Niliposikia toleao jipya la Oppo k10 nikajua itakuwa ina sifa lukuki
Lakini kumbe simu mpya ya oppo k10 ina sifa chache zinazofutia na kushawishi
Kiuhalisia oppo inakuja na chaji yenye spidi kubwa
Display angavu juani
Na uwezo wa kuzuia vumbi kupenya
Ubora mwingine ni wa kawaida kama inavyoonekana kwenye chati za sifa.
Sifa za OPPO K10
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB na RAM 8GB, 6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.59inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 462,178.58/= |
Upi ni ubora wa simu mpya ya oppo k10?
Ukitaka kujua ubora wa oppo K10 tazama kasi yake ya ujazaji wa betri.
Inachukua dakika chache sana simu kujaa
Oppo k10 ina kioo chepesi pale unapotachi.
Kamera yake kuu ina megapixel kubwa apperture ya kamera inapitisha mwanga mwingi
Simu inatumia mifumo ya memori yenye kasi kubwa kusoma na kuandika data
Swali…
Vipi kuhu ubora wa network na chipset.
Fuatilia ubora sifa zingine za oppo k10
Network
Simu mpya ya oppo k10 haina mtandao wa 5G
Na 4g ya simu ina bands chache.
Simu inaweza kudownload faili kwa kasi inayofikia 390Mbps
Kwa sababu aina ya 4G ililyopo kwenye simu ni LTE Cat 13
Kwa Tanzania, 4G ya Halotel na Airtel hazitoshika kwenye hii simu.
Kwa sababu haina bands za 7 na 28
Ubora wa kioo cha oppo K10
Kioo cha oppo a96 ni cha aina ya IPS LCD.
Japokuwa IPS LCD huonyesha rangi chache, lakini resolution yake ni kubwa
Ukubwa wa resolution ya 1080 x 2412 pixels unafanya display ya K10 kuonesha vitu vizuri
Uangavu wa kioo unafika 600nits
Kiwango cha 600nits unaipa screen mwanga wa kuonesha vitu kwa uzuri juani
Kioo cha hii simu ni chepesi ukiwa unaperuzi namba na majina ya simu.
Uwepesi wake unachangiwa na refresh kubwa ya 90Hz
Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G
Simu ya oppo k10 inatumia processor ya simu ya snapdragon 680 4g
Snapdragon 680 4g ina nguvu za wastani
Core kubwa zina kasi inayofikia 2.4GHz
Na core ndogo zina kasi 1.9GHz
Kinachosababisha processor kuwa na nguvu ya wastani ni aina ya muundo iliyo nayo.
Kwani snapdragon 680 4g inatumia Kryo 265.
Tumeeleze uwezo wa snapdragon 680 4g kupitia ukurusa wa Oppo A96
Uwezo wa betri na chaji
Oppo k10 ni simu inayopaswa kukaa na chaji muda mrefu.
Ina betri kubwa lenye ujazo wa 5000mAh.
Simu nyingi za 5000mAh zinaisha chaji baada ya 13 na kuendelea simu ikiwa inatumia intaneti masaa yote
Oppo k1o inakuja fast chaji.
Umeme wa chaji ya oppo unafikia wati 33
Kwa mujibu wa oppo kiasi hiki hujaza simu kwa 50% ndani ya dakika 26
Ukubwa na aina ya memori
Oppo hii mpya inatumia memori za UFS 2.2
Kasi ya kusafirisha data huwa ni kubwa
Kuna aina mbili za oppo k10 upande wa memori
- 128GB na 6GB
- 128GB na 8GB
Ukubwa wa memori huu unaweza kuifadhi mafaili na app nyingi
Uimara wa bodi ya oppo K10
Bodi ya oppo k10 imetengenezwa kwa plastiki
Upande wa nyuma na fremu kote ni plastiki
Kwenye screen ndio kuna kioo lakini sio cha gorilla.
Bodi za plastiki si imara sana kwenye kuzuia michubuko ya rangi
Utahitaji kava na screen protector
Hii simu nzito kutokana na kuwa na uzito wa gramu 189
Ina viwango IP vinavyoonyesha uwezo wa simu kuzuia vumbi
Ubora wa kamera
Kamera za oppo k10 zipo tatu.
Simu haina kamera ya ultrawide na telephoto.
Hivyo kuzoom kunategemea app ya camera.
Kamera yake ina apperture ya f/1.8
Ni aina ya apperture inayopitisha mwanga wa kutosha
Ubora wa video
Oppo k10 inaweza kurekodi video za aina moja.
Video za full hd(1080p)
Na inarekodi video kwa spidi ndogo ya 30fps
Hata selfie kamera inarekodi aina moja tu ya video
Ubora wa Software
Simu mpya ya oppo k10 ni simu ya android 11 yenye software ya ColorOs 11.1
Kitu kimoja kinachovutia kwenye ColorOs 11.1 ni uwezo wa kuunganisha simu na kompyuta
Hautohitaji app ya ziada kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta
App ya music ya colorOs inakupa studio ndogo ndani ya simu.
Inakuwezesha kuhariri rington kwa namna upendavyo
Hii pia inapunguza gharama za kutumia app ya ziada kuedit miziki
Android 11 ina vitu vingi vizuri.
Lakini kuna vitu vipya kama color extraction vilivyopo kwenye android 12
Bei ya oppo K10 Tanzania
Bei ya oppo k10 inafikia shilingi 463,000/= za Tanzania
Bei yake inaoneka ni nafuu.
Lakini kwa n bei hii unapata simu nzuri ya Vivo T1 5G
Vivo T1 5G ina chip yenye nguvu kuliko hii
Yapi Madhaifu ya oppo K10
Kamera za oppo hazitumii teknolojia bora zaidi za kurenga aina ya dual pixel pdaf
Simu haina kamera ya ultrawide kwa ajili ya kupiga picha eneo pana
Processor yake haina nguvu kubwa kiutendaji.
Oppo k10 inatumia bodi za plastiki na sio kioo.
Simu haina kioo cha gorilla glass ambavyo huwa ni vigumu kuchunika na kupasuka.
Teknolojia ya IPS LCD nyakati zake zinaisha.
IPS LCD inapata shida kuonyesha wa rangi nyeusi halisi.
Wakati vioo vya amoled huonesha vizuri.
Network yake ya 4G ina bands chache sana
Simu inakuja na android 11 wakati simu mpya nyingi zina Android 12
Neno la Mwisho
Ukitaka simu inayokaa na chaji muda mrefu oppo k10 ni chaguo sahihi
Kwa mtu ambaye utendaji si kipaumbele hana haja ya kuangalia uwezo wa chip
Lakini kwa mpenzi wa kamera nzuri anapaswa atazame machaguo mengine zaidi.
Kwa bahati mbaya,
Simu zenye kamera nzuri huuzwa bei ghari
Hivyo mnunuaji analazimika kuongeza bajeti
Vinginevyo utapata simu ya uwezo wa kawaida