Una bajeti ndogo na unataka simu ya kukidhi mahitaji yako?
Basi hii ni orodha ya simu zipatazo mia moja ambazo za bei nafuu zaidi
Hii orodha inaorodhesha simu kutoka kampuni zifuatazo
- Samsung
- Apple
- Tecno
- Google Pixel
- Infinix
- Itel
- Oppo
- Redmi
- Realme
- Vivo
- Sony
Bei za kila simu zimetokana na bei za Tanzania, na pia simu zingine ni used na matoleo ya kitambo ila ubora wake unaendana na nyakati za sasa
Pitia moja baada ya nyingine uone ipi inakufaa
Samsung Galaxy A04
Kwa sasa unaweza kuipata Samsung Galaxy A04 kwa shilingi laki mbili ya GB 64
Hii ni simu ya kamera mbili na nguvu ya utendaji inafaa kwa vitu visivyohitaji nguvu kubwa
Betri yake ina ukubwa wa mAh 5000
Samsung Galaxy A04s
Samsung Galaxy A04s ya GB 32 inauzwa 180,000
Hii ni simu ya kamera tatu
Utendaji wake unamfaa mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida kwani haina nguvu kubwa
Uzuri wa hii simu inakubali hadi Android 14
Samsung Galaxy A05
Ni simu ya mwaka 2023 na nguvu yake kiutendaji ni ya kuridhisha
Samsung Galaxy A05 ya GB 64 inauzwa shilingi laki tatu (250,000)
Ina kamera mbili na mfumo wake wa chaji unapeleka umeme mwingi hadi wati 25
Ina kamera mbili moja ikiwa na 50MP
Hii inaweza kutumia android 15
Samsung Galaxy A05s
Bei ya Samsung Galaxy A05s kwa sasa ni 280,000
Hii utendaji wake ni mzuri kwa sababu ya kuwa na prosesa ya Snapdragon 680 4G
Ina jumla ya kamera tatu na chaji inaweza kupokea hadi wati 25
Ambayo ni fast charge
Samsung Galaxy A06
Bei ya Samsung Galaxy A06 ni shilingi laki mbili na tisini (290,000)
Kiutendaji simu haina tofauti na Galaxy A05s
Ila hii inaweza kupokea toleo jipya kabisa la android 16
Samsung Galaxy A04e
Samsung Galaxy A04e inauzwa shilingi 200,000 kwa sasa
Utendaji wake sio mkubwa
Ila kama hela yako ni ndogo sana simu hii inaweza kufanya sikue zisogee
Na ni nzuri kwa kuwanunulia wazazi kwa sababu betri yake kubwa
Samsung Galaxy A07
Ni simu ya mwaka 2025 ambayo bei yake ni shilingi 300,000
Utendaji wa hii simu ni mkubwa zaidi ukilinganisha na matoleo yaliyopita
Samsung Galaxy A11
Hii ni simu ya kitambo kidogo imetoka mwaka 2020
Bei yake ya sasa ni shilingi 170,000 ila upatikanaji wake ni changamoto
Haina utendaji mkubwa
Samsung Galaxy A12
Bei ya Samsung Galaxy A12 kwa 2026 ni shilingi 200,000
Lakini na yenyewe haina utendaji mkubwa kwani inazidiwa na hata Samsung Galaxy A06
Ni maalum kwa mtumiaji aliye na matumaizi ya kawaida ya kila siku
Samsung Galaxy A13
Samsung Galaxy A13 ni simu ya mwaka 2022
Bei yake ni shilingi laki mbili ni nusu
Hii simu haina utendaji mkubwa ila imeboreshwa uimara wa bodi
Hasa kutokana na kuwekewa skrini protekta
Tecno Pop 10
Tecno Pop 10 ya GB 64 inauzwa shilingi laki mbili na nusu
Simu hii inakupa utendaji wa wastani hivyo hata baadhi kubwa zinaweza kufunguka settings za kati
Ina kamera moja yenye resolution ndogo ya 8MP, na betri kubwa ya 5000
Kama kamera sio ishu kubwa hili ni chaguo zuri
Tecno Pop 9
Tecno Pop 9 bei yake ni shilingi laki mbili na arobaini (240,000)
Kiutendaji haina tofauti kubwa sana na toleo la pop 10
Pia na yenyewe haitazamiwi kuwa na utendaji mkubwa sana kwani RAM zake ni GB 3 na GB 4
Tecno Pop 8
Tecno Pop 8 ina ufanano sana na Tecno Pop 9
Na bei yake kwa sasa ni shilingi 230,000
Utofauti pekee hii simu inatumia Android ya nyuma ambayo ni Android 13 Go
Hata hivyo utendaji ni wa kuridhisha japo si mkubwa
Tecno Pop 7
Tecno Pop 7 bei yake ya sasa ni shilingi 190,000
Pop 7 inafaa mtumiaji wa intaneti, kupiga simu, kutuma sms na mambo mengine madogo madogo
Vitu ilivyonavyo vinaifanya simu kuwa na utendaji mdogo
Kwa mfano RAM yake ina GB 2 na memori kubwa ni GB 64
Tecno Pop 7 Pro
Tecno Pop 7 Pro bei yake ni shilingi 190,000
Na yenyewe utendaji wake sio na ina kamera moja tu
Tecno Spark Go 2
Bei ya Tecno Spark Go 2 ni shilingi 250,000 ya GB 64
Hii utendaji wake ni mkubwa ukilinganisha na matoleo Pop
Hata hivyo inakuja na RAM ya GB 3 ama GB 4
Kamera yake ni ya kawaida maana ina 13MP
Tecno Spark Go 2023
Tecno Spark Go 2023 bei yake ni shilingi 250,000
Inatumia prosesa ya Helio A22 hivyo utendaji sio mkubwa
Kamera yake ina 13MP na ipo kamera moja tu
Tecno Spark Go 2024
Tecno Spark Go 2024 inauzwa shilingi 280,000
Utendaji wake ni mkubwa ukilinganisha na spark go 2023
Lakini vitu vingine vyote vinafanana havina tofauti na toleo lililopita
Tecno Spark Go 2022
Hii ni simu ya mwaka 2021 na bei yake kwa sasa 180,000
Tecno Spark Go 2022 inatumia Android 11, ni ya kitambo (2021)
Utendaji wake sio mkubwa, na inamfaa mtumiaji wenye matumizi madogo
Tecno Spark Go
Tecno Spark Go ni simu ya 5G ya bei ndogo
Bei ya hii simu ni shilingi laki tatu na nusu, simu nyingi za 5G huanzia laki nne na nusu
Kwa mantiki hiyo utendaji wa hii simu ni mzruri
Na inatumia mfumo endeshi wa Android 15
Infinix Smart 6
Infinix Smart 6 ni simu ya mwaka 2021 bei yake kwa sasa 200,000
Ni simu ya kamera mbili na utendaji wake sio mkubwa
Inakuja na toleo la Android 11
Infinix Smart 6 HD
Hii ilitoka mwaka 2022 na bei yake ni shilingi 220,000
Haina tofauti na smart 6 isipokuwa hii inakuja na RAM ya GB 3 pekee
Kwani Smart 6 iliyopita zipo zenye ram ya gb 2
Infinix Smart 7
Bei ya Infinix Smart 7 ni shilingi 240,000 kwa sasa
Hii simu ina kamera kubwa lakini utendaji wake ni mdogo
Unaweza kupata smart 7 ya RAM ya GB 3 au 4, na memori ya GB 64
Infinix Smart 7 HD
Bei ya Infinix Smart 7 HD ni shilingi 200,000
Utendaji wake ni mdogo zaidi ya Smart 7
Na inakuja ikiwa na RAM ya GB 3 pekee
Infinix Smart 8
Bei ya Samsung Galaxy 8 ni shilingi 240,000
Ni simu ya mwaka 2023, utendaji wake ni wa kuridhisha
Ina kamera moja yenye megapixel 13
Infinix Smart 8 HD
Bei ya Infinix Smart 8 HD ni shilingi 280,000
Hii ni simu kali kati ya hizi za bei nafuu kutoka tekno na infinix
Uwezo wake umechagizwa na uwepo wa mfumo wa memori wenye nguvu wa UFS
Infinix Smart 9
Bei ya Infinix Smart 9 inauzwa shilingi 290,000
Hii pia inakuja na prosesa yenye unafuu
Pia ipo yenye RAM hadi ya GB 6 ila bei yake ni zaidi ya hii
Inatumia mfumo endeshi wa Android 14
Infinix Smart 9 HD
Bei ya infinix smart 9 hd ni shilingi 240,000
Hii imepunguzwa uwezo hasa upande wa RAM na kiutendaji
Hivyo kama una bajeti sio mbaya ukaongezwa
Infinix Smart 10
Infinix Smart 10 inauzwa shilingi 290,000 kwa sasa
Kamera yake ina maboresho kutokana na kuweza kurekodi video za 1444p
Pia kioo kina refresh rate inayofika 120Hz
Infinix Smart 10 HD
Bei ya Infinix Smart 10 HD ni shilingi 250,000
Kiutendaji ubora umepunguzwa
Maana RAM yake ni GB 2 ambayo hufanya simu kuwa nzito ukiwa unafungua vitu kwa waka
Redmi 10
Redmi 10 bei yake ni shilingi 200,000
Na ni simu ya mwaka 2021, ina kamera zipatazo nne
Ila utendaji wake sio mkubwa na RAM zake zina ukubwa wa GB 4 au GB 6
Redmi 10c
Bei ya Redmi 10C inauzwa shilingi 270,000
Hii pia utendaji wake ni wa kuridhisha, inatumia chip ya Snapdragon 680 4G
Pia inatumia mfumo wa memori wa UFS 2 unaosoma data kwa kasi
Ni simu nzuri ya bei nafuu
Redmi 12
Redmi 12 kwa sasa inauzwa 285,000
Utendaji wake hauna tofauti na Redmi 10
Na ina jumla ya kamera tatu kwa maana inakupa machaguo tofauti
Redmi 12C
Redmi 12C bei yake ni shilingi 250,000 kwa wakati huu
Utendaji wake ni mzuri pia na imepunguzwa idadi ya kamera
Kamera yake ina ukubwa wa Megapixel 50
Redmi 13C
Bei ya Redmi 13C bei yake ni shilingi 280,000
Utendaji wake ni wa kuridhisha
Na ni simu ya kamera mbili huku kubwa ikiwa na megapixel 50
Redmi 15
Hii ni simu ya 5G ambayo bei yake ni 400,000 ya GB 128
Ni moja ya simu za 5G ya bei ndogo
Ina kamera mbili na kamera kubwa ina megapixel 60
Redmi 15C
Bei ya Redmi 15C ni shilingi 300,000
Hii simu ina skrini protekta gorilla glass 3
Faida nyingine ya hii simu ni kuwa na betri kubwa la mAh 6000
Redmi 9
Redmi 9 bei yake ni shilingi 170,000 na ni simu ya mwaka 2020
Haina utendaji mkubwa
Hivyo inamuhitaji zaidi mtumiaji wa matumizi ya kawaida
Redmi 9C
Hii simu kwa sasa bei yake inaenda 150,000
Ni ya kitambo hivyo upatikanaji wake sio mkubwa
Na pia utendaji wake ni mdogo na ina kamera tatu
Vivo T4 Lite 5G
Vivo T4 Lite 5G ni simu nyingine ya bei nafuu upande wa 5G
Bei yake ni shilingi 350,000 ya GB 64
Ina kamera mbili na kamera kubwa ina megapixel 50
Utendaji wake unaweza kusukuma vitu vingi
Vivo T3 Lite 5G
Bei ya Vivo T3 Lite 5G ya ukubwa wa GB 128 ni laki nne
Ni simu nyingine ya bei nafuu upande
Japokuwa imetoka mwaka 2024 bado ni simu kali kwa 2026
Vivo Y19 5G
Bei ya Vivo Y19 5G bei yake ni shilingi 350,000
Hii bei itakupa vivo ya ukubwa wa GB 64
Simu ina kamera moja yenye ukubwa wa MP 13
Vivo Y27 4G
Vivo Y27 4G bei yake kwa sasa ni shilingi laki nne
Ni simu ya mwaka 2023 hivyo upatakinaji wake sio mkubwa sana
Utendaji wa hii simu ni wa wastani
Vivo Y36
Hii simu ni ya mwaka 2023 pia ila bei ipo juu kidogo hata kwa sasa
Bei yake ni shilingi 430,000
Inakuja na betri kubwa na chaji yenye kasi inayoweza kuingiza umeme wa wati 44
Vivo Y22 (2022)
Bei ya Vivo Y22(2022) ni shilingi 300,000
Pia utendaji wake ni kiwango cha kulidhisha
Pia kamera yake sio mbaya na zipo kamera tatu
Realme C61
Bei ya Realme C61 ni shilingi 250,000 ya GB 64
Ni simu ya kamera moja na ni simu yenye waterproof ya kuzuia maji ya kunyunyulizika
Utendaji wake sio mkubwa ni wa wastani
Realme C71
Bei ya Realme C7 ni shilingi laki tatu (300,000) ya GB 64
Na yenyewe pia ina kamera moja tu ya MP 50
Hii ina betri kubwa ya 6300mAh na chaji ya 45W
Realme C67 4G
Bei ya Realme C67 4G inauzwa shilingi 450,000
Hii ina chaji inayopeleka umemwe wa wati 33
Inakupa ukubwa wa GB 128 lakini utendaji wake sio kubwa
Realme P1 Lite 5G
Bei ya Realme P1 Lite 5G ni shilingi 450,000
Hii ina kioo cha AMOLED chenye refresh rate 120Hz
Na ukubwa wa memori ni 128GB na RAM ya GB 6
Realme C85
Hii simu ina bonge la betri la ukubwa wa 7,000mAh
Bei yake ni shilingi 500,000
Na yenyewe ina ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4
Realme C75 4G
Bei ya Realme C75 4G inauzwa shilingi 400,000
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 128
Na yenyewe ina bonge la betri la mAh 6000
Realme Note 60X
Realme Note 60X inauzwa shilingi 250,000
Hii haina utendaji mkubwa na RAM yake ina GB 3
Betri yake sio kubwa kama matoleo ya Realme C75
Realme C55
Hii simu bei yake ni shilingi laki tatu ikiwa na GB 64
Ni simu ya kamera mbili
Na chaji yake inaweza kupeleka umeme wa wati 33
Realme P4X
Bei ya Realme P4X ni shilingi 450,000
Ni simu ya 5G na betri ya ukubwa wa 7000mAh
Hii ni bei ya simu ya GB 6 upande wa RAM na memori ya ukubwa wa GB 128
Oppo a18
Hii ni simu ya mwaka 2023 na bei yake ni 350,000
Utendaji wake ni wa wastani ila kamera ya ina megapixel 8
Hii ni bei ya OPPO A18 ya GB 64
Oppo a79
Hii ni simu ya 5G inayouzwa shilingi 500,000
Mfumo wake memori ni ule wenye kasi (ufs 2)
Memori ni GB 128 na RAM GB 4
Oppo a58 4g
Hii ni simu ya kamera mbili ambayo bei yake ni shilingi 400,000
Utendaji wake ni wa wastani
Chaji yake inapeleka umeme hadi wa wati 33
Oppo a59
Oppo A59 ni simu ya mwaka 2023
Bei yake ni 420,000 na utendaji wake ni mkubwa
Na ni simu inayosapoti mtandao wa 5G
Oppo a6c
Oppo A6C ni simu mpya kabisa mwaka 2026
Bei yake ni shilingi laki tatu na nusu
Ni simu ya kamera moja ya 13MP na betri kubwa ya mAh 6500
Oppo a54
Oppo A54 imetoka mwaka 2021
Bei yake ni shilingi 250,000 kwa wakati huu
Ni simu ya kamera tatu ila utendaji wake sio mkubwa
Oppo a55
Oppo A55 pia ni simu ya mwaka 2021
Bei yake pia ni shilingi 250,000
Na yenyewe pia ina kamera tatu lakini haina utendaji mkubwa
Oppo a57 4g
Bei ya Oppo A57 ni shilingi 280,000
Na ilitoka mwaka 2022 ila kiutendaji inafanana na OPPO A55, na A54
Bei yake ni shilingi 270,000
Oppo a78 4g
Oppo A78 ilitoka rasmi mwaka 2023
Kwa sasa bei yake ni shilingi laki tatu na nusu (350,000)
Hii simu ina skrini protekta ya gorilla glass 5 na ina kioo cha amoled
Ambacho huwa na kina kikubwa cha rangi
Oppo a77 4g
Bei ya Oppo A77 4G ni shilingi 350,000
Ilitoka mwaka 2022
Hii simu haina utendaji mkubwa kutokana na kuwa na prosesa ya helio g35
itel zeno 100
iTel Zeno 100 bei yake ni shilingi 250,000
Hii ni simu yenye utendaji mdogo
Inamfaa zaidi mtumiaji mwenye matumizi madogo
iTel A200+
Bei ta iTel A200+ ni shilingi laki tatu
Utendaji wake unaridhisha kiasi fulani
Hii ni simu toleo jipya kabisa kwa mwaka 2026
iTel A200
Bei ya iTel A200 ni shilingi 280,000
Hii inakuja ikiwa na RAM ya GB 3 na memori ya GB 64
Bado utendaji unamfaa zaidi kwa mtumiaji wa kawaida
iTel City 200
Hii ni simu mpya imetoka mwaka 2026
Bei ya hii simu ni shilingi 320,000
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 4
Hii simu ina cheti IP64 waterproof ya maji ya kumiminika
iTel A100C
Bei ya iTel A100C ni shilingi laki mbili na ishirini (220,000)
Ni simu ya kamera moja yenye ukubwa megapixel 5
Na utendaji wake sio mkubwa ni mdogo
iTel A95
Hii ni iTel A95 ya 5G na yenye kamera nzuri
Utendaji wake ni mzuri hasa mfumo wa memori
Inatumia chip yenye utendaji wa wastani ambayo ni Dimensity 6300
Bei ya hii simu ni shilingi laki nne
iTel A90
Bei ya iTel A90 ni shilingi laki mbili na nusu
Hii ni simu ya ukubwa wa GB 64
Ni simu ya 4G na haina utendaji mkubwa na ina vitu vichache vizuri
iTel City 100
iTel City 100 inafanana kiasi fulani na simu ya iTel City 200
Bei ya iTel City 100 ni shilingi 250,000
Utendaji wake ni wa kuridhisha kwa sehemu kubwa
Upande wa kamera pa kawaida sana
iTel Power 70
Hii simu ina utendaji wa kawaida ila ina betri kubwa la mAh 6000
Bei ya hii simu ni shiligni 280,000
Ina baadhi ya vitu vizuri mfano ni memori kubwa ya GB 128
Google Pixel 3
Google Pixel 3 ilitoka mwaka 2018
Ni zamani sana ila hii simu ina oled na ina kamera nzuri sana
Bei yake ni nafuu kwani inauzwa shilingi 320,000
Google Pixel 3a
Bei ya Google Pixel 3a ni shilingi laki tatu
Hii simu inasapoti eSIM
Ila inakuja na memori ndogo ya GB 64 na RAM ya GB 4
Google Pixel 4
Hii ni simu ya kamera mbili, na zote zinapiga vizuri
Ya GB 64 unaweza kuipata kwa shilingi laki nne
Hii simu inaweza kurekodi mpaka video za 4K
Google Pixel 4a
Bei ya Google Pixel 4a ni shilingi 400,000
Hii simu imeongezewa ukubwa wa RAM ya gb 6 ukilinganisha na Pixel 4
Hata hivyo ina kamera moja
Google Pixel 4 XL
Google Pixel 4 XL ni simu ndefu ya inchi 6.3
Pixel 4 na Pixel 4a sio ndefu kama hii xl
Bei yake ni shilingi laki nne na nusu
Google Pixel 5
Hii ni simu inayokuja na kioo cha hdr10+ hivyo ina kina kikubwa cha rangi
Pia ina RAM kubwa ya GB 8 na inapokea hadi android 14
Bei ya hii simu ni shilingi laki nne na nusu
Google Pixel 6
Hii ni simu nyingine yenye RAM ya ukubwa wa GB 8
Ni simu ya kwanza Google kutumia prosesa wanazotengeneza wenyewe
Na pia betri lake kubwa ukilinganisha na matoleo ya nyuma
Bei ya hii simu ni shilingi laki nne na elfu themanini(480,000)
Google Pixel 6a
Bei ya Google Pixel 6a ni shilingi 400,000
Hii imepunguzwa betri ambalo ukubwa wake ni 4410mAh
Na pia imepunguzwa ukubwa wa RAM ambayo ni GB 6 kutoka GB 8
iPhone 6
iPhone 6 inauzwa shilingi laki mbili ikiwa ni used
Hakuna iPhone 6 mpya kwa sasa
Ni simu ya kitambo
iPhone 6s
Bei ya iPhone 6s ni shilingi 250,000
Hii ni simu ya mwaka 2015
Na ni simu ya kwanza kutumia prosesa inayoundwa na apple wenyewe
iPhone 6s Plus
Bei ya iPhone 6s Plus ni shilingi 280,000
Hii imeongezewa ukubwa wa betri na kuwa 2700mAh
Ni ndogo kwa wakati wa sasa
Ila kamera ya hii simu ni nzuri hata kwa wakati huu
iPhone 7
Hii ni simu ya mwaka 2016
Na bei yake kwa sasa ni shilingi 320,000 ya gb 128
Kwa bahati mbaya hii simu inapokea mwisho iOS 15
iPhone 7 Plus
Bei ya iPhone 7 Plus inauzwa shilingi 340,000 ya gb 128
Hii simu ina kamera mbili zenye MP 12
Na kamera zote zinapiga picha vizuri tu
iPhone 8
iPhone 8 inaweza kupokea mpaka toleo la iOS 16
Bei ya hii simu ni shilingi 350,000
Kamera ya hii simu inaweza kurekodi mpaka video za 4K
iPhone 8 Plus
iPhone 8 Plua ya GB 64 na yenyewe inauzwa kwa shilingi 350,000
Hii simu ilianza kuongezwa ukubwa wa betri ambayo ni 2691mAh
Hii simu sio ndefu ina ukubwa wa inchi 5.5
iPhone se
iPhone SE ilitoka mwaka 2016 ikiwa na urefu wa inchi 4.4
Ni simu fupi sana ukilinganisha na simu za sasa
Bei yake ni shilingi laki mbili kwa sasa
iPhone X
Hizi ndizo simu zilionza kuja na mabadiliko makubwa zaidi
Ni simu iliyowekwa kamera inayoweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha 240fps
Bei ya iPhone X kwa sasa ni shilingi laki nne kwa sasa
iPhone XS
Hii ndio iPhone ilyoanza kuja na RAM kubwa
RAM hiyo ina ukubwa wa GB 4
Hii simu inapokea hadi iOS 18 japo kwa sasa kuna iOS 26