni refresh rate kubwa ya kuanzia 90Hz
Refresh rate kubwa hufanya simu kuwa nyepesi(smooth) unapokuwa unatachi kwa kupeleka juu na chini
Nguvu ya processor Apple A10 Fusion
Kwa miaka mingi apple wamekuwa wakiunda processor za simu zenye nguvu zaidi ukilinganisha na kampuni za Snapdragon na Mediatek
Fikiria kuwa Apple A10 Fusion ina miaka sita ila inaizidi chip ya Snapdragon 680 4G iliyopo kwenye simu ya Oppo A96
Kwenye app inayopima nguvu za chip ya Geekbench, apple a10 fusion ina alama zaidi ya 700 kwenye core moja
Hivyo inaifanya simu kuweza kufungua apps nyingi bila na kucheza magemu makubwa mengi japo si kwa kiwango kikubwa kiivyo
Ufanisi wa matumizi madogo ya umeme ni wa kiwango cha kati
Kwa maana chip pia ina matumizi makubwa betri hasa pale unapofanya kazi zinazotumia nguvu kubwa ya processor
Hii chip ina core nne tu tofauti na matoleo mengi ya siku hizi yanayoanzia na idadi ya core sita na kuendelea
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iPhone 7 Plus ina ukubwa wa 2900mAh
Ni betri dogo kiuhalisia
Ukiwa unaongea na simu muda wote betri inakaa kwa masaa 21
Ni muda mdogo na kama ukiwa unaperuzi muda wote simu inakaa masaa 13
Hata hivyo ni muda unaoendana na simu nyingi zilizotoka hivi karibuni
Na pia kumbuka kiwango hicho cha muda ni pale simu ikiwa mpya kabisa
Kwa kuwa sasa hivi utapata iphone used usitegemee kupata muda huo kwani afya ya betri inaweza ikawa imeshuka
Simu haina fast chaji kwa maana upelekaji wake wa chaji ni wa taratibu
Ukubwa na aina ya memori
Kwenye upande wa memori kuna matoleo matatu yenye ukubwa wa 32GB, GB 128 na GB 256 na zote zina RAM ya GB 3
Bei ya GB 32 ni ndogo kwani unaweza kuipata kwa laki tatu na nusu
Aina ya memori simu inayotumia ni NVMe
NVMe huwa inasafirisha data kwa kasi, hii hufanya iPhone kuwa nyepesi
Ila ya GB 32 inaweza ikawa ndogo kwa sababu simu haina sehemu ya memori ya zaida
Hivyo kuhifadhi mafaili ya kutosha itakulazimu uchukue ya kuanzia GB 128
Uimara wa bodi ya iPhone 7 Plus
iPhone 7 Plus ina viwango vya IP67
IP67 inamaanisha simu haiwezi kuingia maji kama ikizama kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa
Ni ishara kuwa simu ina bodi ngumu na imara
Upande wa nyuma imewekewa vioo vya Glasi na upande wa mbele hivyohivyo
Vioo vyake vimeundwa na kampuni ya Corning wanaounda vioo vya gorilla
Simu pia sio ndefu ni fupi kwani ina inchi 5.5
Ni nyepesi kuibeba
Ubora wa kamera
Kwa kiwango cha picha ni cha kuridhisha na kinachuana na simu nyingi za madaraja ya kati
Kwenye mwanga picha zinatoka vizuri ila kuna cha noise (chengachenga) kinaonekana kwa mbali kama ukiikuza picha
Usahihi wa rangi na wa kuridhisha japo si mkubwa
Ila kumbuka simu nyingi bado haziwezi piga picha kwa ubora
Fuatilia: Picha zilizopigwa na simu ya iphone 7 plus
Kiujumla simu ina kamera mbili na zote zina megapixel 12 ambazo zinatosha kabisa kutoa picha nzuri
Kamera ya Telephoto(kwa ajili ya vitu vilivyopo mbali) inatumia optical zoom
Optical zoom huwa inakisogeza kitu cha mbali kwa kutumia lenzi ni sio app
Hii inafanya ubora wa picha kutokupotea tofauti ukizoom kwa kutumia kamera
Ubora wa Software
Wakati inatoka simu ilikuwa inakuja na iOS 10.0.1 ya zamani kwa sasa
Na kadri miaka inavyokwenda kuna iOS zinagoma kutumia baadhi ya apps kama sio zote
Ila iphone 7 plus inakubali kupokea toleo mpaka la iOS 15 inayopatikana kwenye iPhone 13 Pro Max
Hii inakupa uhakika wa kuitumia simu miaka mingi
Japo haipokei toleo jipya la iOS 16, toleo la 15 pia ni zuri na linaipa simu thamani ya muda mrefu
Washindani wa iPhone 7 Plus
Mshindani mkubwa wa iPhone 7 Plus kwanza kabisa ni simu zote za madaraja ya kati yenye 5G
Simu mfano wa Samsung Galaxy A14 5G au Redmi Note 12 Pro 5G zina teknolojia mpya na kamera kali kuliko iPhone 7 Plus
Samsung Galaxy S9 ni simu ya zamani yenye ubora sawa na hii iphone
Neno la Mwisho
Kuna watu wanapenda kumiliki simu za iphone ila bei huwa ni kikwazo
Ni ngumu kupata iphone mpya kabisa kwa shilingi laki tano
Mbadala ni kutumia simu ambazo zimetumika tena za zamani
iPhone 7 Plus inaweza ikawa ni huo mbadala tena kwa bei ya chini
Kumbuka Apple hawaundi tena hizi simu kwa sasa utakazokutana nazo zote kwa wakati huu ni used haijalishi ipo kwenye hali gani
Maoni 11 kuhusu “Bei ya iPhone 7 plus na Nafasi Yake 2023”
Itakaaa kwa muga
Naomba kujua je naweza kupata betri original ya iPhone 7 Plus hapa Dar Es Salaam. Na bei yake ni kiasi gani?
Ngoja nikuangalizie kama betri orijino inapatikana
Nina 400,000, nasaidika vipi kiongozi.
Je, matumizi yake mwisho ni mwaka gani? Ya iPhone 7 plus
Matumizi ya iPhone 7 plus mwisho ni mwaka gani?
Iphone A1784 ya GB 128 ni shilingi ngapi ? Unaeza kuitumia myaka mingapi?
Bila Shaka unazungumzia iPhone 7 Plus, bei yake ni 350,000
Iphone A1784 ya GB 128 ni shilingi ngapi ? Unaeza kuitumia myaka mingapi?
Reply
Matumizi yake mwisho lini
iphone 7 inapokea mpaka toleo la iOS 15.8.1, uhai wake wa kusapoti app bado upo muda mwingi