SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy S26 Ultra na Sifa Zake Muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

March 16, 2026

Samsung wamezindua simu mpya ya Samsung Galaxy S26 Ultra

Imekuja na upekee fulani lakini hauleti utofauti mkubwa sana na Samsung GalaxyS25 Ultra

Kama ingekuwa ni mimi nisingeona haja ya kubadili simu

Ila kumbuka hayo mabadiliko madogo yana upekee wa kuvutia watu wengine

Tuitazame hii simu kiundani.

Bei ya Samsung Galaxy S26 Ultra

Kwa Tanzania Samsung Galaxy S26 Ultra inauzwa shilingi milioni 3.8

Hii ni bei ya Samsung Galaxy S26 Ultra ya GB 256

Kuna mpaka ya TB 1 na bei yake ni kubwa zaidi

Matoleo yote yana RAM za ukubwa wa GB 12

Na zinazumia mfumo wa memori zenye kasi zaidi wa UFS 4

Sifa za Samsung Galaxy S26 Ultra

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g,5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 8 Elite Gen 5 
  • Core Zenye nguvu(2) – 22×4.74 GHz Oryon V3 Phoenix L
  • Core Za kawaida(6) – 6×3.62 GHz Oryon V3 Phoenix M
  • GPU-Adreno 840
Display(Kioo) Dynamic LTPO AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 16
  • One UI 8
Memori , 256GB,512GB, 1TB na RAM 12GB
Kamera Kamera NNE

  1. 200MP,dual pixel PDAF(wide)
  2. 10MP, Telephoto
Muundo Urefu-6.9inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 300,000/=

Uwezo wa network

Samsung Galaxy S26 Ultra inasapoti aina zote za mitandao

Ukiwa mazingira yenye 5G utaweza kutumia mtandao huo wenye kasi

Na kwenye 4G itatumia aina hiyo ya mtandao

Ukiondoa aina ya mtandao, kwenye hii simu unaweza kutumia laini za eSIM

Hizi ni laini zinazokuwa ndani ya simu na uhitaji kuwa na laini ya plastiki

Ubora wa kioo

Ubora wa kioo ndio eneo lilofanyiwa maboresho makubwa zaidi

Maboresho haya yameleta faragha kwenye kioo

Na pia uwepo wa anti-reflective ambayo imeanza kuwekwa kwenye Samsung S25

Hii inasaidia kioo kuonyesha vitu vizuri pasipo kuludisha mwanga kuelekea kwenye macho

Kioo cha hii simu kinaweza kumzuia mtu wa pembeni asione unachokitazama kwenye simu

Tofauti na hapo mambo mengine yapo sawa

Nguvu ya utendaji

Utendaji wa simu umeongezeka zaidi kutokana na kutumia prosesa mpya

Prosesa hiyo ni Snapdragon 8 Gen 5

Kwenye app zinazopima uwezo wa utendaji zinaonyesha ongezeko la ufanisi zaidi

Hii prosesa ina utendaji mkubwa na inatumia kiasi kidogo cha umeme

Inaizidi hata prosesa za apple katika ufanisi wa utumiaji umeme

Qualcomm hawajaamua kuongeza uwezo wa kiutendaji zaidi bali wamelenga matumizi madogo ya nishati

Uimara wa bodi

Kama kawaida Galaxy S26 Ultra ina waterproof

Hii inaonyeshwa na uwepo wa cheti cha IP68

Ikiwa na maana simu haipitishi maji hata ikizama kwenye kina cha mita 1.5

Lakini kwa muda wa nusu saa

Samsung wamerudi kwenye bodi za Alumiam kutoka kwenye chuma aina Titanium

Ubora wa kamera

Hii simu ina kamera zipatazo nne

Kamera kubwa ikiwa na MP 200 kama tu mwaka uliopita

Hata ubora wa kamera ni jambo la kawida kwenye samsung za bei kubwa

KIujumla hii simu ina kamera nzuri kwenye upigaji picha na kurekodi video

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya Samsung Galaxy S26 Ultra betri lake lina ukubwa wa 5000mAh

Ukiwa kwenye intaneti muda wote betri huchukua masaa 13

Ni tofauti na simu za China sasa hivi

Zinakuja na betri mno mfano ni Xiaomi 17 Pro Max

Hitimisho

Utofauti mdogo kati ya toleo hili na la mwaka jana unaweza ukamzuia mtu kuichukua hii simu

Lakini vitu vichache vipya vimeleta upekee mkubwa

Ubora wa skrini ni wa kiwango kikubwa hasa kwenye utunzaji wa faragha

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Samsung Galaxy A07 na Sifa zake muhimu

Samsung Galaxy A07 ni simu ya bajeti ndogo Ipo ilioyotoka mwaka 2026 na nyingine 2025, hapa tunaiangazia ya mwaka 2025 Bei yake sio kubwa hivyo inaambatana na vitu vizuri vichache […]

infinix hot 60 pro thum

Bei ya Infinix Hot 60 Pro na sifa zake muhimu

Je unajua kuwa simu ya Infinix Hot 60 Pro inaiacha mbali Samsung Galaxy A16? Wakati huo Infinix Hot 60 Pro bei yake iko chini ukilanganisha Samsung Kwenye hii post utafahamu […]

bei ndogo

Simu za laki tatu zenye ubora wa kuridhisha kwa 2025

Iwapo unapanga kununua simu chini ya laki tatu au zisizozidi laki nne usitarajie kupata simu yenye ubora mkubwa Kwa maana usitarajie kamera kali na utendaji mkubwa Ila kwenye hii post […]

infinix note 50 thumb

Ubora wa simu mpya za Infinix Note 50

Katika baadhi ya nchi, Infinix walitoa toleo jipya la Infinix Note 50 Matoleo hayo ni Infinix Note 50 4G Infinix Note 50s Infinix Note 50 Pro 4G Infinix Note 50 […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company