Samsung Galaxy A18 4G imetoka takribani mwezi mmoja
Bei ya Samsung Galaxy A18 imenifanya nipigwe na butwaa ukilinganisha na sifa zake
Ni simu ya bajeti ndogo ambayo bei yake inaweza kuleta kigingi kwa mteja mpya kuinunua
Sasa hebu tuipatie hii simu kinaga ubaga kwa kufananisha bei yake na sifa za simu za Tecno Spark 50 Pro, Samsung Galaxy A17 4G na Redmi Note 14 Pro
Ukisoma mpaka mwisho utapigwa na butwaa na utajua kama inakufaa ama la.
Kwanza tuanzie na bei.
Bei ya Samsung Galaxy A18 ya GB 128
Samsung Galaxy A18 inauzwa shilingi laki sita (600,000)
Bei hii inakupa galaxy ya GB 128 na RAM ya GB 4
Kabla ya kuzama kwenye sifa zingine kiundani unaona hapa bei ni ukubwa wa memori tayari inaleta maswali
Maana kwa sasa simu zenye hii bei ulikuwa unapata simu ya RAM ya gb 8
RAM ni kitu kimoja kikubwa sana na cha msingi kwenye simu
Pitia hapa kuhusu ram ya simu na umuhimu wake
Ila maajabu yapo hapa kwenye sifa zake. Zipitie
Sifa za Samsung Galaxy A18
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:90Hz |
| Softawre |
|
| Memori | UFS 2, 64GB, 128GB, 256GB na RAM 4GB, |
| Kamera | Kamera TATU
|
| Muundo | Urefu-6.7inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 600,000/= |
Kama inakupa utata tutathmini baashi ya sifa kulingana ma uchunguzi niliofanya kuhusu hii simu.
Uwezo wa network
Kwanza hii simu inatumia laini zile za kawaida na inasapoti laini mbili
Kwa maana haina uwezo eSIM
Ni simu ya 4G haina 5G
Na inasapoti masafa yote yanayotumiwa na mitandao yote ya kampuni za simu
Kiujumla haina tofauti na Samsung Galaxy A17 ama Tecno Spark 40 Pro kwenye eneo hili
Lakini tukija Redmi Note 14 Pro toleo la China lina mpaka 5G lakini yake ipo chini ukilinganisha na hii Samsung
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A18
Kioo cha hii simu kinaonyesha vitu vizuri sana
Ina kina kikubwa cha rangi unaofanya vitu kuwa na muonekano mzuri wa kima kikubwa cha rangi
Hii inasababishwa na simu kuwa kutumia kioo aina cha amoled Super Amoled
Mbali na hilo kina mwitiko wa haraka unapotachi na kuskroll
Lakini haipo fasta sana kama tecno spark 50 pro maana samsung ina refresh rate ya 90Hz wakati matoleo mengine hayo yana 120Hz
Lakini kitu cha muhimu zaidi ni aina ya kioo, samsung kioo chake kizuri na cha gharama
Nguvu ya utendaji ya Exynos 1610
Hapa kuna Samsung Galaxy A18 za aina mbili
Matoleo ya Afrika yanatumia prosesa za mediatek wakati sehemu zingine ni hiyo exynos
Hata hivyo utendaji wake kiujumla ni mzuri
Ila ukubwa wa RAM ya GB 4 wa hii simu ni kizuizi kwa prosesa ya exynos kuweza kufanya kazi kubwa
Maana kama utacheza yale magemu makubwa makubwa yanawahi kujaza RAM
Baada ya muda utaanza kuona simu inakuwa nzito
Ni tofauti na Redmi Note 14 Pro yenye utendaji unaofanana isipokuwa yenyewe ina RAM kubwa ya GB 8
Ubora wa kamera
Samsung Galaxy A18 ina kamera zipatazo tatu
Ubora wa picha ni mzuri hasa katika mazingira yenye mwanga wa kutosha
Ila kuna mazingira inazidiwa na mwanga mwingi hasa kama ukiwa ndani na mwanga wa jua ukawa unaingia ndani labda kupitia dirisha
Ukitazama mazingira ya namna hiyo usahihi wa rangi za mawingu unakuwa sio sahihi hapa utalazimika kutumia HDR
Kwenye mwanga mdogo hasa nyakati za usiku ubora wa picha si mkubwa kwani ukiizoom picha kuna kiwango cha chengachenga(noises) kinaweza kuonekana
Lakini kwenye app ya kamera kuna kitu kinaitwa night mode.
Hii night mode inasaidia kurekebisha picha kiasi zinazopigwa nyakati za usiku
Hii simu haina uwezo wa kurekodi video za 4k. Eneo lingine ambalo linaloleta utata
Bei yake hii inaweza kukupa pia Tecno Camon 40 Pro ambayo inaweza kurekodi video za uangavu mkubwa wa 4k
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Samsung Galaxy A18 ina ukubwa wa mAh 5000
Kimakadirio hii simu inaweza kudumu takribani masaa 13 ukiwa unaitumia muda wote kwa matumizi ya kawaida
Kwa bahati mbaya simu haiji na chaji hivyo utalazimika kununua chaji kama hauna kichwa chake
Kwa kichwa cha wati 25 hii simu inachua hadi lisaa na dakika 30 kujaa kwa 100%
Eneo hili Samsung itakutana na ushindani wa simu mpya za kichina, tena sio kidogo
Simu za china za bajeti siku hizi zina betri za kuanzia mAh 6000
Ubora wa software
Kitu kikubwa ambacho hii simu inajitofautisha na simu zingine ni kipengele cha software
Samsung Galaxy A18 itapata maboresho ya mfumo wa Android kwa miaka 6
Kwa maana ina mfumo wa Android 17 na itapokea hadi Android 23
Hivyo simu itakuwa inapokea vitu vipya na maboresho yatakayoondoa changamoto za kimfumo na kiulinzi
Pia mfumo wake unasapoti uwezo wa kutumia app mbili kwa wakati mmoja
Yaani kwenye skrini inajigawanya sehemu mbili juuu na chini
Upande wa juu unaweza kuwa unatumia WhatsApp na upande wa chini instagram
Neno la mwisho
Hii simu ni nzuri lakini bei yake ni kubwa ukilinganisha na sifa zake
Maana bei ya laki sita unapata simu lali zaidi za matoleo ya miaka miwili iliyopita
Kiujumla hapa Samsung watahitajika kufanya kazi kubwa sana kushawishi watu kuinunua hii simu
Bei kubwa za simu tutaendelea kuzishuhudia kwa miaka kadhaa mbeleni
Hii inasababishwa na makampuni ya AI kununua memori za ram kwa wingi
Hivyo wamesababisha vitu vingi vinavyohitajika na simu kupanda bei