Hii ni orodha ya baadhi ya simu mbalimbali za vivo
Katika kundi hili kuna vivo za bei rahisi na vivo za bei kubwa
Kama hujui kampuni hii hutoa matoleo ya madaraja yote
Kwa hiyo zipo za ubora mkubwa sana na vivo za ubora wa kawaida
Orodha iliyopo inakurahisishia kuchagua vivo kali bila kujali aina ya vivo unayotaka kununua
Vivo Y500 Pro
Vivo Y500 Pro ni simu iliyotoka novemba 2025
Bei yake ni shilingi laki saba (700,000) kwa hapa Tanzania
Bei yake inaakisi ubora katika maeneo matatu yafuatayo

Uimara wa bodi, skrini na utendaji
Upande wa bodi ina cheti cha IP68 waterproof ya kuzuia maji hata simu ikizama kwenye kina kirefu cha mita 1.5
Utendaji wake pia ni mkubwa kutokana na kutumia prosesa ya Mediatek dimensity 7400
Vivo Y19s
Bei ya Vivo Y19s ni shilingi 330,000 kwa hapa Tanzania
Kadri bei ya simuinavyokuwa ndogo ndivyo vitu ubora hupungua
Hii simu ubora upo kwenye uwepo wa waterproof ya IP54
Na pia uwepo wa betri kubwa inayofikia 5500mAh

Na kiasi fulani upande wa kamera sio mkubwa sana
Kiujumla hii simu ni nzuri zaidi kwa mtu mwenye matumizi ya kawaida ya kila siku
Kama ni mpenzi wa kamera, magemu na nguvu kubwa ya utendaji itakulazimu uiangalie vivo inayofuata
Vivo X300 Pro
Vivo X300 Pro ndio vivo bora zaidi kwa wakati huu na yenye ubopra katika vipengele karibu vyote
Hivyo bei yake sio ya kawaida kabisa maana inachuana na iPhone 17 Pro na Samsung Galaxy S25 Plus
Kwa Tanzania bei yake ni shilingi 4,200,000 (milioni nne na laki mbili)

Haya ni baadhi ya maeneo yenye ubora mkubwa zaidi kwenye hii simu
Utendaji wake una nguvu sana kwa sababu ina chip ya Mediatek dimensity 9500
Kamera yake ni kali naweza sema kuliko hata simu zote kwa sasa
Betri yale ni kubwa na kasi ya kuchaji ni kubwa pia
Vivo V60e
Vivo V60e ni simu ya daraja la kati ila bei yake ni shilingi 850,000
Inatumia prosesa yenye nguvu ya wastani ya Mediatek dimensity 7360 Turbo
Hivyo vitu vingi vinafanyika kwa ufanisi bila kukwama kwama

Ina waterproof ya IP68, hata ikizama kwa muda wa nusu saa maji hayataingia ndani ya simu
Pia betri yake ni kubwa ina mAh 6500 japokuwa ukaaji wa chaji bado unacheza kwenye masaa 12
Itakuwa ikipokea android mpya kwa muda wa miaka mitatu mfululizo
Vivo Y31
Vivo Y31 imetoka rasmi septemba 2025 na ni simu ya daraja la kati
Bei yake kwa Tanzania ni shilingi 54o,000
Ubora mkubwa wa hii simu upo kwneye utendaji

Hii inasababishwa na kutumia prosesa aina ya Snapdragon 4 Gen 2
Utendaji wake ni wa wastani ila inaweza kufanya mambo mengi bila shida
Maeneo mengine simu ina uwezo wa kawaida
Vivo Y400
Simu ya Vivo Y400 haina tofauti sana na Vivo Y31
Isipokuwa vivo y400 imewekewa mfumo wa memori zaidi kuliko vivo y31
Bei ya Vivo Y400 ni shilingi 750,000
Pia betri yake ina mAh 6000 ni ndogo kuliko Y31

Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia chip ya Snapdragon 4 Gen 2
Pia inakuja na kioo cha Amoled ambacho huwa na kina kikubwa cha rangi
Vivo Y31 Pro
Simu ya Vivo Y31 Pro inauzwa shilingi 550,000 kwa hapa Tanzania
Inatumia mfumo mwa meoroi wa UFS 3.1 ambao una kasi kubwa ya kuchaji
Pia chaji inapeleka umeme mpaka wa kiwango cha juu cha wati 90

Upande wa memori, inatumia RAM ya GB 8
Vitu vingine simu inafanana tu na vivo y31
Vivo T4 Pro
Bei ya Vivo T4 Pro kwa Tanzania ni shilingi 850,000
Ukiona bei ya kiwango hiki jua simu ina vitu vizuri
Maeneo ambayo Vivo T4 Pro yana ubora mkubwa ni yafuatayo

Kwanza ni simu imara inayoweza kuzuia maji hata ikiwa imezama kwenye maji mengi
Hii inaonyeshwa na simu kuwa na cheti cha IP68 na IP69
Na skrini yake ina kikubwa cha rangi kutokana na uwepo wa teknolojia ya HDR10+