Bei ya Apple iPhone 17 kwa hapa Tanzania ni shilingi milioni tatu (3)
Hii ikiwa ni iphone yenye ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 8
Sasa basi, kwa nini utumie milioni tatu kwa ajili ya simu wakati Tecno Camon 40 bei yake ni 650k?
Sifa za iphone 17 zitakuonyesha utofauti mkubwa wa iphone na Tecno, pia simu zingine.
Hivyo basi hii post itakufafanulia kila sifa muhimu ya iphone 17
Sifa za Apple iPhone 17
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NMVe,256GB,512GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,000,000/= |
Uwezo wa Network
Apple iPhone 17 inasapoti mitandao ya aina yote
Upande wa laini, inatumia laini za eSIM pekee kwa matoleo ya USA
Kwa nchi zingine zinasapoti laini za kawaida pia
Kwenye kudownload spidi yake inazidi zaidi ya 1000Mbps upande wa 5G
Sina uhakika kama 5G ya hapa Tanzania inasogea kiwango hiko
Kwa uzoefu wangu wa Airtel hufika 300Mbps
Ubora wa kioo cha Apple 17
Apple A17 inakuja na kioo cha LTPO OLED japo apple wanakiita super retina xdr
Ina kina kikubwa cha rangi kutokana na uwepo wa teknolojia za HDR10 na Dolby vision
Pia imewekewa refresh rate ya 120Hz ambayo haikuwepo toleo lililopita
Simu nyingi za Samsung zimekuwa zikitumia LTPO Amoled
Hiki kioo hudhibiti kiwango cha refresh rate kulingana na aina ya matumizi
Maana refresh rate kubwa hutumia umeme mwingi pia hivyo sio nyakati zote utahitaji kutumia 120Hz
Nguvu ya processor Apple A19
Mpaka sasa chip ya Apple A19 inazidiwa na Apple A19 Pro kiutendaji
Kwa mujibu wa app ya Geekbench Apple A19 inafika mpaka alama 3000
Pia hii chip ina ufanisi mzuri wa matumizi ya umeme
Kitu kinachofanya simu kukaa na chaji muda mrefu
Hii inamaanisha shughuli zinazohitaji nguvu kubwa bado hazitumii umeme kupitiliza
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ina ukubwa wa 3692mAh
Ukitazama unaweza kuona ni ndogo
Kiuhalisia simu hii inakaa na chaji muda mrefu na inazizidi hata baadhi ya simu zenye 5000mAh
Ufanisi wa chaji unachagizwa na chip pia mfumo wake endeshi wa iOS 17
Uimara wa bodi ya Apple 17
Bodi ya Apple ni imara na ina uwezo wa kuzuia maji pindi simu ikizama kwenye kina kirefu
Kwa maana ina cheti cha IP68
Hii inamaanisha simu inaweza kuzuia maji hata ikizama kwenye kina cha mita 6
Pia imewekewa kioo cha Ceramic shield 2, hiki kioo kigumu zaidi ku-scratch na himilivu kupasuka kwenye kina cha mita mbili
Lakini hata hivyo vioo ni vioo tu umakini ni muhimu
Ubora wa kamera
iPhone 17 ina kamera mbili zote zikiwa na megapixel 48
Kamera zote zinatoa picha nzuri kwa kiwango kikubwa
Nyakati za mchana na hata mazingira ya mwanga hafifu vitu vinaonekana kwa uzuri
Inaweza kurekodi video za 4K kwa kiwango cha 60fps
Kamera zake zote zinaweza kutuliza mtikisiko wakati unarekodi video huku ukitembea
Hii inasaidiwa na uwepo wa sensor shift IOS
Ubora wa Software
iOS 26 haina tofauti kubwa na mfumo endeshi uliotangulia
iOS 26 inaweza kubadili rangi za icons kwa kuchukua rangi ya kava uliyoweka
Kitu kingine ni uwezo wa kupangalia home icons kwa namna unavyotaka
Mambo mengine ni uwepo wa matumizi ya AI
Japokuwa huku hakuna matumizi makubwa kama Samsung
Washindani wa Apple 17
Mshindani wa kwanza anaweza kuwa ni iPhone 16
Hizi simu mbili hazina utofauti mkubwa sana unaweza mshawishi kujipatia toleo jipya
Ikizingatiwa pia iphone 16 itapata ios 26 muda si mrefu
Pia Samsung Galaxy S25 ni mbadala sahihi
Neno la Mwisho
iPhone 17 ni moja ya simu bora mwaka 2025
Ila kulingana na bei yake unahitaji kuwa na sababu ya msingi sana kununua kama unayo iPhone 16
Kuna mabadiliko madogo sana kwenye toleo jipya
Wazo moja kuhusu “Bei ya Apple iPhone 17 na Sifa zake muhimu”
Maoni yangu kuhusu IPhone 17 kitu gani kipya ambacho mmetuwekea ili niweze kuitambuwa hii iPhone 17 ni sim OG na siyo feki maana wajanja wengi sasa..