Ni takribani imefika miezi miwili mpaka tangu iphone 17 pro max
iPhone 17 Pro Max ni moja ya simu kali kabisa iliyopo sokoni kwa sasa
Bei ya iPhone 17 Pro Max kwa hapa Tanzania ni shilingi milioni 4
Hapa kuna swali!
iPhone 16 Pro Max bado ina ubora wa hali ya juu kushinda simu nyingi mpya sokoni
Kwa nini mtu ashawoshike kumiliki simu hii mpya?
Majibu ya sahihi ya hili swali utayapa baada kuelewa sifa kamili za iphone 17 pro max zilizopo hapa
Bei ya iPhone 17 Pro Max (GB 256)
iPhone yenye ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 12 utaipata kuanzia milioni nne
Bei yake kubwa haichagizwi na ukubwa wa memori pekee
Memori ni sehemu ndogo kati ya sehemu nyingi za simu

Japokuwa bei za hii simu hupanda kulingana na ukubwa wa memori
Maana ipo mpaka ya GB 2000 (2TB) ambayo bei yake ni tofauti na hii
Sifa za iPhone 17 Pro Max
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | NMVe, 256GB,512GB,1TB,2TB na RAM 12GB |
| Kamera | Kamera TATU
|
| Muundo | Urefu-6.9inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 4,000,000/= |
Uwezo wa network
Hii simu inakubali aina zote za mtandao
Hivyo ukiwa eneo lenye 5G utapata kasi kubwa ya mtandao
Pia simu inasapoti laini za eSIM
Kwa matoleo ya USA iPhone 17 Pro Max inatumia laini za eSIM pekee
Iwapo utakuwa unatumia toleo la huko hakikisha mtandao unaotumia unakubali laini za eSIM
Ubora wa kioo
Kioo cha hii simu ni cha aina ya oled
Vioo vya oled huwa na kina kikubwa cha rangi
Hivyo huonekana kwa uangavu mkubwa tofauti na vioo ips lcd
Pia kioo kina mwitiko mkubwa unapo-scroll na kutachi

Hii inasababishwa na uwepo wa kitu kinaitwa refresh rate inayofika hadi 120Hz
Uwepo wa teknolojia za Dolby na HDR10 kunaongeza zaidi kina cha rangi
Kwa kifupi ubora wa kioo cha iPhone 17 Pro Max ni mkubwa
Nguvu ya processor ya Apple A19 Pro
Kwenye prosesa za simu kwa wakati huu hakuna inayoifikia Apple A19 Pro kiutendaji na kiufanisi
Kwenye app ya geekbench inayopima nguvu za prosesa apple a19 pro huonyesha uwezo wa kufanya kazi kubwa nyingi
Kwani ina alama zinazokaribia 4000
Ina uwezo wa kufungua kurasa za mtandaoni zipatazo 229 kwa sekunde bila kukwama
Gemu zote zinacheza bila kukwama na kwa utumiaji mdogo wa umeme
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iphone 17 pro max ni ndogo kuliko samsung galaxy s25 ultra
Lakini iPhone 17 Pro Max inakaa sana na chaji kuliko samsung
Hii inasababishwa na ufanisi mkubwa wa prosesa ya Apple A19 Pro
Pia mfumo endeshi ulioundwa vizuri wa iOS
Kasi ya kuchaji sio kubwa kwani kiwango cha juu ni wati 25
Hata hivyo iPhone 17 Pro Max haiji na kichwa cha chaji
Uimara wa bodi
Bodi ya iPhone 17 Pro Max ina uimara mkubwa katika maeneo haya
Kwanza ina cheti cha IP68
Hiki cheti kinaashiria uwezo wa waterproof wa kuzuia maji simu ikizama kwenye kina cha mita 6
Simu haitodhurika kwa muda wa nusu saa
Pia ina skrini prorekta ya Ceramic Shield 2

Protekta hii huweza kuathiriwa mkwarizo iwapo kioo kikikutana na kisu chenye matirio ya chuma
Pia protekta ni imara zaidi pale simu inapodondoka
Hata hivyo umakini ni kitu cha muhimu
Haijalishi simu ipo na aina ipi ya protekta
Ubora wa kamera
Kamera za iPhone 17 Pro Max zinapiga picha nzuri kwenye mazingira yote
Hasa kwenye mazingira ya mwanga mwingi, picha huonyesha usahihi mkubwa wa rangi
Rangi halisi za kinachopigwa picha hutokea kama kilivyo kwa sehemu kubwa

Kwenye mazingira ya mwanga mdogo kuna kiasi fulani cha noise
Hasa kama kitu kipo mbali
Unaweza kuangalia hii picha kwenye linki
Ubora wa Software
Simu za iPhone mpya 2025 zinatumia mfumo endeshi wa iOS 26
Moja ya sifa kubwa ya iOS ni ufanisi wa matumizi ya chaji
Apple wameuunda mfumo wa iOS kutumia vizuri chaji

Ndio maana iphone hukaa na chaji muda mrefu japo betri lake ni dogo
Eneo ambalo apple wameonekana kutopiga hatua kubwa ni AI
Wapo nyuma ukilinganisha na simu za Samsung na Google Pixel
Washindani wa iPhone 17 Pro Max
Ukitazama simu bora duniani utaona vyuma vingine vyenye simu kali
Pitia hii linki simu bora duniani 2025
Kiujumla matoleo ya daraja la juu kutoka samsung, xiaomi, vivo, google, oneplus nk wanatoa simu nzuri
Hivyo washindani ni wengi sana kwenye kitengo chake
Neno la mwisho
Japo iPhone 17 Pro Max ina maboresho kadhaa ila sio maboresho yanayoleta tofauti kubwa na iPhone 16 Pro Max
Kwa mmiliki wa iPhone 16 Pro Max anaweza asihangaike kuipata iphone mpya
Bei yake ni kubwa ila inaendana na sifa zake nyingi inazoambatana nazo