Simu ya infinix note 10 pro ni simu iliyotoka katikati mwa mwaka 2021
Pamoja na kupita miezi mingi infinix note 10 pro bado ina ubora unaoweza kushindana na matoleo mapya ya simu za 2022
Itazame sifa ya hii simu upande wa processor, kamera na memori.
Utakachokiona ni sifa zile zile zinazopatikana kwenye simu mpya nyingi za android
Ndio maana hata bei ya infinix note 10 pro haijapungua kivile mpaka sasa.
Bei ya infinix note 10 pro
Bei ya infinix note 10 pro inatofautiana kulingana na ukubwa memori na ram
Infinix note 11 pro ya GB 128 na RAM ya GB 4 inauzwa shilingi 450,000/= kwenye baadhi ya maduka kariakoo
Wakani infinix ya GB 128 na RAM ya GB 8 inauzwa shilingi 630,000/=
Kwa kutazama ubora wake, sifa na washindani wake, simu inaonekana kuwa na bei ya juu kidogo
Sifa za Infinix note 10 pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,64GB,256GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera nne(Infinix macho manne)
|
Muundo | Urefu-6.95inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 450,000/= |
Upi ubora wa Simu ya Infinix note 10 pro
Utaupata ubora wa simu ya infinix note 10 pro kwenye display yake.
Ni nyepesi unapotachi na inakupa ufanisi mkubwa unapocheza gemu
Ina chaji yenye kasi na betri yake inahifadhi umeme muda mrefu
Simu inatumia aina ya memori yenye kasi kubwa kusafirisha data za simu
Ubora wa nyanja zingine umegawanyika, kuna madhaifu na uimara.
Tuzame kiundani kwenye kila sehemu ya simu
Uwezo wa Network
Simu ya infinix note 10 pro inkubali network za aina zote isipokuwa 5G
Simu ina network bands za 4G zinazoshika intaneti ya mitandao yote ya 4G hapa Tanzania
Aina ya 4G iliyotumika ni LTE Cat 12
LTE Cat 12 inaweza kudownload kwa spidi ya juu inayofikia 600Mbps
Kwa bahati hakuna mtandao wa simu unaotoa kasi hii ya 4G hapa nchini
Hii simu ina network bands 13, hivyo itakubali intaneti ya 4G kwenye nchi nyingi hasa za kiafrika
Ubora wa kioo cha Infinix note 10 pro
Kioo cha infinix note 10 pro ni cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz
Vioo vya IPS LCD ni vya bei rahisi ila vina changamoto ya kuonyesha rangi kwa usahihi hasa rangi nyeusi
Refresh rate ya 90Hz inafanya simu kucheza gemu kwa burudani
Simu inakuwa nyepesi.
Kioo chake kina resolution inayoonyesha vitu kwa ustadi,
Kwani resolution yake ina pixels 1080×2460
Nguvu ya processor Helio G95
Processor ya Helio G95 ni chip ya simu ya daraja la kati.
Hii ni processor yenye core nane zilizogawanyika mara mbili
Kiutendaji, chip ina nguvu na inayoifanya infinix note 10 pro kucheza gemu nyingi kwa urahisi
Helio G95 inapata alama za juu pia kwenye app zinazopima nguvu ya processor
Antuntu inaipa chipset alama 342626
Na geekbench inaipa alama 518 kwenye core moja
Aina ya mgawanyo wa core zinaipa uwezo wa juu simu katika kutumia applikesheni ya simu yoyote
Uwezo wa core ndogo
Kuna core kubwa mbili ambazo hutumika kusukuma app zinazohitaji nguvu kubwa
Kila core ina spidi inayofikia 2.05GHz
Utendaji wa core ni wa wastani na unaweza kucheza gemu kubwa kwa resolution tofauti tofauti
Hii ni kwa sababu core zenye nguvu zimeundwa na Cortex A76
Uwezo wa core kubwa
Kuna core ndogo sita zenye spidi inayofikia 2.0GHz
Hizi core zinatumia muundo wa Cortex A55, ni maalumu kwa kazi ndogo ndogo.
Ni muundo unaotumia umeme mdogo zaidi ukilinganisha Cortex A53
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii smartphone ya 2021 ina ukubwa wa 5000mAh aina ya Li-Po
Hili ni aina ya betri inayoweza kutumika muda mrefu bila kuisha chaji kwa haraka.
Chaji yake inapeleka umeme wa kasi unaofikia Wati 33
Ni aina ya chaji itakayoweza kujaza simu kwa haraka chini ya masaa mawili
Ukubwa na aina ya memori
Infinix note 10 pro ina mfumo wa memori unaosafirisha data kwa kasi
Kasi yake ya kuandika data inafika 1200MBps.
Kama unakopi faili la ukubwa wa GB 1.2, simu inaweza kulikopi ndani ya sekunde
Na faida nyingine ya memori za UFS 2,2 ni kuwasha simu kwa haraka
Infinix hii zipo za GB 64 na ram ya GB 6, GB 128 na RAM GB 8, GB 256 na RAM GB 8
Ukubwa wa memori unatosha kuhifadhi app nyingi na mafaili ya kutosha pia
Uimara wa bodi ya Infinix note 10 pro
Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kuzipata taarifa nyingi kuhusu aina ya bodi ya simu kama ni kioo au plastiki.
Kitu cha uhakika simu haijatumia vioo vya gorilla glass ambavyo ni vigumu kuchunika na kupasuka
Bodi yake ni ndefu inayokaribia inchi saba.
Kwa mtu anayependa simu pana basi atafurahia kuwa na hii infinix
Kutokana na simu kuwa ndefu, uzito wake pia umeongozeka
Kwani gramu zake zinafika 209
Ubora wa kamera
Kamera kuu ina sensa yenye resolution ya 64MP
Wingi wa megapixel unaweza kusaidia digital zoom kutopoteza ubora wa picha.
Ikizingatiwa, simu haina telephoto
Kamera zake zinaweza kurekodi video za 4k na full hd kwa spidi ndogo ya 30fps
Kitu kinachokosekana kwenye mfumo wa kamera ni OIS na gyro-eis,
Pia infinix hawajazingatia matumizi ya autofocus bora zaidi kama dual pixel pdaf
Ubora wa Software
Infinix note 10 pro inatumia mufmo wa android toleo la 11.
Na simu inatumia mfumo wa XOS 7.6
XOS 7.6 ina vitu vingi vizuri
Ila moja linaloweza kukuvutia ni uwepo wa app inayoficha taarifa zako za kibenki na password mbalimbali
Kwenye mfumo wa xos kuna app ya Xhide
Xhide inaweza kuficha picha, taarifa za kibenki na mengineyo.
Ili mtu mwingine aangalie taarifa zako atahitaji kukushirikisha
Fahamu zaidi kuhusu mfumo wa XOS 7.6
Yapi Madhaifu ya Infinix note 10 pro
Hii ni infinix yenye ubora mwingi tu hivyo simu ilipaswa itumie vioo bora vya amoled au oled
Baadhi ya simu za laki nne kama redmi note 10 ina vioo vya amoled
Kwenye kamera hakuna kamera ya telephoto
Bei ya infinix note 10 pro inaonekana kuwa kubwa ukilinganisha na ubora wa simu kiujumla
Simu inakosa ulinzi wa kuzuia maji kupenya ndani ya bodi ya simu
Hakuna ishara ya kupokea toleo jipya la android 12
Neno la Mwisho
Hii ni simu moja ya simu bora za infinix kutokana na uwezo mkubwa wa processor
Japokuwa washindani wapo wengi.
Zipo simu za kampuni zingine zenye processor ya Helio G95 na processor zenye nguvu zaidi G95
Baadhi ya hizo simu ni Realme Narzo 30 inayouzwa kwa 520,000/=
Kuna tecno camon 17 pro lakini pia simu ya vivo t1 5g ambayo ina uzuri kuliko hii infinix
Lakini infinix note 10 pro ni moja ya simu nzuri ya infinix yenye kamera nzuri