Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series
Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni
Haina tofauti sana na infinix note 30 pro na tofauti yenyewe ipo katika sehemu moja tu upande wa network
Ila bei ya infinix note 30 VIP ni kubwa kiasi na inazidi laki tisa kwa hapa Tanzania
Ni muhimu kuitazama vipengele vyote vya hii infinix kujua kama inakidhi mahitaji yako
Bei ya Infinix Note 30 VIP ya GB 256
Kwa hapa Tanzania infinix note 30 vip yenye RAM GB 8 inauzwa kwa shilingi laki tisa na elfu arobaini (940,000) ikiwa mpya
Bei yake inachagizwa na ubora katika maeneo matatu ambayo ni kioo, memori zenye kasi na kamera na pia uwepo wa wireless chaji ya kasi
Infinix wametumia vioo vyenye ustadi mkubwa wa uonyeshaji vitu
Aina hii ya vioo huchangia gharama kubwa katika uundaji wa simu
Ndio maana hata kioo kikipasuka mtumiaji hulazimika kutoa kiasi kikubwa cha bei kurekebisha kioo cha simu
Sifa za Infinix Note 30 VIP
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Kimo-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 940,000/= |
Ubora wa infinix note 30 vip kiujumla
Infinix hii ina kioo kizuri chenye uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Chaji yake inajaza betri kwa haraka na pia inakaaa muda mrefu na chaji
Inakuja na memori kubwa inayotosheleza kuhifadhi mafaili mengi kwenye simu
Utendaji wake ni wa kuridhisha kutokana na kutumika kwa processor yenye nguvu
Ni simu inayokuja na mtandao wenye kasi
Uwezo wa network
Infinix Note 30 VIP ni simu ya 5G inayosapoti pia 4G yenye kasi
Network yake ina masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu hapa nchini
Kama ilivyo kwa iPhone 15 Pro Max, note 30 vip inakubali 5G za SA(Stand Alone) na NSA(Non Stand Alone)
Kwa maana utaweza kuitumia simu unapotembelea maeneo mengi duniani
Pia simu inatumia 4G aina ya LTE Cat 21 inayoweza kupakua faili kwa kasi inayofika 4700Mbps
Yaani kama unadownload labda sizoni(filamu) ya MB 1,175, filamu itamalizika kudownload ndani ya sekunde mbili
Ila kumbuka kwa hapa Tanzania hakuna mtandao unaotoa kasi hii, na hata ikiwepo gharama yake lazima iwe kubwa
Ubora wa kioo
Kioo cha infinix note 30 vip ni cha aina ya amoled chenye refresh rate inayofika 120Hz
Vioo vya amoled huwa ni vizuri katika uonyeshaji mzuri wa vitu kwani kina uwanda mpana wa rangi
Hivyo vitu vingi huonekana kwa usahihi mkubwa
Kitu kingine kinachoongeza ubora wa skrini ya hii simu ni kuwa na resolution kubwa
Kwa bahati mbaya infinix hawajeka teknlojia ya HDR kwenye kioo
HDR huboresha zaidi muonekano wa vitu kwani huongeza kina cha rangi
Hutopata tabu ya kuona vitu vizuri pindi ukiwa unatumia simu kwenye jua
Kwani uangavu wa kioo unafika nits 900
Nguvu ya processor ya Mediatek Dimensity 8050
Chochote unachokifanya kwenye simu yako basi kinafanyiwa kazi na processor (chip)
Simu ikiwa na chip dhaifu basi jua kuwa simu uliyonayo ni mbaya na yenye uwezo mdogo
Mediatek dimensity 8050 ina nguvu ya kuweza kufanya vitu bila tatizo
Ndio chip ambayo inatumiwa na infinix note 30 vip
Kwenye app ya geekbench inayopima nguvu ya utendaji wa processor, mdeiateek dimensity 8050 ina alama 1100
Kwa chip za kundi la kati hii ni alama nyingi
Japo inaachwa karibu mara mbili na processor iliyopo kwenye samsung galaxy s23 ultra, ila nguvu yake inaweza kucheza magemu bila kukwamakwama
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya infinix note 30 vip ina ukubwa 5000mAh, kwa maana simu inaweza kudumu kwa masaa zaidi ya kumi ukiwa unaperuzi intaneti muda wote
Infinix wameendelea kuimarika katika matumizi ya teknolojia
Ukiwa na hii simu utaweza kuichaji bila kutumia waya wa chaji
Kwani simu inasapoti wireless chaji yenye kasi inayofika 50W, na chaji yake ya waya kasi yake 68W
Kiwango hiki kinaweza kujaza betri kwa 50% ndani ya dakika 30
Ndani ya dakika 70 simu inaweza kujaa kwa 100%
Uwezekano wa kuichaji simu mara moja au mara mbili kwa siku upo,inategemea na matumizi yako
Ukubwa na aina ya memori
Infinix note 30 VIP zipo za aina mbili zinatofautiana kwenye ukubwa RAM
Ukubwa wa memori ni GB 256 ila unaweza kupata yenye ram ya GB 8 au GB 12
Hii simu inatumia memori za UFS 3.1, UFS 3.1 inasafirisha data kwa kasi
Ukiwa unakopi kitu utaona kazi inamalizika ndani ya muda mfupi
Uimara wa bodi ya Infinix note 30 vip
Bodi ya Infinix note 30 vip ina ulinzi wa kuzuia maji ya kiwango cha kunyunyulizika
Haina uwezo wa kuzuia maji pindi ikizama kwenye kina kikubwa mfano ndoo ya lita 20
Ustahimilivu wake upo kwenye kiwango cha maji tiririka kama mvua
Hii inatokana na simu kuwa na viwango IP53
Hata hivyo infinix wameendelea kuboresha uimara wa simu zao
Ila kwa bei yake walipaswa waweke walau IP67
Ubora wa kamera
Infinix note 30 vip ina jumla ya kamera tatu
Kamera kuu ina ukubwa wa megapixel 108, kamera zingine hazijaainishwa ni za aina gani
Hii simu haina kamera ya telephoto wala ultrawide
Kwa kuzitazama vitu vinavyozingatiwa kwenye simu zenye kamera nzuri za bei kubwa, utaona kuwa kuna vitu infinix inavikosa
Ubora wa picha nyakati za mchana ni nzuri kwani kamera inakusanya data kwa kiwango kizuri na vitu vinaonekana kwa uzuri
Upande wa selfie kamera ubora si mzuri sana kwani mng’ao unaopoteza muonekano halisi wa mtu
Hii simu inaweza kurekodi video za 4k kwa kiwango cha 30fps
Ubora wa software
Hii simu inatumia android 13 na XOS 13
Kwa sasa android wameachia toleo jipya la Android 14
Hakuna taarifa kama hii simu itapata toleo jipya
Hata hivyo hakuna tofauti kubwa kati ya android 13 na android 14
Washindani wa Infinix note 30 VIP
Bei ya infinix note 30 vip inaipeleka simu kwenye ushindani na baadhi ya simu za sasmung
Samsung hizo ni Samsung Galaxy A54 na Samsung Galaxy A34
Bei ya Galaxy A54 inaendana na hii infinix
Ila sasa Samsung A54 inaizidi infinix kwenye kila kitu isipokuwa upande wa chaji pekee
Infinix wanahitaji nguvu kubwa kupromoti hii simu kutokana na aina ya bei
Neno la mwisho
Katika orodha ya simu mpya na nzuri za infinix hii ni moja wapo
Kikubwa ni kwamba utahitajika kuwa na kiwango cha kutosha kuimiliki
Kama bajeti ni ndogo basi huna budi kutafuta matoleo mengine yenye unafuu
Maoni 4 kuhusu “Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake”
the best company infinix me and my family we use infinix for communication,,,congratulation to you
Naitaka mnikopeshe nilipage kidogo kidogo
nahitaji kaza hii simu maana huku kwetu hakuna
Unapatikana wapi